Na Mwandishi Wetu,Dodoma MWANDISHI wa Habari kutoka Star TV Blaya Moses ameshinda kwa kishindo kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) .
Chama hicho kimefanya uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya Katibu Mkuu iliyoachwa wazi miezi michache iliyopita na aliyekuwa Katibu Mkuu Ben Bago ambaye alijiuzulu .
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Leo Disemba 2,2023 katika Ofisi za CPC kufuatia taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wake Musa Yusuf amesema Blaya ameshinda katika nafasi hiyo.
Akitoa matokeo hayo Mwenyekiti huyo amesema"*Kura zilizopigwa 79,_Kura zilizoharibika 0,*Blaya Moses Mase amepata kura 62_,na Daniel Andrew Mkate amepata kura 17_,
"_Hivyo Ndugu Blaya Moses Mase amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa CPC_"amesema Yusuf
No comments:
Post a Comment