Miaka 64 ya Uhuru: TBN Yasema “Amani Kwanza, Ujenzi wa Taifa Daima”



Published from Blogger Prime Android App



Na Mwandishi wetu

Leo Desemba 9, tunapoadhimisha miaka 64 tangu Taifa la Tanzania  lipate Uhuru, Tanzania Bloggers Network (TBN) inawapongeza Watanzania wote kwa kufikia hatua hii muhimu katika historia ya Taifa letu. Hii ni siku ya kutafakari safari tuliyotoka, mahali tulipo, na mwelekeo tunaoujenga kwa pamoja.

Waasisi wetu walituwachia zawadi kubwa—Uhuru. Lakini walituonya kuwa Uhuru hauwezi kuwa kamili bila kujitegemea. Leo tunakumbusha maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyewahi kusisitiza:

"Uhuru hauwezi kukamilika pasipo kujitegemea. Hatuwezi kuitwa huru kama tunategemea wengine kutupatia mahitaji yetu ya kimsingi."
 
Tujenge Taifa Letu – Tusiibomoe Tanzania

Kama mtandao wa habari za kidijitali, TBN inasisitiza kuwa mafanikio yetu kama Taifa yametokana na utulivu, umoja na mshikamano. Ili kuendelea mbele, tunahitaji kudumisha amani na maridhiano—nguzo muhimu za maendeleo.

Rais mstaafu Benjamin William Mkapa alituasa kwa busara:

"Amani si kitu cha asili; tunahitaji kuilinda na kuitunza kila siku. Bila amani, hakuna maendeleo ya kweli."

Tukikubali kuongozwa na chuki, uchochezi na vurugu, juhudi za waasisi wetu za kupambana na ujinga, umaskini na maradhi zitapotea. Tusiitumie mitandao au uhuru wa maoni kuharibu Taifa letu; tuitumie kulijenga.
Kila Zama na Kiongozi Wake – Tuunge Mkono Mageuzi

Kila kizazi kina wajibu wake. Kama alivyoeleza Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi:

"Kila utawala na zama zake. Kila kiongozi na mchango wake katika ujenzi wa Taifa hili."

Katika awamu ya sasa chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanzania inaendelea na mwelekeo wa 4R: Reconciliation, Resilience, Reforms, and Rebuilding. Huu ni mwaliko kwa Watanzania wote kushiriki katika kujenga Taifa lenye maridhiano, mageuzi chanya na uimara wa kiuchumi na kijamii.

Tuna nafasi ya kuzungumza—basi tuseme kwa njia inayojenga, si inayobomoa. Kuthamini Uhuru ni kufanya kazi kwa bidii, kulinda amani, na kuacha kutumiwa kuharibu misingi ya Taifa letu.
 
TBN Inawatakia Maadhimisho Mema ya Miaka 64 ya Uhuru!

Tanzania Kwanza — Kazi, Utu na Mshikamano. Tusonge Mbele!

Beda Msimbe
Mwenyekiti, Tanzania Bloggers Network (TBN)
Share:

Serikali Yaendelea Kuwezesha Vijana Kupata Fursa za Maendeleo – Maganga*


Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App



Na Mwandishi wetu,Mbeya

Serikali chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaendelea kutekeleza mikakati kuhakikisha vijana wanapata fursa sawa za kujiletea maendeleo binafsi na kuchangia katika ustawi wa Taifa kwa ujumla.

Mikakati hiyo inajumuisha uanzishaji wa mifumo ya kitaasisi, kisera, mipango kazi, miongozo na sheria zinazolenga kutatua changamoto zinazowakabili vijana katika nyanja tofauti za kijamii na kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Mary Maganga wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la siku mbili la Vijana Tanzania linalofanyika kuanzia leo 12 Oktoba hadi 13 Oktoba, 2025 Jijini Mbeya katika Ukumbi wa City Park Garden.

