FMJ hardware wapongeza juhudi za Dkt.Samia katika uwekezaji

Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Pichani ni bidhaa za aina mbalimbali zinazopatikana katika maduka ya FMJ Hardware


Na Joyce Kasiki,Dar Salaam

KAMPUNI ya vifaa vya ujenzi FMJ hardware imeipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kwenye sekta ya uwekezaji na biashara na hivyo kuwawezesha hata wazawa kufanya biashara.

 Akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea banda la serous kwenye maonyesho ya 48 ya Kmataifa ya Biashara 77 Jijini Dar es Salaam Afisa masoko,Jacqueline  Yanga amesema wao kama wauzaji na wasambazaji wa vifaa vya ujenzi wamekuja kuonyesha bidhaa bora na zenye viwango vya hali ya juu .

Amesema  serikali ya awamu ya sita imejipambanua kwa sababu imewapa wawekezaji hususan wazawa  wigo mpana kwenye sekta ya uuzaji na usambazaji wa bidhaa mbalimbali zikiwemo za ujenzi .

Ameongeza kuwa FMJ hardware ni kampuni ya kizawa na ipo kwa ajili ya Watanzania wote na hata  kwa nchi jirani  kwa maana ya Afrika mashariki kwani inasambaza vifaa hivyo hadi hizo nchi za jirani.

Ameongeza wapo tayari kuwahudumia wananchi kipindi hiki cha 77 na hata baada ya 77  kwani ofisi zao zipo jijini Dar es laam Buguruni kisiwani.

"Ndugu wananchi wa Dar es laam na viunga vyake mnakaribishwa kwenye banda la serous kuja kujionea bidhaa bora kutoka FMJ HARDWARE", amesema Jacqueline

Ameongeza kuwa kampuni hiyo inasambaza  vya ujenzi vya aina zote.

Xxxxx




Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.