Bonanza CRDB, wabunge lafana Dodoma


Published from Blogger Prime Android App


Na Joyce Kasiki, Dodoma 


SPIKA wa Bunge  Dkt Tulia Ackson amesema bajeti ya mwaka wa fedha ujao  imegusa wananchi moja kwa moja wakiwemo wanamichezo kwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 280  zitakazo tekeleza mambo mbalimbali kwenye sekta hiyo .

Dkt.Tulia ameyasema hayo kwenye  Bonanza la wabunge lililoandaliwa na Benki ya CRDB ambapo amewataka wanamichezo kuendelea kumuunga mkono Rais  Dkt Samia Suluhu Hassan katika jitihada mbalimbali anazozifanyankwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

"Katika bajeti ijayo sekta yanmichezo ni miongoni mwa sekta ambazo zinetengewa fefha za kutosha kwa lengo la kuimarisha michezo nchini."amesema Dkt.Tulia

Kwanuoande wake Makamu wa pili wa Rais wa Zanziba Hemed Suleiman Abdullah amewataka watanzania kutumia michezo kudumisha Muungano amani na mshikamano kwani Ndio Tunu ya Taifa la Tanzania

Amesema watumishi wa serikali na Wabunge walitumie Bonanza hilo kuimarisha afya zao lakini pia kuwa na desturi ya kufanya mazoezi mara kwa mara.

Katika hatua nyingine ameomba  ushirikia baina ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo michezo. 

"Bonanza hili limefana sana na limenifurahisha niwapongeze sana bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maandalizi na niwasihi kuendeleza ushirikiano baina yenu na baraza la wawakilishi katika masuala mbalimbali kama hivi leo mlivyofanya katika bonanza hili,"alisema. 

Naye Tuli Mwambapa ni Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja Benki ya CRDB amesema Lengo la kufanya Matamasha ni kuwakutanisha viongozi wa serikali na wananchi ambapo pia amewek wazi ujio wa CRDB Marathon ambayo itafanyika agust 18 mwaka huu.

Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni pamoja na  Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Kufukuza Kuku, kupokezana vijiti, kula, kunywa soda, kukimbia na magunia na riadha.
Share:

Wananchi waaswa kujiunga na Bima kujikinga na maafa


Published from Blogger Prime Android App
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Biara George Simbachawene akizungumza alipotembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) kwenye maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umama yanayofanyika jijini Dodoma .


 Joyce Kasiki,Dodoma

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) imewataka wananchi  watumie huduma za bima ili waweze kupata fidia pindi wanapopatwa na majanga mblimbali.

Meneja Utekelezaji ,Sheria na kushughulikia Malalamiko kutoka TIRA Okoka Mgavilenzi 
ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yaliyozinduliwa Juni 19 mwaka huu jijini Dodoma.

Amesema wanqnchi wamekuwa wakimiliki vitu vya thamani lakini hawaoni haja ya kuvikatia bima mwisho wa siku yanapotokea majanga mbalimbali ikiwemo vitu kuungua moto,wengi wao h7baki masikini.

"Wananchi sasa wabadilishe mitazamo ,watumie pesa zao kukata bima ya mali zao ikiwemo nyumba,na vitu vingine vingi kama simu,makochi ili likitokea janga  lolote,waweze kufidiwa."amesema Mgavilenzi

Pia amesema ipo bima ya kilimo ambayo humsaidia mkulima kufidiwa pindi kunapokuwa na mabadiliko ya hali ya hewa huku akitolea mfano uwepo wa mvua za elnino mwaka huu ambazo zimesababisha wakulima wengi kukosa mavuno .

Amewaasa wananchi kuhakikisha wanapeleka malalako yoyote yanayohusiana  na bima ili waweze kuoata haki zao jinsi inavyostahili.

"Sisi TIRA ndio wasimamizi wa bima zote zinazotolewa hapa nchini,hivyo inapitokea shida yoyote kwa mwananchi kucheleweshewa madai yake,kupunjwa fidia,au kutendewa ndivyo sivyo inavyostahili,waje TIRA kwani ndio msaada pekee wa kutatua changamoto hizo."amesema Mgavilenzi."

Awali Meneja Mawasiliano wa TIRA  Khadija Maulid amesema Mamlaka hiyo sasa imepanua wigo wa huduma zake na kwamba sasa wapo katika Kanda 10 ambapo huwezesha huduma ya uelimishaji wananchi kufika hadi vijijini.

Aidha amesema idadi ya watumiaji wa huduma za Bima ineongezeka hadi kufikia milioni 12 mwaka huu kutoka milioni sita mnamo 2021.

Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.