Ns Joyce Kasiki Dsr Es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungezi wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Khalfan Khalfan amesema PURA itahakikisha inaongeza wawekezaji kwenye sekta ya utafutaji wa mafuta ili kuongeza tija katika eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara kwenye banda la PURA jijini Dar Es Salaam Mwenyekiti huyo amesema hilo ni jukumu la PURA na kwamba waeekezaji hai lazima watafutwe kiushindani.
"Ili kutekeleza suala la kupata wawekezaji kwa ushindani ,taasisi imekuwa zinafanya matayarisho ya kuwatafuta wawekezaji hao kwa ushindani siyo kwa kuokotwa ,
"Na ili uwapate kwa ushindani tunafanya Duru kwa maana ya kutosha mkutano wa 'kupromote' maeneo halafu wawekezaji wanakuja mkutanoni wanadikiliza sera kisha wanachama maeneo."amesema Profeda Khalfan
Aidha ametaja majukumu makubwa ya PURA kuwa ni pamoja na kumshkuru Esziei wa Nishati maduala ya mkondo wa juu wa Petroli ambao ni utafutaji ,uzalishajina usambazaji wa gesi nchini.
Pia amesema jukumu lingine ni kusimamia ufanisi wa sekta ya utafutaji na uzalishaji pamoja na watafutaji kwa ujumla wake lakini pia kuhakikisha watanzania nao wanashiriki kwenye shughuli za uzalishaji na utafutaji kwenye sekta hiyo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo,jukumu lingine ni kusimamia pale zitakapoanzishwa shughuli za uuzaji wa gesi nje ya nchi huku akitoka mfano mradi ambao Serikali imekuwa ikifanya mazungumzo na wawekezaji huku akisema mazungumzo hayo yanaendelea vizuri.
Amesema mazungunzo hayo yakifanikiwa ,wawekezajinwataweka mtambo wa kuchakata gesi mkoa wa Lindi eneo la Likongo ambapo gesi ile itaenda kuuzwa nje ya nchi.
Aidha ametaja mafanikio yaliyopatikana kwenye gesi asilia kuwa ni pamoja na kuchangia kwa wastani wa asilimia 50 ya Umeme unaozalishwa nchini, kuongeza matumizi ya gesi asilia viwandani, majumbani pamoja na matumizi ya gesi kwenye magari huku watanzania zaidi ya 1,428 wakipata ajira za kudumu na za muda katika miradi ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini na kupunguza changamoto ya ajira nchini.
No comments:
Post a Comment