Mkuruhenzi wa PURA Mhandisi Charles
Na Joyce Kasiki ,Dar Es Salaam
MKURUGENZI Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mhandisi Charles Sangweni amesema,Tanzania ina viashiria vya kuwepo mafuta katika wneo la ukubwa wa skweakilomita 534,000.
Akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la PURA katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) Mhandisi Sangweni amesema hayo ni matokeo ya utafiti wa awali huku akisema eneo hilo ni asilimia zaidi ya asilimia 50 ya eneo lote la Tanzania lenye ukubwa wa skwea kilomita karibu 900,047.
"Hapa nchini tumefanya tafiti za awali katika maeneo mbalimbali ,ikumbukwe kwamba nchi yetu ukubwa wake inakava skwea kilomita karibu 900,047, kati ya hizo tafiti tulizofanya maeneo yenye viashiria vya kuwepp mafuta ni eneo la skwea kilomita 534,000 ,
"Sasa hiyo ni karibu asilimia zaidi ya 50 ya eneo lote la Tanzania,lakini katika haya maeneo ambayo yana viashiria vya mafuta au gesi asilia hadi sasa tumefanya yafiti eneo la ukibwa skwea kilomia 160,200.., sasa bado tuna eneo kubwa ambalo tunaamini lina miamba tabata na linaweza kuwa na mafuta hatujafanyia tafiti"amesema Mhandisi Sangweni
Aidha amesema ,mpaka mwishoni mwa mwaka huu au mwaka ujao , wanatarajia kutangaza maeneo mbalimbali ambayo yatavutia wawekezaji kwa ajilli ya kushirikiana na PURA na kampuni yao Tanzu la Shirika la Maendeleo ya Patroli nchini (TPDC) kwenye kutafuta mafuta.
Vilevile amesema kutokana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamefanya Dunia yote inataka kibafilisha mwelekeo kutoka kwenye matumkzi ya nishati chafu na kwenda kwenye matumizi ya nishati safi ,Tanzania nayo ipo kwenye muelekeo huo.
"Tunafahamu kwamba dunia inabadilika,kwenye upande wa nishati dunia yote inaongelea nishati safi na inataka kutoka kwenye nishati hiyo ya petroli kwenda kutumia nishati ya hewa ambayo inazuia uchafuzi wa mazingira ,malengo ni kufika 2060 dunia iwe imefikia kwenye matumizi ya nishati jadidifu kwa kiasi kikubwa."
Amesema,kwa upande wa Tanzania malengo ya kufikia nishati safi ya kupikia kwa hadi asilimia 80 ifikapo 2034 huku akisema kuhama kwenye nishati ambayo inachafua hali ya hewa na kutumia nishati ambayo uchafuzi wake siyo wa kiasi kikubwa au haichafui kabisa.
"Sasa sisi kama watafutaji wa petroli ,ni wadau wakubwa kwenye hilo na katika hili sisi tunafanya tafiti mbalimbali za kuwezesha hili liwezekane,lakini wakati huo tunatafuta kiasi cha gesi ambacho ndiyo tuliyogundua hivi sasa hapa nchini."amesema Mhandisi huyo
Kwa mujibu wa Mhandisi Sangweni ,gesi hiyo itasaidia kutumika majumbani ,kwenye magari na maeneo mengine ya uendeshaji mitambo kwa sababu gesi asilia iliyopo ambayo kwa sasa imegunduliwa Songosongo na Mnazibay imepitishwa duniani kama chanzo cha nishati ambacho kitatumika kwa kipindi cha mpito kuelekea matumizi ya nishati jadidifu .
"Kwa hiyo sisi kama taasisi ya Serikali tunatekeleza hilo kwa kujenga mazingira bora na yanayovutia kwa wawekezaji ambao ndio wenye makampuni wanaokuja kufanya tafiti kwenye eneo hili la mkondo wa juu wa petroli."amesisitiza
Sasa sisi tunadhibiti shughuli A utafutaji hapa nchini
No comments:
Post a Comment