Serikali Yaendelea Kuwezesha Vijana Kupata Fursa za Maendeleo – Maganga*


Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App



Na Mwandishi wetu,Mbeya

Serikali chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaendelea kutekeleza mikakati kuhakikisha vijana wanapata fursa sawa za kujiletea maendeleo binafsi na kuchangia katika ustawi wa Taifa kwa ujumla.

Mikakati hiyo inajumuisha uanzishaji wa mifumo ya kitaasisi, kisera, mipango kazi, miongozo na sheria zinazolenga kutatua changamoto zinazowakabili vijana katika nyanja tofauti za kijamii na kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Mary Maganga wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la siku mbili la Vijana Tanzania linalofanyika kuanzia leo 12 Oktoba hadi 13 Oktoba, 2025 Jijini Mbeya katika Ukumbi wa City Park Garden.

Bi. Mary Maganga, amesema lengo la kongamano hilo ni kuwajengea vijana ujuzi na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, kukuza ushirikiano na ubadilishanaji wa mawazo, pamoja na kutambua na kuunga mkono mipango na miradi ya vijana inayolenga kuinua uchumi wao.

“Vijana ni nguvu ya mabadiliko na maendeleo katika jamii zetu. Ni lazima tutumie vema nguvu hii kubadilisha dunia kuwa mahali bora kwa ajili ya wote,” amesema Katibu Mkuu huyo.

Aidha, amewataka vijana kutumia kongamano hilo kama fursa ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto zinazowakabili, ili Serikali iweze kuyachukua maoni yao na kuyatumia kuboresha sera, sheria, kanuni na miongozo kwa manufaa ya Vijana wote nchini.

Sambamba na hilo, Bi. Mary amewahimiza vijana kote nchini kujitokeza kushiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, kwa kuchagua viongozi wanaoakisi matumaini, malengo na ndoto za taifa hili.
Awali Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Rodrick Mpogolo aliwasihi vijana kuendelea kuipenda nchi na kujivunia Taifa la Tanzania kwa kuwa ni mahala ambapo kila kijana ana mchango wa kuleta maendeleo.
Akizungumza kuhusu idadi ya washiriki wa kongaamano hilo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Seleman Mvunye alisema limehusisha zaidi ya vijana 1,500 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na Maafisa Vijana toka Halmashauri zote nchini.

MWISHO.
Share:

Brigaedia Jenerali Ndagala afungua kongamano la wadau wa Usimamizi wa Maafa Mbeya

Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App


 

Wadau watakiwa kutoa mapendekezo yenye tija kuboresha usimamizi wa maafa nchini


Na Mwsnfisho wetu,MBEYA

MKURUGENZI wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Brigedia Jenerali Hosea Ndagala amefungua Kongamano la Wadau wa Usimamizi wa Maafa linalofanyika kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Athari za Maafa kwa mwaka 2025.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo leo 12 Oktoba 2025 jijini Mbeya, Brigedia Jenerali Ndagala aliwataka washiriki kuja na mapendekezo yenye tija katika usimamizi wa maafa.

 “Kongamano hili limekusudiwa kuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto, na kutoa mapendekezo ya kuboresha mifumo ya kitaifa ya usimamizi wa maafa.

Alisisitiza kuwa:”Nitoe wito kwa washiriki wote kushiriki kikamilifu katika mijadala, kwa sababu michango yenu ni muhimu katika kuhakikisha tunapata mapendekezo yatakayokuwa na tija katika usimamizi wa maafa.

Vilevile aliwataka washiriki kutumia fursa hiyo kuimarisha ushirikiano na kubuni njia mpya za kuongeza ustahimilivu wa jamii zetu ili kupunguza athari za maafa na kulinda maisha na mali.

Brigedia Jenerali Ndagala aliwashukuru wadau wote wanaoendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu katika juhudi za kujenga Taifa lenye ustahimilivu dhidi ya majanga.

Alisema mchango wao katika kupanga, kutekeleza, na kufuatilia mipango ya usimamizi wa maafa nchini umeendelea kuwa wa thamani kubwa.

Kwa upande wake, Inspector Damian Muheya kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji amesema kuwa, ili kufanikisha ustahimilivu endelevu usio na maafa, ni muhimu jamii kushiriki kikamilifu katika hatua za kinga na tahadhari dhidi ya majanga.

Naye Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Dkt. Barnabas Msongaleli ameeleza Taasisi yao imeendelea kutoa mchango katika kuzalisha wataalam wa kada ya usimamizi wa maafa nchini ili kuwa na wabobezi wa eneo hili na kuendelea kuleta tija katika masuala ya menejimenti ya maafa. 

