Mtendaji Mkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa (katikati) mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa jumla wa tatu katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya yanayondelea jijini Dar Es Salaam
Na Joyce Kasiki
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imefurahishwa na ushindi wa jumla wa tatu katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea jijijini Dar es Salaam .
Akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao mara baada ya kukabidhiwa ngao ya ushindi wa tatu na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,Mtendaji Mkuu wa Brela Godfrey Nyaisa amesema hayo ni mafanikio makubwa kwao ikilinganishwa na mwaka jana ambapo walikuwa mshindi wa pili katika eneo la taasisi zinazofanya kazi kama za BRELA.
"Tupo hapa kuonesha tunahokifanya pamoja na kuwahudumia wananchi wanaofika bandani kwetu,kwa hiyo ,tunatoa leseni za biashara,tunasajili makampuni..,na leo tunashukuru kuwa washindi wa tatu na kukabidhiwa ngao na Rais ,hii ni uthibitisho unaoonesha kwamba tumetoka wapi ,tulipo na tunakoelekea."amesema Nyaisa
Amesema,siri ya ushindi wao ni kufanya kaI kila wanapokuwa huku akitolea mfano katika maonesho hayo kwamba licha ya kuwa wapo kwenye maonesho lakini shughuli zote zinafanyika hapo.
"Kwa hiyo kama mnavyoona sisi tunakuja kwenye maonesho lakini pia tunafanya na kazi zetu za kuwahudumia wananchi humu humu kwenye maonesho ,Mtu anayetaka leseni au kusajili kampuni huduma hizo atazipata kwenye maonesho lakini pia tunafanya kazi zetu kupiia mifumo."amesema Nyaisa
Vile vile amesema ushindi huo pia umechangiwa na morali ya wafanyakazi ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii na kujituma na hivyo kuketa tija inayohitajika.
"Sisi ndio tunaowasajili wafanyabiashara,wawekezaji wote wawe wa ndani au nje ya nchi,hivyo hakuna mwekezaji anakuja tz bila kupitia BRELA hata kama kampuni ya nje ya nchi,maana hilo ni lango kuu la kutambua biashara zote."amesisitiza Nyaisa
Ametumia nafasi hiyo kiwaasa wqfanyakazi waendelee kuongeza tija katika utendaji wao ili ushindi huo uendane na kazi wanazozifanya
No comments:
Post a Comment