Na
Joyce Kasiki
VIJANA nchini wameaswa kujiunga na vyuo vya ufundi VETA vilivyopo nchini ili waweze kupata ujuzi utakaowawezesha kujiajiri au kuajiriwa na kujiunga kiuchumi.
Akizungumza katika.maneosho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye banda la VETA kitengo cha useremala mwalimu Yusuph Mkahala kutoka Chuo cha VETA mkoa wa Tanga amesema VETA ni shule muhimu kwa vijana kwa mustakabali wa maisha yao.
"Nawasihi vijana wake wabunge na VETA ni sehemu sahihi katika maisha yao ambayo itawawezesha kupata ujuzi na kuwa wabunifu wa bidhaa mbalimbali zinatakazowezesha kutatua changamoto katika jamii ambapo na wao wataweza kujiinua kiuchumi kwa kujiajiri wenyewe au kuajiriwa." amesema mwalimu Mkahala
Kuhusu bidhaa walinazo katika banda hilo amesema wametengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutumia vipande vya mbao vilivyobaki kutokankwenye kazi kubwa.
"Kama unavyoona hapa tuna bidhaa zinazotengenezwa kutokana na mbao lakini katika maonesho ya mwaka huu tumewaletea bidhaa zilizotengenezwa na vijana kwa tushirikiane na sisi walimu kwa kutumia vipande vya mbao."amesema mwalimu Mkahala
Amesema bidhaa hizo zipo katika mifumo mikubwa miwili ambayo ni mfumo wa kujikunja ambao kumwezesha mteja kusafirisha kwa urahisi.
Amesema chuo Chao kimeamua kuwafundisha vijana kutumia vipande vidogo vidogo vya mbao ambavyo hutaki wanapofanya kazi kubwa ili kuwafundisha kuwa wabunifu kwa kutumia mpaka kipande kidogo cha mwisho hii ni katika kujiongezea kipato kwa sababu mbao yote dukani imenunuliwa hivyo ili apate ufanisi na kupata faida lazima ahakikishe kila mbao aliyonunua imemuingizia kipato.
Vile vile maesema,wao kama walimu ia wao kama walimu wanaotoa ujuzi na ubunifu mbalimbali kwa vijana wamepata faida ambapo mpaka sasa wawekezaji mbalimbali waliopita kwenye banda lao eneo lao wameomba kuwachukua vijana walioshiriki kutengeneza bidhaa hizo pindi watakapomaliza masomo yao.
Kwa kutumia mbao na vipande vidogo vidogo,vijana hao wametengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo saa za ukutani,meza,stuli,kifaa cha kuwekea sukari,meza na viti vya chakula na meza za kuzungumza (podium).
.
No comments:
Post a Comment