“UDOM tumeendelea kutoa elimu, tunaendesha shahada ya awali ya menejimenti ya vihatarishi vya maafa ( Bachelor of Disaster Risk Management). Pia tunafanya tafiti mbalimbali zinazohusu kupunguza au kuzuia vihatarishi  vya maafa. Na kutoa huduma kwa jamii kwa njia ya kuwafikia jamii kuwapa elimu ya vihatarishi vya maafa na namna bora ya kukabiliana na maafa kabla hayajatokea,” alisisitiza Dkt. Msongaleli.

=MWISHO=
Share:

VETA inavyokuza ujuzi wa vijana kwa kuwafundisha Teknolojia mpya ya utengenezaji magari yasiyotumia mafuta


Published from Blogger Prime Android App



Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki, MBEYA

CHUO  cha Ufundi Stadi (VETA) mkoa wa Mbeya kimeonesha ubunifu mkubwa katika teknolojia ya kisasa kwa kuja na mfumo wa mafunzo ya magari ya Hybrid yanayotumia mota za umeme, huku yakipunguza au kuondoa kabisa utegemezi wa mafuta. 

Teknolojia hiyo imewasilishwa katika maonesho ya Wiki ya Vijana kitaifa, yakionesha mwelekeo mpya wa VETA katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya teknolojia duniani.

Mwanafunzi Adam Akyoo kutoka VETA Mbeya ameleza kuwa, mashine hiyo ya Hybrid imeundwa kwa kutumia mota maalum inayoweza kuzalisha umeme na kusaidia gari kusafiri hata pasipo mafuta.

 "Faida kubwa ya mota hii ni kwamba inaweza kuendesha gari bila kutumia mafuta kabisa,inapunguza gharama za uendeshaji na kumrahisishia mtumiaji safari, hasa pale mafuta yanapokatika na sheli ipo mbali," amesema Adam.

Adam amehimiza vijana wa Kitanzania kutumia fursa zilizopo kupitia vyuo vya VETA ambavyo vinaendelea kuimarishwa na serikali ili kuwapa vijana ujuzi wa kujiajiri au hata kuajiri wenzao.

“Tuna 'mode' ya kujifunza kwa vitendo, kila mwanafunzi anapata nafasi ya kujua teknolojia inavyofanya kazi. VETA haitoi tu nadharia, bali inakuandaa kuwa mtaalamu wa kweli wa teknolojia ya kisasa,” ameongeza.

Kwa mujibu wa Afisa Habari na Uhusiano wa VETA, David Mpondyo, teknolojia hiyo mpya ya magari ni sehemu ya juhudi za VETA kufundisha vijana ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la sasa.

 “Tuko kwenye maonesho ya Wiki ya Vijana tukionyesha kile ambacho vijana wanafundishwa kwenye vyuo vyetu. Si wote wanaofika vyuoni, lakini kupitia maadhimisho haya, wananchi wanaweza kuona na kuelewa kile kinachotolewa na VETA,” amesema Mpondyo.

Ameongeza kuwa VETA kwa sasa ina vyuo 80 ambapo kuna chuo katika kila mkoa, na kwamba ujenzi wa vyuo vingine 65 unaendelea katika kila wilaya nchini, juhudi zinazoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ili kuongeza fursa za mafunzo ya ufundi stadi kwa wananchi wote.

Mpondyo amesema pia kuwa VETA imeamua kuandaa vijana kwa ajili ya teknolojia ya magari ya umeme kwa kuwa magari hayo sasa yameanza kuingia kwa kasi nchini. 

“Awali magari yote yalikuwa ya dizeli au petroli, lakini leo magari mengi yanatumia umeme,wateja wakipeleka magari hayo gereji, mafundi wengi wanayaharibu kwa sababu hawana ujuzi huo,ndiyo maana VETA imeamua kufundisha mfumo huu mpya kupitia 'mode' za kisasa,” amefafanua.

Mpondyo amesema, VETA inaendelea kuwa chachu ya maendeleo ya teknolojia na ujuzi nchini, ikiwapa vijana wa Kitanzania fursa ya kuendana na mabadiliko ya dunia na kuwa sehemu ya nguvu kazi yenye maarifa  yanayoendana na wakati .

.

Share:

Mavunde azindua rasmi shughuli za ujenzi wa mgodi wa Madini Kinywe Mahenge



Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App



▪️Rais Samia apongezwa kwa mazingira wezeshi ya biashara

▪️Aitaka Kampuni ya Faru Kutoa Kipaumbele cha Ajira kwa wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi,

▪️Ni Uwekezaji wa zaidi ya Tsh Trilioni 1.3.

▪️Serikali kuvuna zaidi ya shilingi trilioni 7 kama mapato.