Bi. Mary Maganga, amesema lengo la kongamano hilo ni kuwajengea vijana ujuzi na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, kukuza ushirikiano na ubadilishanaji wa mawazo, pamoja na kutambua na kuunga mkono mipango na miradi ya vijana inayolenga kuinua uchumi wao.

“Vijana ni nguvu ya mabadiliko na maendeleo katika jamii zetu. Ni lazima tutumie vema nguvu hii kubadilisha dunia kuwa mahali bora kwa ajili ya wote,” amesema Katibu Mkuu huyo.

Aidha, amewataka vijana kutumia kongamano hilo kama fursa ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto zinazowakabili, ili Serikali iweze kuyachukua maoni yao na kuyatumia kuboresha sera, sheria, kanuni na miongozo kwa manufaa ya Vijana wote nchini.

Sambamba na hilo, Bi. Mary amewahimiza vijana kote nchini kujitokeza kushiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, kwa kuchagua viongozi wanaoakisi matumaini, malengo na ndoto za taifa hili.
Awali Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Rodrick Mpogolo aliwasihi vijana kuendelea kuipenda nchi na kujivunia Taifa la Tanzania kwa kuwa ni mahala ambapo kila kijana ana mchango wa kuleta maendeleo.
Akizungumza kuhusu idadi ya washiriki wa kongaamano hilo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Seleman Mvunye alisema limehusisha zaidi ya vijana 1,500 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na Maafisa Vijana toka Halmashauri zote nchini.

MWISHO.
Share:

Brigaedia Jenerali Ndagala afungua kongamano la wadau wa Usimamizi wa Maafa Mbeya

Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App


 

Wadau watakiwa kutoa mapendekezo yenye tija kuboresha usimamizi wa maafa nchini


Na Mwsnfisho wetu,MBEYA

MKURUGENZI wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Brigedia Jenerali Hosea Ndagala amefungua Kongamano la Wadau wa Usimamizi wa Maafa linalofanyika kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Athari za Maafa kwa mwaka 2025.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo leo 12 Oktoba 2025 jijini Mbeya, Brigedia Jenerali Ndagala aliwataka washiriki kuja na mapendekezo yenye tija katika usimamizi wa maafa.

 “Kongamano hili limekusudiwa kuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto, na kutoa mapendekezo ya kuboresha mifumo ya kitaifa ya usimamizi wa maafa.

Alisisitiza kuwa:”Nitoe wito kwa washiriki wote kushiriki kikamilifu katika mijadala, kwa sababu michango yenu ni muhimu katika kuhakikisha tunapata mapendekezo yatakayokuwa na tija katika usimamizi wa maafa.

Vilevile aliwataka washiriki kutumia fursa hiyo kuimarisha ushirikiano na kubuni njia mpya za kuongeza ustahimilivu wa jamii zetu ili kupunguza athari za maafa na kulinda maisha na mali.

Brigedia Jenerali Ndagala aliwashukuru wadau wote wanaoendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu katika juhudi za kujenga Taifa lenye ustahimilivu dhidi ya majanga.

Alisema mchango wao katika kupanga, kutekeleza, na kufuatilia mipango ya usimamizi wa maafa nchini umeendelea kuwa wa thamani kubwa.

Kwa upande wake, Inspector Damian Muheya kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji amesema kuwa, ili kufanikisha ustahimilivu endelevu usio na maafa, ni muhimu jamii kushiriki kikamilifu katika hatua za kinga na tahadhari dhidi ya majanga.

Naye Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Dkt. Barnabas Msongaleli ameeleza Taasisi yao imeendelea kutoa mchango katika kuzalisha wataalam wa kada ya usimamizi wa maafa nchini ili kuwa na wabobezi wa eneo hili na kuendelea kuleta tija katika masuala ya menejimenti ya maafa. 

