Mhandisi Mramba aipa tano EWURA

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki,Dar Es Salaam 

KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kwenye maeneo ya gesi asilia ambapo amesaidia  na anaendelea kufuatilia  kutoa leseni kwa wale wanaojenga vituo hasa vya gesi iliyokandamizwa (CNG), pamoja na vituo vya mafuta.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na  Mhandisi  Mramba, alipotembelea banda la EWURA katika maonesho ya 48 ya Kimataiafa ya Biashara Dar es Salaam (DITF),amesema Mamlaka hiyo inasimamia  na kuhakikisha huduma zinazotolewa na vile vituo vinakidhi mahitaji ya jamii.

Mhandisi Mramba huyo amesema jukumu la Wizara ya Nishati ni kuhakikisha kwamba EWURA inafanya kazi yake kulingana na sheria na sera zilizopo na kwamba  wanaiwezesha kutekeleza majukumu yake katika mazingira yanayokubalika ndani ya sekta.

"Tunaendelea kuwatia moyo watanzania kuwa zipo huduma za kiushauri ambazo EWURA inazitoa, zipo huduma za kusikiliza malalamiko na kuyafanyia kazi, amesema Mhandisi Mramba.

 Mkurugenzi Mkuu wa EWURA James Andilile amesema Mamlaka hiyo imeingia mkataba na  Shirika la umeme Tanzania (TANESCO), kwa lengo la kusimamia utendaji kazi wao ili kuboresha utendaji  huo na upatikanaji wa umeme .

Amesema kuwa  kwa sasa Serikali inafanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Nishati ili kuhakikisha sekta hiyo inaimarika.

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.