Na Joyce Kasiki,Dar Es Salaam
SERIKALI imesema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu itakuwa imejenga vituo vya kujaza gesi kwenye magari (CNG) maeneo ya Muhimbili, Kibaha, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sinza, Mwenge, Goba, Mbezi Beach na Mbagala .
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felichesmi Mramba alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) huku akisema baadhi ya vituo hivyo vitajengwa na TPDC na vingine sekta binafsi.
"Hili la kuwa na kituo kimoja cha Ubungo Maziwa na Airport tutaachana nalo ndani ya mwaka huu na mwakani, tutakuwa na magari mengi yanazunguka ndani ya jiji ambapo wateja watafikiwa na kujaza gesi,
"Kwa hiyo suala la kujaza gesi kwenye magari tunajaribu kulirahisisha na kadiri inavyowezekana ili kuondoa adha ambayo ipo sasa." Amesema Mhandisi Mramba
Akizungumza kuhusu bomba la mafuta amesema mradi huo umefikia zaidi ya asilimia 30 ambapo hadi sasa kilomita zaidi ya 600 za mabomba zimeshaingia nchini .
Amesema matarajio ya Serikali, hadi kufikia mwishoni mwa 2025 mradinuwe umekamilikq.
Mhandisi Mramba amesema,mkataba rasmi wa kuanza utekelezaji wa mradi huo ulifanyika Februari 2022 na uwekezaji umedhaanza na unatekelezwa kwa kasi .
"Mradi huu umezungumzwa muda mwingi, umeanza kuzungumzwa tangu awamu ya tano, awamu hii ya sita, ni mradi mkubwa unachukua muda mrefu, ujenzi unahusisha usanifu, kulipa watu fidia, kujenga mtambo mkubwa wa kufanya mafuta yasipoe.amesisitiza
Aidha ameitaka kampuni Tanzu ya TPDC ya GASCO kujitangaza zaidi kupitia maonesho ya sabasaba kwani kuna Watanzania wanahitaji huduma ambazo GASCO wanazitoa.
"Tunataka iwe na mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa nchi yetu, eneo ambalo tunataka waongeze ushiriki wao katika uchumi ni eneo la gesi, tunataka gesi iliyopatikana nchini isambae kwa haraka zaidi. Isambae kweney vituo vya kujaza kwenye magari, isambae na majumbani. "
Aidha ametaka sekta binafsinishirikishwe zaidi katika usambazaji wa gesi majumbani na gesi za kwenye magari badala ya kutegemea TPDC peke yake hatua ambayo itachukua muda mrefu kuwafikia Watanzania wengi.
"Lakini tukishirikisha sekta binafsi wakasambaza mabomba kwa ajili ya gesi majumbani, kujenga vituo vingi vya CNG, wakaenda mpaka mikoani gesi hii itasambaa haraka. "Amesisitiza
No comments:
Post a Comment