Na Joyce Kasiki, Dodoma
SPIKA wa Bunge Dkt Tulia Ackson amesema bajeti ya mwaka wa fedha ujao imegusa wananchi moja kwa moja wakiwemo wanamichezo kwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 280 zitakazo tekeleza mambo mbalimbali kwenye sekta hiyo .
Dkt.Tulia ameyasema hayo kwenye Bonanza la wabunge lililoandaliwa na Benki ya CRDB ambapo amewataka wanamichezo kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika jitihada mbalimbali anazozifanyankwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
"Katika bajeti ijayo sekta yanmichezo ni miongoni mwa sekta ambazo zinetengewa fefha za kutosha kwa lengo la kuimarisha michezo nchini."amesema Dkt.Tulia
Kwanuoande wake Makamu wa pili wa Rais wa Zanziba Hemed Suleiman Abdullah amewataka watanzania kutumia michezo kudumisha Muungano amani na mshikamano kwani Ndio Tunu ya Taifa la Tanzania
Amesema watumishi wa serikali na Wabunge walitumie Bonanza hilo kuimarisha afya zao lakini pia kuwa na desturi ya kufanya mazoezi mara kwa mara.
Katika hatua nyingine ameomba ushirikia baina ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo michezo.
"Bonanza hili limefana sana na limenifurahisha niwapongeze sana bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maandalizi na niwasihi kuendeleza ushirikiano baina yenu na baraza la wawakilishi katika masuala mbalimbali kama hivi leo mlivyofanya katika bonanza hili,"alisema.
Naye Tuli Mwambapa ni Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja Benki ya CRDB amesema Lengo la kufanya Matamasha ni kuwakutanisha viongozi wa serikali na wananchi ambapo pia amewek wazi ujio wa CRDB Marathon ambayo itafanyika agust 18 mwaka huu.
Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni pamoja na Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Kufukuza Kuku, kupokezana vijiti, kula, kunywa soda, kukimbia na magunia na riadha.
No comments:
Post a Comment