Na Joyce Kasiki,DODOMA
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umejipanga kuanza kuwasajili Wakulima kwa kuwapa nembo ambayo itawatambulisha kibiashara.
Afisa Usajili wa BRELA Gabriel Giranangay ameyasema hayo katika maonesho ya Wakulima (88) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Wakala huo.
Amesema BRELA inawasaidia wakulima kusajili biashara zao rasmi ili kuwa na usajili wa kampuni, ushirika, au biashara ndogo ndogo zinazohusiana na kilimo na hivyo kufanya biashara kwa ufanisi zaidi.
Aidha amesema usajili wa alama za Biashara ni muhimu kwa wakulima kulinda jina la bidhaa zao .
Gabriel amesema BRELA hutoa huduma hizo ili kuhakikisha biashara za kilimo zinakubalika kisheria ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za ushauri kuhusu jinsi ya kufuata taratibu za kisheria katika biashara ya kilimo, ikiwa ni pamoja na kanuni za usajili, sheria za biashara, na masharti ya leseni.
"Kwa hiyo mchango wa BRELA ni kuhakikisha inachangia katika kuhakikisha kuwa wakulima wanapata huduma zinazohitajika ili kuendesha shughuli zao za kilimo kwa njia rasmi na kisheria, " amesema
Amesema lengo la BRELA ni kurahisisha mchakato wa usajili, kutoa huduma za leseni, na kuhakikisha kuwa biashara zinakubaliana na sheria na taratibu za nchi.
Aidha amesema huduma kuu zinazotolewa na BRELA ni pamoja na Usajili wa Kampuni,Kusajili kampuni, mashirika, na ushirika ikiwa ni pamoja na kutoa mwongozo na ushauri kuhusu sheria za biashara na taratibu za kisheria.
Xxxxx
No comments:
Post a Comment