UDOM yaendelea kupanua wigo utoaji elimu ya Juu

Published from Blogger Prime Android App


Na Joyce Kasiki,Dar Es Salaam

CHUO  Kikuu cha Dodoma (UDOM) kinatarajia kufungua kampasi mpya katika Mkoa wa Njombe itakayoanza kutoa mafunzo mwaka wa masomo 2026/2027 kwa lengo la kupanua wigo na kusogeza huduma inayotolewa na chuo hicho kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho  Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Wineaster Anderson wakati akizungumza  na waandishi wa habari  kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam alipotembelea mabanda ya chuo hicho.

Amesema, ujenzi wa kampasi hiyo utatekelezwa kupitia fedha za mradi wa Hits ambapo  kupitia mradi huo chuo kimepokea Dola za Marekani milioni 23 ambapo zinatumika kujenga miundombinu ya madarasa, maabara na kufungua kampasi hiyo mpya katika Mkoa wa Njombe.

Profesa Anderson amesema Kampasi hiyo ya  Njombe itajikita kutoa mafunzo katika eneo la misitu, madini, uvuvi na kuziboresha zaidi sekta zilizoko katika mkoa huo.

Akizungumza kuhusu uwepo wao katika maonesho hayo amesema,wamekuja na bidhaa za kipekee zilizobuniwa na wanafunzi wanaosoma katika chuo Kikuu cha Dodoma.

"Chuo chetu kinafanya ubunifu kupitia tafiti mbalimbali zinazofanywa na watafiti wetu na baada hapo hubuni bidhaa kulingana na tafiti husika ambayo inakwenda kutatua changamoto katika jamii ,hii ninkwa sababu tafitinzetu zimejikita katika jamii."amesema Prof.Anderson

 Xxxxxxc
Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.