Raphael Mwambalaswa fundi seremala asiyeona aliyepata mafunzo VETA
Na Joyce Kasiki, Dar es Salaam
VYUO vya VETA vimedhihirisha umahiri wake katika kufundisha hadi watu wenye ulemavu na kuwatoa katika dimbwi la utegemezi.
Watoto wengi wenye ulemavu wamekuwa wakatiwa tamaa katika jamii ambapo wengi wao hawapelekwi shule.
Mwanafunzi Raphael Mwambalaswa amekuwa kivutio kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ambapo watu wanaofika katika banda hilo wamekuwa wakishangaa namna anavyofanya kazi na uwezo wake katika fani hiyo ya ufundi seremala.
Mwambalaswa ambaye pia ni Mhadhiri Msaidizi katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), amesema aliamua kwenda VETA kwa sababu aliamini wanaweza kumsaidia mtu asiyeona kuweza kujitegemea ndiyo maana aliamua kwenda kujifunza.
Amesema baadhinya watu katika jamiinwamekuwa wakiamini kuwa na ulemavu mtu hawezi kufanya kitu chochote jambo ambalo siyo sahihi.
Kupitia maonesho hayo ameiasa jamii kuhakikisha inawapa elimu watu wenye ulemavu kuanzia wanapokea wadogo na mwishoni siku wawapeleke VETA ndiko ambapo walimu wana ujuzi na umahiri wa kufundishwa watu wenye ulemavu na wakala mafundi Waziri kabisa na hivyo kujitegemea kiuchumi.
Naye Mkufunzi katika Fani ya Useremala Chuo cha Veta Dar es Salaam, Mwalimu Salehe Omary, amesema wana miongozo inayowawezesha kutoa mafunzo kwa watu wenye ulemavu wamekuwa wakiwapa maelekezo ya kuzingatia usalama.
“Moja ya majukumu yetu ni kuhakikisha kila mtu anapata ujuzi awe mwenye uwezo wa viungo au asiye na viungo, nimepata mafunzo ya namna ya kuwahudumia watu wenye mahitaji maalumu. Changamoto aliyonayo mwanafunzi wangu Mwambalaswa (asiyeona) kwangu ilikuwa ni kitu kipya.
“Lakini kwa sababu nina utayari haikuwa shida, mwanafunzi wangu pia alitumika kama mwalimu kwa kunipa mbinu za kumfundisha, zimetufanya mimi na yeye kazi yetu kuwa rahisi.
Amesema mwanafunzi huyo alipofika chuoni hapo walitumia siku mbili kumzungusha katika mazingira yote ya chuo kuanzia anapoingia getini hadi katika karakara ya kujifunzia bila kupata changamoto yoyote
No comments:
Post a Comment