“UDOM tumeendelea kutoa elimu, tunaendesha shahada ya awali ya menejimenti ya vihatarishi vya maafa ( Bachelor of Disaster Risk Management). Pia tunafanya tafiti mbalimbali zinazohusu kupunguza au kuzuia vihatarishi  vya maafa. Na kutoa huduma kwa jamii kwa njia ya kuwafikia jamii kuwapa elimu ya vihatarishi vya maafa na namna bora ya kukabiliana na maafa kabla hayajatokea,” alisisitiza Dkt. Msongaleli.

=MWISHO=
Share:

VETA inavyokuza ujuzi wa vijana kwa kuwafundisha Teknolojia mpya ya utengenezaji magari yasiyotumia mafuta


Published from Blogger Prime Android App



Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki, MBEYA

CHUO  cha Ufundi Stadi (VETA) mkoa wa Mbeya kimeonesha ubunifu mkubwa katika teknolojia ya kisasa kwa kuja na mfumo wa mafunzo ya magari ya Hybrid yanayotumia mota za umeme, huku yakipunguza au kuondoa kabisa utegemezi wa mafuta. 

Teknolojia hiyo imewasilishwa katika maonesho ya Wiki ya Vijana kitaifa, yakionesha mwelekeo mpya wa VETA katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya teknolojia duniani.

Mwanafunzi Adam Akyoo kutoka VETA Mbeya ameleza kuwa, mashine hiyo ya Hybrid imeundwa kwa kutumia mota maalum inayoweza kuzalisha umeme na kusaidia gari kusafiri hata pasipo mafuta.

 "Faida kubwa ya mota hii ni kwamba inaweza kuendesha gari bila kutumia mafuta kabisa,inapunguza gharama za uendeshaji na kumrahisishia mtumiaji safari, hasa pale mafuta yanapokatika na sheli ipo mbali," amesema Adam.

Adam amehimiza vijana wa Kitanzania kutumia fursa zilizopo kupitia vyuo vya VETA ambavyo vinaendelea kuimarishwa na serikali ili kuwapa vijana ujuzi wa kujiajiri au hata kuajiri wenzao.

“Tuna 'mode' ya kujifunza kwa vitendo, kila mwanafunzi anapata nafasi ya kujua teknolojia inavyofanya kazi. VETA haitoi tu nadharia, bali inakuandaa kuwa mtaalamu wa kweli wa teknolojia ya kisasa,” ameongeza.

Kwa mujibu wa Afisa Habari na Uhusiano wa VETA, David Mpondyo, teknolojia hiyo mpya ya magari ni sehemu ya juhudi za VETA kufundisha vijana ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la sasa.

 “Tuko kwenye maonesho ya Wiki ya Vijana tukionyesha kile ambacho vijana wanafundishwa kwenye vyuo vyetu. Si wote wanaofika vyuoni, lakini kupitia maadhimisho haya, wananchi wanaweza kuona na kuelewa kile kinachotolewa na VETA,” amesema Mpondyo.

Ameongeza kuwa VETA kwa sasa ina vyuo 80 ambapo kuna chuo katika kila mkoa, na kwamba ujenzi wa vyuo vingine 65 unaendelea katika kila wilaya nchini, juhudi zinazoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ili kuongeza fursa za mafunzo ya ufundi stadi kwa wananchi wote.

Mpondyo amesema pia kuwa VETA imeamua kuandaa vijana kwa ajili ya teknolojia ya magari ya umeme kwa kuwa magari hayo sasa yameanza kuingia kwa kasi nchini. 

“Awali magari yote yalikuwa ya dizeli au petroli, lakini leo magari mengi yanatumia umeme,wateja wakipeleka magari hayo gereji, mafundi wengi wanayaharibu kwa sababu hawana ujuzi huo,ndiyo maana VETA imeamua kufundisha mfumo huu mpya kupitia 'mode' za kisasa,” amefafanua.

