Mkurugenzi Mkuu VETA aeleza umuhimu wa VETA

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki,Dar es Salaam

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Anthony Kasore amepongeza juhudinza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kujenga vyuo vingi vya VETA ambapo hadi kufikia 2025 kutakuwa na idadi ya vyuo takriban 145 vitakavyokuwa katika wilaya zote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam kwenye Banda la VETA,Mkurugenzi huyo amesema lengo la Dkt.Samia na Serikali kwa ujumla no kuhakikisha kila eneo lenye wahitimu wa VETA kunakuwa na nyenzo rahisi zinazoweza kutatua changamoto za jamii husika.

"Nia ya vyuo hivinsiyo kujenga tu ,bali ni kwa shughuli maalum ya kupata wataalam wenye ujuzi wa kutatua changamoto.kwenye eneo husika kulingana na rasilimali zilizopo na mahitaji yake."

Ameongeza kuwa "Mwaka 2022 tulikuwa na vyuo vya VETA  vipatavyo 29 ambavyo vilitoanhufuma  sasa vipo 80 na ujenzi unaendelea wa vyuo 65 katika wilaya  ifikapo 2025 vyuo vyote vitakuwa vimekamilika na kufanya idadi ya vyuo vya VETA kuwa takriban 145  ambapo kila wilaya itakuwa ina chuo hiki."

Kasore amesema hatua hiyo pia inakwenda kuleta Tina katika uwekezaji ambapo wataalam katika fani mbalimbali wanakwenda kupatikana kupitia vyuo hivyo na kufanya kazi kwenye maeneo ya uwekezaji na viwanda.

Vile vile amesema VETA imekuwa ikitoa elimu ya ufundi kwa wenye ulemavu ambao nao wamekuwa karibuni nyenzo za kifundishia watu wenye ulemavu kutokana na changamoto za ufundishaji nanujifunzaji wanaouona wanapokuwa wanafundishwa na walimu wao.

"Ndio maana tunasema kwetu VETA aletwe mtoto mwenye ulemavu wowote sisi tutamuangalia sina ya ulemavu na tutajua aseme fani gani na namna ya kumfundisha."amesisitiza

Pia amesema katika maonesho hayo wamekuwa kuonesha nini VETA inafanya ambapo zipo bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na walimu kwa kushiriliana na wanafunzi wao ambazo kimsingi zinaenda kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

"Kwa mfano kuna machine ya kumenya viazi vya chips ambapo unakuta ni mjasiriamali mdogo anataka kumenya dunia la viazi,huyu hawezi kupata adha ya kuweka mtu wa kumenya viazi kama atakuwa na mashine hii,kwa hiyo zipo bidhaa nyingi ambazo zinaenda kurahisisha kazi huko katika jamii zetu." Amesema

Pia amesema VETA inatoa mafunzo kwa wafanyakazinwa ndani na wanaohudumia wazee na watoto huku akisema wakina hiyo ni changamoto wakaongeza na mtaala huo ili hata wale wanaohitaji kwenda kufanya kazi za ndani nje ya nchi wamekuwa na mtaalam huo na hivyo kufanya kazi kwa kujiamini na uhakika.
Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.