Matukio katika picha yakionesha Mkuu wa Chuo cha CBE alipotembelea banda la chuo hicho kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) jijini Dar Es Salaam
Na Joyce Kasiki Dar Es Salaam
MKUU wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Profesa Tandi Luoga amesema chuo hicho kimekuja kivingine kwani kimeanza kutoa masters kwa njia mtandao.
Akizungumza alipotembelea banda la Chuo hicho kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar Es Salaam ,Profesa Luoga amesema hatua hiyo inakwenda kumrahisishia mtumishi kusoma bila kuathiri shughuli zake.
Amesema Programu ya mtandaoni imeanza Machi mwaka huu huu huku akisema hii ni kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia katika kurahisisha mambo.
Amesema ,Chuo hicho chenye matawi manne katika mikoa ya Dar Es Salaam ,Dodoma,Mwanza na Mbeya kimefikia maamuzi huo wa masomo mtandaoni ili kutoa wigo mpana hasa kwa watumishi na makundi mengine kujiendeleza kielimu.
"Kwa hiyo kwa sasa tuna wanafunzi wanaoshiriki masomo kwa njia ya mtandao ambapo mahali popote walipo wanapata masomo yao ." Amesema
Amesema mwanafunzi wa Masters anayesoma kwa njia ya mtandao , hahitaji kwenda mpaka CBE Mwanza,Dodoma Mbeya au Dar Es Salaam kusoma isipokuwa wakati wa mitihani ambapo mwanafunzi anaenda kwenye Tawi lolote la chuo hicho lililo karibu naye.
"Hatua hii imesaidia kusambaza elimu ya biashara ndani na nje ya Tanzania, lakini imepunguza gharama kusafiri na malazi kwa mwanafunzi husika." Amesisitiza
Pia amesema chuo hicho kina kozi nyingine nyingi kwa ngazi mbalimbali zikiwemo za mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ambapo katika mafunzo ya muda mrefu wanaotoa elimu kuanzia ngazi ya cheti ,diploma,bachelor na masters .
Ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wote wenye sifa na vigezo kuomba nafasi za masomo katika chuo hicho .
Xxxxxx
No comments:
Post a Comment