Mpondyo amesema, VETA inaendelea kuwa chachu ya maendeleo ya teknolojia na ujuzi nchini, ikiwapa vijana wa Kitanzania fursa ya kuendana na mabadiliko ya dunia na kuwa sehemu ya nguvu kazi yenye maarifa  yanayoendana na wakati .

.

Share:

Mavunde azindua rasmi shughuli za ujenzi wa mgodi wa Madini Kinywe Mahenge



Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App



▪️Rais Samia apongezwa kwa mazingira wezeshi ya biashara

▪️Aitaka Kampuni ya Faru Kutoa Kipaumbele cha Ajira kwa wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi,

▪️Ni Uwekezaji wa zaidi ya Tsh Trilioni 1.3.

▪️Serikali kuvuna zaidi ya shilingi trilioni 7 kama mapato.

▪️Ni Mradi Mkubwa zaidi kuwahi kutokea Mkoa wa Morogoro.


Na Mwandishi wetu Mahenge, Morogoro. 

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Peter Mavunde (MB), amezindua rasmi shughuli za ujenzi wa mgodi wa madini ya graphite wa Kinywe, unaotekelezwa na kampuni ya Faru Graphite Corporation kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania (hisa 16%) na Black Rock Mining Limited (hisa 84%) ikiwa ni hatua kubwa katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya sekta ya madini nchini.

Akizungumza katika hafla iliyofanyika leo tarehe 9 Oktoba 2025 katika eneo la Mahenge, Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro, Mhe. Mavunde amesema uzinduzi huo ni ishara ya kasi mpya ya uendelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati katika Sekta ya Madini, kutokana na maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

“Mradi huu si uchimbaji wa rasilimali pekee, bali ni injini ya maendeleo itakayochochea ukuaji wa viwanda, biashara, ajira, na ustawi wa jamii katika eneo la Mahenge kwa ujumla” amesema Waziri Mavunde.

Kwa mujibu wa Waziri Mavunde, mradi wa Mahenge unatarajiwa kugharimu takribani dola za Marekani milioni 510,(zaidi ya tsh trilioni 1.3)na utazalisha ajira zaidi ya 400 wakati wa ujenzi na zaidi ya 900 ajira za kudumu mgodi utakapoanza uzalishaji kamili. Nje ya mgodi, takribani ajira zisizo za moja kwa moja zaidi ya 4,500 zitachochewa kupitia mnyororo wa thamani wa wachuuzi, wakulima, wasambazaji wa bidhaa na watoa huduma.

Aidha, amesisitiza kuwa, Serikali inatarajia kupata mapato ya zaidi ya dola bilioni 3.2 (zaidi ya tsh trilioni 7) katika kipindi cha uhai wa mgodi, kupitia kodi, tozo, gawio, na mrabaha wa madini.

Akifafanua umuhimu wa madini ya graphite, Waziri Mavunde amesema madini hayo ni miongoni mwa madini muhimu katika utengenezaji wa betri za magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, na paneli za umeme wa jua na kuwa kupitia mradi huo na mengine iliyopo nchhui Tanzania inajiweka kama kitovu cha malighafi za teknolojia safi duniani.

Pia, Waziri Mavunde ameitaka Kampuni ya Faru Graphite Corporation kuzingatia matakwa ya  Ushikishwaji wa Watanzania (local content) na Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kwa kutoa kipaumbele cha ajira kwa Watanzania, hususan wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi, na kutoa fursa kwa makampuni ya ndani kushiriki katika mnyororo wa ugavi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, amemshukuru Waziri Mavunde kwa uongozi na usimamizi wake thabiti katika Sekta Madini, akibainisha kuwa Mkoa wa Morogoro umebahatika kuwa mwenyeji wa miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo huu wa Faru Graphite wenye thamani ya takribani Shilingi Trilioni 1.3.

