Na Joyce Kasiki,Dar es Dalaam
WAFUGAJI wa kuku na samaki wamerahisishiwa namna ya kupata chakula cha kuku au samaki kwa kutumia mashine yenye gharama nafuu kutoka chuo cha VETA Songea.
Mwalimu Sussac Mbulu amezungumza katika maonesho ya 48 ya Kinataiga ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo amesema ,kwa kiwa na mashine hiyo mfugaji atatengeneza chakula bora cha mifugo yake na kuifanya kuwa na afya bora.
Amesema wamebuni mashine za aina mbili ambapo moka ni inayotumia mkono na nyingine ya umeme.
Mbulu amesema mashine inayotumia umeme ina uwezo wa kusaga kilogramu 200 za chakula kwa siku huku ya mkono uwezo wake ni kisaga kilogramu 100 kwa siku.
Ametoa rai kwa wanaofuga kuku na samaki kununua mashine hiyo ambayo itamrahisishia katika upatikanaji wa chakula cha mifugo yake.
Vile vile amesema,mashine hiyo itawasaidia hata wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu kiweza kujiajiri wenyewe kwenye eneo la ufugaji wa kuki na samaki.
No comments:
Post a Comment