Na Joyce Kasiki,Dodoma
SPIKA wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ameshiriki mbio za Bunge (Bunge Marathon) ambazo lengo lake ni kuchangia ujenzi wa shule ya Sekondari ya Bunge ya wavulana.
SPIKA wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ameshiriki mbio za Bunge (Bunge Marathon) ambazo lengo lake ni kuchangia ujenzi wa shule ya Sekondari ya Bunge ya wavulana.
Akizungumza katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ,Dkt.Tulia ambaye pia ni Rais wa Bunge la Dunia (IPU) amesema mbali na kuchangia ujenzi huo pia mbio hizo zinasaidia katika kuimarisha afya za wabunge na wananchi mbalimbali.
Dkt.Tulia ametumia fursa hiyo kuiasa jamii kuendelea na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujikinga dhidi ya maradhi yasuo ya kuambukiza na hivyo kuipunguzia Serikali mzigo wa kumtibu magonjwa hayo .
"Serikali imekuwa nilitumia gharama kubwa kumtibu magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo hivi sasa yamekuwa ni changamoto kutokana namrindo wa maisha ya watu ,lakini kwa kufanya mazoezi ya mara kwa mara tunaweza kujikinga dhidi ya magonjwa haya na tukaipunguzia Serikali gharama katika kuyatibu."amesema Dkt.Tulia
Aidha Dkt.Tulia amefurahishwa na kushiriki wa mzee wa Miaka 91 kukimbia mbio za kilomita 10 na watoto kuanzia umri wa miaka 5 hadi 11 kukimbia mbio za kilomita 5 pamoja na mlemavu mmoja.
"Huu ni utaratibu mzuri hasa kuanza kuwakinga watoto kujenga utaratibu wa kufanya mazoezi,na hivi ndiyo tunatakiwa kufanya mara kwa mara."alisisitiza Dkt.Tulia
Dkt.Tulia ametumia nafasi hiyo kuwashukuru watu wote walioshiriki mbio hizo huku akisema Bunge linatambua mchango wao huku akisema kula aliyechangia ,jina lake litaandikwa kwa wino wa dhahabu na kihifadhiwa katika shule hiyo.
No comments:
Post a Comment