Na Joyce Kasiki,Dar Es Salaam
KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Tigo,imezindua simu mahiri za bei nafuu zaidi ZTE A34 kwa ushirikiano na ZTE Tanzania kupitia Sako kwa Bako na Simu janja kwa Mpango kampeni.
Meneja wa Kifaa wa Tigo Imelda Edward amezungumza jijini Dar Es Salaam kwenye maonesho ya Sabasaba Julai 4 mwaka huu huku akisema uzinduzi huo ni mwendelezo wa Tigo wa kuunganisha watu ambao hawajaunganishwa na mtandao wa Tigo kuwapa fursa ya kufurahia mtandao ulioboreshwa na mpana zaidi wa 4G nchini.
"Kwa kutoa simu janja ya bei nafuu ya ZTE A34 kwa bei ya chini kabisa ya TZS 650/- kwa siku kupitia kampeni yetu ya Sakokwa Bako na SimujanjakwaMpango inawapa wateja wetu fursa ya kupata huduma ya Tigo."amesema Imelda
Amesema hii ni katika kuhakikisha kila mtanzania anafaidika na fursa zinazoletwa na muunganisho wa kidijitali.
“Hii ni furaha kwa Tigo maana kwenye jalada letu la ufadhili wa kifaa linaloitwa Sako kwa Bako na simu janja kwa Mpango wa kampeni Kifaa hiki kitapatikana katika sehemu zetu zote za mguso na chaguo rahisi za malipo ambapo wateja wanaweza kuchagua mpango wa miezi 12, ambao unahitaji amana ya awali ya TZS 35,000 na marejesho ya jumla ya kila siku ya TZS 650 kwa muda wa siku 365,lakini pia ZTE A34 inapatikana kwa bei ya pesa taslimu TZS 180,000.” amesisitiza Imelda
Amewaalika wateja wote na wapenda teknolojia kujumuika nasi katika Banda la Tigo la Saba Saba na maduka yote ya Tigo kote nchini ili kujionea moja kwa moja simu mahiri za ZTE A34.
No comments:
Post a Comment