▪️Ni Mradi Mkubwa zaidi kuwahi kutokea Mkoa wa Morogoro.


Na Mwandishi wetu Mahenge, Morogoro. 

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Peter Mavunde (MB), amezindua rasmi shughuli za ujenzi wa mgodi wa madini ya graphite wa Kinywe, unaotekelezwa na kampuni ya Faru Graphite Corporation kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania (hisa 16%) na Black Rock Mining Limited (hisa 84%) ikiwa ni hatua kubwa katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya sekta ya madini nchini.

Akizungumza katika hafla iliyofanyika leo tarehe 9 Oktoba 2025 katika eneo la Mahenge, Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro, Mhe. Mavunde amesema uzinduzi huo ni ishara ya kasi mpya ya uendelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati katika Sekta ya Madini, kutokana na maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

“Mradi huu si uchimbaji wa rasilimali pekee, bali ni injini ya maendeleo itakayochochea ukuaji wa viwanda, biashara, ajira, na ustawi wa jamii katika eneo la Mahenge kwa ujumla” amesema Waziri Mavunde.

Kwa mujibu wa Waziri Mavunde, mradi wa Mahenge unatarajiwa kugharimu takribani dola za Marekani milioni 510,(zaidi ya tsh trilioni 1.3)na utazalisha ajira zaidi ya 400 wakati wa ujenzi na zaidi ya 900 ajira za kudumu mgodi utakapoanza uzalishaji kamili. Nje ya mgodi, takribani ajira zisizo za moja kwa moja zaidi ya 4,500 zitachochewa kupitia mnyororo wa thamani wa wachuuzi, wakulima, wasambazaji wa bidhaa na watoa huduma.

Aidha, amesisitiza kuwa, Serikali inatarajia kupata mapato ya zaidi ya dola bilioni 3.2 (zaidi ya tsh trilioni 7) katika kipindi cha uhai wa mgodi, kupitia kodi, tozo, gawio, na mrabaha wa madini.

Akifafanua umuhimu wa madini ya graphite, Waziri Mavunde amesema madini hayo ni miongoni mwa madini muhimu katika utengenezaji wa betri za magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, na paneli za umeme wa jua na kuwa kupitia mradi huo na mengine iliyopo nchhui Tanzania inajiweka kama kitovu cha malighafi za teknolojia safi duniani.

Pia, Waziri Mavunde ameitaka Kampuni ya Faru Graphite Corporation kuzingatia matakwa ya  Ushikishwaji wa Watanzania (local content) na Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kwa kutoa kipaumbele cha ajira kwa Watanzania, hususan wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi, na kutoa fursa kwa makampuni ya ndani kushiriki katika mnyororo wa ugavi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, amemshukuru Waziri Mavunde kwa uongozi na usimamizi wake thabiti katika Sekta Madini, akibainisha kuwa Mkoa wa Morogoro umebahatika kuwa mwenyeji wa miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo huu wa Faru Graphite wenye thamani ya takribani Shilingi Trilioni 1.3.

“Huu ndio mradi mkubwa zaidi kuwahi kutekelezwa katika Mkoa wa Morogoro,” amesema Mhe. Malima, huku akielekeza wataalamu wa mkoa kuandaa semina maalum zitakazowaelimisha wananchi kuhusu fursa za kiuchumi na kijamii zitakazotokana na mradi huo.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga alisema Serikali ilitoa leseni ya uchimbaji mkubwa mwaka 2024, na tayari fidia ya zaidi ya Shilingi Bilioni 13 imelipwa kwa wananchi 254 waliopisha eneo la mradi, ambao pia watajengewa nyumba mpya.

Ameongeza kuwa miundombinu ya umeme wa kilovolt 220 kutoka Mahenge imeanza kuandaliwa ili kuhakikisha mgodi unapata umeme wa uhakika, sambamba na kuanzishwa kwa miradi ya kijamii (CSR) inayolenga elimu, afya na maji.

Kwa upande wake Msajili wa Hazina, Ndg. Nehemiah Mchechu, ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Faru Graphite Corporation, amesema Serikali kupitia ubia huu inalinda maslahi ya taifa, ikinufaika kupitia hisa, kodi, ajira na mzunguko wa fedha.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi na Mwakilishi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Faru na Blackrock Mining, Black Rock Mining Limited, Ndg. Richard Crookes, amesema kampuni yake imejipanga kuhakikisha utekelezaji wa mradi unafuata viwango vya kimataifa vya usalama na uhifadhi wa mazingira, sambamba na kuwekeza katika teknolojia rafiki kwa mazingira na pia wamemshukuru Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi yaliyopokea uwekezaji huo mkubwa Morogoro.
Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.