Wakulima sasa kutambuliwa kibiashara


Published from Blogger Prime Android App




      Na Joyce Kasiki,DODOMA


WAKALA  wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umejipanga kuanza kuwasajili Wakulima kwa kuwapa nembo ambayo itawatambulisha kibiashara.

Afisa Usajili wa BRELA Gabriel Giranangay ameyasema hayo  katika  maonesho ya Wakulima (88) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Wakala huo.

Amesema BRELA inawasaidia wakulima kusajili biashara zao rasmi ili kuwa na usajili wa kampuni, ushirika, au biashara ndogo ndogo zinazohusiana na kilimo na hivyo kufanya biashara kwa ufanisi zaidi.

Aidha amesema usajili wa alama za Biashara  ni muhimu kwa wakulima kulinda jina la bidhaa zao .

Gabriel amesema BRELA hutoa huduma hizo ili kuhakikisha biashara za kilimo zinakubalika kisheria ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za ushauri kuhusu jinsi ya kufuata taratibu za kisheria katika biashara ya kilimo, ikiwa ni pamoja na kanuni za usajili, sheria za biashara, na masharti ya leseni.


"Kwa hiyo mchango wa BRELA ni kuhakikisha inachangia katika kuhakikisha kuwa wakulima wanapata huduma zinazohitajika ili kuendesha shughuli zao za kilimo kwa njia rasmi na kisheria, " amesema

Amesema lengo la BRELA ni kurahisisha mchakato wa usajili, kutoa huduma za leseni, na kuhakikisha kuwa biashara zinakubaliana na sheria na taratibu za nchi.


Aidha amesema huduma kuu zinazotolewa na BRELA ni pamoja na Usajili wa Kampuni,Kusajili kampuni, mashirika, na ushirika ikiwa ni pamoja na kutoa mwongozo na ushauri kuhusu sheria za biashara na taratibu za kisheria.

Xxxxx
Share:

Watakaofanya ununuzi nje ya Mfumo wa NeST kufungwa jela

Published from Blogger Prime Android App



Na Mwandishi Wetu


WATUMISHI wa Serikali watakaofanya ununuzi wa Umma nje ya Mfumo wa NeST watakuwa wamefanya kosa la jinai, na kukabiliwa na adhabu ya kifungo jela pamoja na kulipa faini, kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023.

Akizungumza kwenye kipindi maalum cha Tenda Radio, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Wakili Paul Kadushi, amewataka viongozi wa taasisi za serikali na watumishi kwa ujumla kuzingatia matakwa ya sheria hiyo iliyoanza kutumika Juni 17, 2024 na kanuni zake ambazo zimeanza kutumika Julai 1, 2024.

Kadushi amefafanua kuwa sheria iliyofutwa haikuweka ulazima wa kutumia mfumo wa kielektroniki kufanya ununuzi, hatua iliyosababisha taasisi nyingi kufanya ununuzi nje ya mfumo. 

“Lakini kwa sheria hii mpya [Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023] sasa imeweka sharti la lazima kwa taasisi nunuzi zote kutumia mfumo wa kielektroniki katika kufanya ununuzi,” Wakili Kadushi aliiambia Tenda Radio.
Share:

Kanda ya Kati wakiwa na kampeni ya Sako kwa Bako

Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki,Dodoma
Afisa Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Mtandao wa Tigo Tanzania Isaac Nchunda amesema kampuni hiyo ni moja ya mitandao inayokua kwa kasi na hivyo kurahisisha maisha ya watanzania .

Akizungumza katukanofusi za Tigo jijini Dodoma na waandishi wa habari leo Agosti Mosi,2024 Nchunda amesema katika kuhakikisha kampuni ya Tigo inaendelea kurahisisha maisha ,imepeleka kampeni ya SakoKwaBako ambayo sasa ina miezi miwili tangu ianzishwe.

"Leo tigo ipo kanda ya kati na tumewaletea kampeni ya SakoKwaBako  ambayo sasa ina miezi miwili, ikiwa Kanda ya kati Dodoma Makao Makuu ya nchi na ni siku nzuri ambayo usafiri wa reli ya mwendokasi (SGR) imezinduliwa ,tigo ndiyo mtandao bora zaidi Tanzania kwa sababu tuna teknolojia ya karne ya hivi sasa ya 4G na 5G ,

"Na hapa Dodoma tunayo 5G hivyo tunatoa huduma nzuri kwa wateja wanaotumia mtandao wa Tigo ambapo wanafurahia huduma yenye kasi zaidi ya 5G."amesema Isaac
Amesema SakoKwaBako inatoa bonasi kwa kila mteja  anayenunua bando la tigo anapata MB na dakika za bure.
Amewaasa wananchi wajiunge zaidi na mtandao huo ili wanaufaike na ofa hizo ambapo pia ameizungumzia kampeni yao kupitia simu aina ya ZTE A34 ambapo amesema hiyo ni simu ya kisasa na inapatika kwa unafuu zaidi.
"Simu hii inauzwa shilingi  180,000 lakini pia inatolewa kwa mkopo ambapo mteja atatanguliza kiwango cha awali cha sh.35,000 na atalipa sh.650 kwa siku hadi mteja atakapomaliza deni lake na wakati huo huo anaendelea kutumia simu yake kabla hata ya kumaliza deni lake."amesisitiza

Akizungumzia kuhusu huduma za tigo kwa ujumla amesema, kampuni hiyo inahudumia wateja zaidi ya milioni 21 huku akisema hiyo ni kwa sababu ya ubora wa huduma zake.

"Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) na kwamba Tigo ndiyo mtandao unaokua kwa kasi zaidi nchini. "Amesema

Awali Mkurugenzi wa Kampuni ya Tigo Kanda ya Kati Said Iddy amesema kufuatia umuhimu wa uwepo wa Reli ya SGR ,wananchi wanapaswa kutumia mtandao wa Tigo kwa ajili ya kukata tiketi ya treni hiyo.

Amesema kampuni hiyo imefanya maboresho makubwa ya mtandao wake kwa ajili ya kuboresha mtandao na biashara kwa ujumla kwa kutumia mtandao wa tigo.

Pia amesema Tigo inashiriki maonesho ya wakulima na wafugaji (88 ) viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma huku akiwasihi wananchi wote kutembelea banda la tigo kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.

Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.