Na Joyce Kaaiki,Dar es Salaam
USUGU wa vimelea vya Dawa umekuwa ukiongezeka siku hadi siku kutokana na matumizi ya dawa yasiyo sahihi kwa baadhi ya watumiaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar Es Salaam ambapo amewataka
Pia imewataka wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya dawa na kuacha kutumia dawa kiholela bila maelekezo ya wataalamu.
"Katika kuhakikisha dawa zinatumika kwa ufasaha na usahihi wananchi wanapaswa kufuata maelekezo sahihi yanayotolewa na wataalam na ndio maana pamoja na mambo mengine,sisi TMDA timeshiriki maonesho haya pia kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya dawa na kufahamu majukumu ya Taasisi hii."amesema Fimbo
Ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutembelea kwenye banda lao kupata elimu ya udhibiti na matumizi sahihi ya dawa na vitendanishi.
No comments:
Post a Comment