Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Biara George Simbachawene akizungumza alipotembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) kwenye maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umama yanayofanyika jijini Dodoma .
Joyce Kasiki,Dodoma
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) imewataka wananchi watumie huduma za bima ili waweze kupata fidia pindi wanapopatwa na majanga mblimbali.
Meneja Utekelezaji ,Sheria na kushughulikia Malalamiko kutoka TIRA Okoka Mgavilenzi
ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yaliyozinduliwa Juni 19 mwaka huu jijini Dodoma.
Amesema wanqnchi wamekuwa wakimiliki vitu vya thamani lakini hawaoni haja ya kuvikatia bima mwisho wa siku yanapotokea majanga mbalimbali ikiwemo vitu kuungua moto,wengi wao h7baki masikini.
"Wananchi sasa wabadilishe mitazamo ,watumie pesa zao kukata bima ya mali zao ikiwemo nyumba,na vitu vingine vingi kama simu,makochi ili likitokea janga lolote,waweze kufidiwa."amesema Mgavilenzi
Pia amesema ipo bima ya kilimo ambayo humsaidia mkulima kufidiwa pindi kunapokuwa na mabadiliko ya hali ya hewa huku akitolea mfano uwepo wa mvua za elnino mwaka huu ambazo zimesababisha wakulima wengi kukosa mavuno .
Amewaasa wananchi kuhakikisha wanapeleka malalako yoyote yanayohusiana na bima ili waweze kuoata haki zao jinsi inavyostahili.
"Sisi TIRA ndio wasimamizi wa bima zote zinazotolewa hapa nchini,hivyo inapitokea shida yoyote kwa mwananchi kucheleweshewa madai yake,kupunjwa fidia,au kutendewa ndivyo sivyo inavyostahili,waje TIRA kwani ndio msaada pekee wa kutatua changamoto hizo."amesema Mgavilenzi."
Awali Meneja Mawasiliano wa TIRA Khadija Maulid amesema Mamlaka hiyo sasa imepanua wigo wa huduma zake na kwamba sasa wapo katika Kanda 10 ambapo huwezesha huduma ya uelimishaji wananchi kufika hadi vijijini.
Aidha amesema idadi ya watumiaji wa huduma za Bima ineongezeka hadi kufikia milioni 12 mwaka huu kutoka milioni sita mnamo 2021.
No comments:
Post a Comment