Bunge Marathon kujenga shule ya Bunge ya wavula


Published from Blogger Prime Android App


Na Joyce Kasiki,Dodoma

SPIKA  wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson  ameshiriki mbio za Bunge (Bunge Marathon)  ambazo lengo lake ni kuchangia ujenzi wa shule  ya Sekondari ya Bunge ya wavulana.

Akizungumza  katika uwanja wa Jamhuri jijini  Dodoma ,Dkt.Tulia ambaye pia ni Rais wa Bunge la Dunia  (IPU) amesema mbali na kuchangia ujenzi huo pia mbio hizo zinasaidia katika kuimarisha afya za wabunge na wananchi mbalimbali.

Dkt.Tulia ametumia fursa hiyo kuiasa jamii kuendelea na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujikinga dhidi ya maradhi yasuo ya kuambukiza na hivyo kuipunguzia Serikali mzigo wa kumtibu magonjwa hayo .

"Serikali imekuwa nilitumia gharama kubwa kumtibu magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo hivi sasa yamekuwa ni changamoto kutokana namrindo wa maisha ya watu ,lakini kwa kufanya mazoezi ya mara kwa mara tunaweza kujikinga dhidi ya magonjwa haya na tukaipunguzia Serikali gharama katika kuyatibu."amesema Dkt.Tulia

Aidha Dkt.Tulia amefurahishwa na kushiriki wa mzee wa Miaka 91 kukimbia mbio za kilomita 10 na  watoto kuanzia umri wa miaka 5 hadi 11 kukimbia mbio za kilomita 5 pamoja na mlemavu mmoja.

"Huu ni utaratibu mzuri hasa kuanza kuwakinga watoto kujenga utaratibu wa kufanya mazoezi,na hivi ndiyo tunatakiwa kufanya mara kwa mara."alisisitiza Dkt.Tulia

Dkt.Tulia ametumia nafasi hiyo kuwashukuru watu wote walioshiriki mbio hizo huku akisema Bunge linatambua mchango wao huku akisema kula aliyechangia ,jina lake litaandikwa kwa wino wa dhahabu na kihifadhiwa katika shule hiyo.



Share:

Kapinga aeleza Sekta ya Nishati inavyotatua kero za wananchi 


Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki,Dodoma

NAIBU Waziri wa Nishati Judith Kapinga ameeleza mafanikio ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati katika sekta ya Nishati inayojengwa chini ya Serikali ya awamu sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia suluhu Hassan.

Kapinga ameyasema hayo wakati akizungumza baada ya kutembelea mabanda ya maonesho bungeni jijini Didoma katika wiki ya Nishati 2024 kujionea   jinsi Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Wadau wake walivyojipanga kwa ajili ya kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.

"Katika miaka mitatu ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kazi kubwa imefanyika katika Sekta ya Nishati ..,kwa mfano kuna  utekelezaji wa miradi mbalimbali kama vile  Julius Nyerere (JNHPP) ambao umeshaanza kuzalisha umeme, miradi ya usambazaji umeme mijini, vijijini na vitongojini, nishati safi ya kupikia pamoja na sekta ndogo ya Mafuta na Gesi Asilia."amesema Kapinga

Aidha, Kapinga ametumia nafasi hiyo kumshukuru  Spika wa Bunge, Dkt.Tulia Ackson kwa kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Nishati ambao umewezesha Wiki ya Nishati kufanyika kwa umahiri mkubwa

 Ametoa wito kwa  Wabunge  kutembelea Maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma ili kufahamu masuala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali chini ya Serikali ya Awamu ya Sita.


“ Katika mabanda haya tasisi zetu zinaonesha namna gani zinatekeleza miradi mbali mbali yenye mabufaa makubwa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla,hivyo niwaombe na niwakaribishe wabunge kwenye Wiki hii muhimu sana ya Nishati, maana hapa tunatatua kero mbalimbali zinazowasilishwa na  Wabunge na Wananchi watajionea utekelezaji wa miradi katika wilaya zote, majimbo yote na mikoa yote Tanzania.”  Ameema Kapinga

Aidha Naibu Waziri huyo amesema,katika Maonesho hayo Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Nishati pamoja na kampuni zake tanzu zimeshiriki.

Maonesho ya Wiki ya Nishati yameanza April 15 na yanatarajiwa kuhitimishwa April 19 mwaka huu.


Share:

Wizara yajivunia amani na utulivu miaka 60 ya Muungano


Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App




Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki,Dodoma

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt .Stargomena Tax amesema suala la amani na utulivu vilivyopo nchini ni moja ya mafanikio ya kazi iliyofanywa na Wizara yake kupitia  sekta ya ulinzi  katika kipindi cha miaka  60 ya Muungano na hivyo kuifanya Nchi kuwa shwari tangu wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hadi sasa.

Waziri huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kazi zilizofanywa na wizara yake kupitia sekta ya ulinzi katika ipindi cha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar .

 “Katika kulinda mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uhuru, na usalama wa nchi, Wizara kupitia JWTZ imechangia katika kujenga uchumi imara ambapo wananchi hujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali bila hofu. “alisema na kuongeza kuwa

“Yote hayo yamewezekana kutokana na kuwepo kwa sera, sheria, kanuni na mipango madhubuti katika ulinzi wa nchi, vinavyotoa fursa kwa wananchi kujikita katika ujenzi wa Taifa lao. “

Aidha alisema , Serikali kupitia Wizara imeendelea kutekeleza, na kuliimarisha Jeshi kwa kulipatia zana na vifaa bora na vya kisasa, rasilimali watu, na nyenzo za kufanyia mazoezi ili kuwa imara wakati wote.

Pia alisema mchango mwingine mkubwa wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania katika miaka 60 ya Muungano, ni ulinzi madhubuti wa Mipaka ya nchi , Uhuru, na Katiba.

“Mafanikio mengine ni ushiriki wa Wizara kupitia Taasisi zake, hususan Jeshi la Wananch wa Tanzania (JWTZ)  katika kukabiliana na majanga au maafa mbalimbali pale yanapotokea,

 “Katika kutekeleza jukumu hilo, JWTZ imeendelea kushiriki kikamilifu katika kutoa misaada ya uokoaji na ile ya kibinadamu kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.”

 Kwa mujibu wa Waziri huyo , Wizara kupitia JWTZ imeendelea kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika Miradi ya Kimkakati huku akisema baadhi ya maeneo ambayo JWTZ imeshirikiana na Mamlaka za Kiraia ni pamoja na kushiriki katika kuboresha huduma katika Taasisi za Serikali, kushiriki katika ulinzi wa miradi na maeneo ya kimkakati kwa nchi ikiwemo katika migodi mbalimbali, ulinzi wa miundombinu kama Reli, ikiwa ni pamoja na reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR).

Pia ulinzi wa Mradi wa Bwawa la kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (Julius Nyerere Hydro Power Project - JNHPP), ulinzi katika Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Kampuni ya Simu (TTCL), na maeneo ya Viwanja vya Ndege.

 Eneo jingine ni pamoja na utoaji wa huduma za afya na tiba kupitia hospitali za Jeshi za Kanda ambazo ni Lugalo Dar es Salaam, MH Mwanza, Bububu Zanzibar, Mirambo Tabora, MH Arusha, MH Mbeya ambazo hutoa huduma kwa 8 wanajeshi, na pia kwa wananchi waishio maeneo yaliyo jirani na kambi za Jeshi, na katika hospitali nyingine.

Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.