Ubunifu uchoraji picha Rais Samia washangaza wananchi maaonesho sabasaba

Na Joyce Kasiki,Dar
PICHA moja  ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan iliyochorwa na mwanafunzi wa chuo Kikuu cha Dodoma inayomuelezea Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa  katika majukumu yake matatu makubwa ya Kitaifa imekuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wengi wanaotembelea maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar Es Salaam Mkuu wa Idara ya Sanaa na Taaluma za Habari Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Dkt.Deograsia Ndunguru amesema,watunwengi wanaotembelea banda lao wamekuwa wakishangazwa na ubunifu na ujuzi ambao ametumia mwanafunzi wa mwaka wa kwanza fani ya sanaa chuoni hapo Enock Tarimo kuchora moja inayomuelezea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa katika mavazi matatu tofauti katika majukumu yake ya kitaifa.

"Picha hii ni moja lakini inamuonesha Dkt.Samia katika majukumu matatu tofauti,Ukisimama katikati anaonekana akiwa katika vazi la kiremba chekundu ambayo hutumika maeneo yote kwamba ni picha Rais,ukisimama kushoto anaonekana kama Mwenyekiti wa CCM akiwa katika vazi la kijani na nyeusi na ukisimama upande wa kulia anaonekana katika vazi la kijeshi kama  Amiri Jeshi Mkuu ,kwa hizi ni ubunifu ambazo zinafanya na wanafunzi wetu."

Amesema taaluma ya Sanaa ni moja ya fani ambazo zina fursa ya ajira kwa vijana na hivyo kuwawezesha kujiajiri wenyewe .

Dkt.Ndunguru alisema  wanafunzi wa fani hiyo katika Chuo hicho   wamekuwa wakifundishwa kutumia fursa mbalimbali kupitia rasilimali zinazowazunguka katika mazingira yao  katika kujipatia kipato kwani sanaa ni ajira.

"Kwa mfano chupa za wine na chupa nyingine,chupa hizi hutupwa kila baada ya matumizi ,lakini kwa fani ya sanaa hii ni fursa ambapo zinatengenezwa mapambo."alisema Dkt.Ndunguru

Ameongeza kuwa"Katika maonesho haya tumekuja kuonesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo pamoja na wanafunzi ,kwa hiyo katika banda letu kuna bunifu mbalimbali zilizofanywa na wanafunzi wetu ikiwemo hiyo picha ya Rais Dkt.Samia ,mapambo pamoja na picha nyingine nyingi zilizochorwa na wanafunzi wetu.

Ametumia nafasi hiyo kuwaasa wangependa fani hiyo na hawana nafasi ya kufika ngazi za elimu ya juu,kusoma hata kozi fupi ili waweze kupata ujuzi wa kutosha.

Mhitimu wa UDOM 2023 Sultan Samwel ambaye amejiajiri katika kampuni yake ya mambo ya sanaa Talnis Creative Agency, ametembelea banda hilo na kufurahishwa kuona picha zake alizochora akiwa shuleni.

"Nimefurahi kukuta picha nilizochora katika moja ya mitihani yangu nikiwa chuoni pamoja picha za wanafunzi wenzangu,kimsingi niseme tu sanaa ni ajira kama zilivyofani nyingine kama daktari au sheria na nyingine nyingi,kama hivi mimi nimejiajiri katika kampuni yangu.

Xxxxx

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.