“Huu ndio mradi mkubwa zaidi kuwahi kutekelezwa katika Mkoa wa Morogoro,” amesema Mhe. Malima, huku akielekeza wataalamu wa mkoa kuandaa semina maalum zitakazowaelimisha wananchi kuhusu fursa za kiuchumi na kijamii zitakazotokana na mradi huo.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga alisema Serikali ilitoa leseni ya uchimbaji mkubwa mwaka 2024, na tayari fidia ya zaidi ya Shilingi Bilioni 13 imelipwa kwa wananchi 254 waliopisha eneo la mradi, ambao pia watajengewa nyumba mpya.

Ameongeza kuwa miundombinu ya umeme wa kilovolt 220 kutoka Mahenge imeanza kuandaliwa ili kuhakikisha mgodi unapata umeme wa uhakika, sambamba na kuanzishwa kwa miradi ya kijamii (CSR) inayolenga elimu, afya na maji.

Kwa upande wake Msajili wa Hazina, Ndg. Nehemiah Mchechu, ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Faru Graphite Corporation, amesema Serikali kupitia ubia huu inalinda maslahi ya taifa, ikinufaika kupitia hisa, kodi, ajira na mzunguko wa fedha.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi na Mwakilishi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Faru na Blackrock Mining, Black Rock Mining Limited, Ndg. Richard Crookes, amesema kampuni yake imejipanga kuhakikisha utekelezaji wa mradi unafuata viwango vya kimataifa vya usalama na uhifadhi wa mazingira, sambamba na kuwekeza katika teknolojia rafiki kwa mazingira na pia wamemshukuru Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi yaliyopokea uwekezaji huo mkubwa Morogoro.
Share:

Wagombea kiri cha Rais na Makamu wa Rais SAU nao wachukua fomu INEC


Published from Blogger Prime Android App
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Jacobs Mwambejele akiwakabidhi mkoba wenye fomu za kuwania kiti cha urais wagombea kutoka chama cha sauti ya Umma ( SAU).Majalio Paul Kyara (mgombea kiti cha Rsis) na Mhe. Satia
Mussa Bebwa (kushoto) Kiti cha Makamu wa Rais

Published from Blogger Prime Android App

Wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mhe.
Majalio Paul Kyara na Mhe. Satia
Mussa Bebwa (kushoto) wakionesha mkoba wa fomu za uteuzi waliokabidhiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi leo Agosti 13, 2025
Share:

Chama cha DP wachukua fomu kuwani kiti cha Rais na Makamu wa Rais uchaguzi Mkuu ujao


Na Mwandishi Wetu,INEC

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP), Mhe. Abdul Juma Mluya. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Sadoun Abrahman Khatib (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 13, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. (Picha na INEC).

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Mhe. Abdul Juma Mluya. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Sadoun Abrahman Khatib (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 13, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima. 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhani Kailima, akimwelekeza Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Mhe. Abdul Juma Mluya
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Mhe. Abdul Juma Mluya akisaini kitabu.

Mgombea Mwenza, Mhe. Sadoun Abrahman Khatib akisaini kitabu huku akishuhudiwa na Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Mhe. Abdul Juma Mluya akisaini kitabu.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza, Kushoto aliyeketi ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk. 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza, Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk na kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima.
Share:

TAWA YASAINI MIKATABA YA UWEKEZAJI MAHIRI YENYE THAMANI YA TZS BILIONI 719


Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App




📍 Neema yaja kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya uwekezaji

Na Beatus Maganja, Dar es Salaam

Katika hatua ya kihistoria na kishindo kwa sekta ya utalii nchini, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), leo Agosti 12, 2025, imesaini mikataba minne ya uwekezaji wa utalii kupitia utaratibu wa Uwekezaji Mahiri (SWICA) na kampuni ya kitanzania ya Uhusiano International ICT Ltd.

Mikataba hiyo inatarajiwa kuingiza mapato ya Dola za Marekani milioni 281.5 (sawa na Shilingi Bilioni 719 za Kitanzania) kwa kipindi cha miaka 20 ikiwa ni wastani wa Shilingi Bilioni 36 kwa mwaka.

Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam na imehusu uwekezaji katika vitalu vinne vya Burko Open Area (Monduli – Arusha), Selous MHJ1, Selous MHJ2 na Selous ML1 (Liwale – Lindi), vyote vikiwa chini ya kampuni ya Uhusiano International ICT Ltd inayomilikiwa na Watanzania kwa asilimia 100.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana amesema uwekezaji huo utaimarisha sekta ya uwindaji wa kitalii na utalii wa picha, sambamba na kuleta ajira, kuboresha huduma za jamii na kuchochea maendeleo ya wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya uwekezaji. Miradi ya maendeleo itakayoibuliwa na wananchi wenyewe inakadiriwa kugharimu Dola milioni 1.8 (sawa na Shilingi Bilioni 4.6) kwa miaka 20.

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana pia alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake madhubuti katika kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia filamu za Amazing Tanzania na The Royal Tour, zilizochochea ongezeko la watalii na wawekezaji.

Aliahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kusisitiza umuhimu wa matumizi endelevu ya rasilimali kwa kuzingatia sheria, kanuni na misingi ya uhifadhi bora. Alitoa wito kwa wawekezaji zaidi kuja kuwekeza katika vivutio vya kipekee vya utalii vilivyopo nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA, Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis R. Semfuko, amesema TAWA imepiga hatua kubwa kwa kusaini mikataba minne mipya ya SWICA na kufikisha jumla ya mikataba 13 kati ya 14 iliyopangwa  sawa na asilimia 92.3 ya lengo, hatua iliyowezesha kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 27.4 kati ya Januari 2024 na Agosti 2025.

Aidha, Meja Jenerali Semfuko alibainisha kuwa TAWA ipo katika hatua za mwisho kusaini mkataba na kampuni ya GBP Trading Ltd (GTL) kwa ajili ya ujenzi wa kambi za kudumu za kitalii katika hifadhi za Kijereshi, Mpanga-Kipengere na Wami-Mbiki, hatua itakayoongeza vitanda 240 na kupunguza uhaba wa malazi kwa watalii.

Awali, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, Bw. Mlage Yusuph Kabange, alisema tangu kusainiwa kwa mikataba ya awali ya SWICA mwaka 2024, TAWA imeshuhudia ongezeko kubwa la mapato  kutoka Shilingi Bilioni 55 hadi Shilingi Bilioni 87.12 katika mwaka wa fedha 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 158.2.

Aliongeza kuwa TAWA inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa uwekezaji, ikiwemo ujenzi wa kilomita 453.2 za barabara kwa kiwango cha changarawe katika maeneo ya kimkakati  sawa na asilimia 40 ya lengo la kujenga kilomita 1,127 ifikapo mwaka 2026.

Kamishna Kabange alisisitiza kuwa TAWA ipo tayari kushirikiana na wawekezaji ili kuhakikisha utekelezaji bora wa mikataba hiyo kwa manufaa ya Taifa na wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Kampuni ya Uhusiano International ICT Ltd, Bw. Zahir Hassan Mulla, alitoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Maliasili na Utalii, pamoja na Bodi na Menejimenti ya TAWA kwa kuridhia pendekezo lao la uwekezaji. Alisema huu ni mwanzo mzuri kwa wawekezaji wa ndani kuonesha uwezo wao katika sekta ya utalii.
Share:

Dkt.Biteko:Watanzania tusikubali uchaguzi utugawe


Published from Blogger Prime Android App



📌 Asema Kuna Maisha baada ya Uchaguzi

📌 Amwakilisha Rais Samia,miaka 40 Kanisa Anglikana Dayosisi ya Kagera

📌 Rais Samia achangia Tsh. Milioni 50 Ujenzi wa Kanisa Dayosisi ya Kagera

📌 Anglikana Waishukuru Serikali, washirika wa maendeleo

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kuwapima wagombea wa nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu ujao na kuchagua kwa haki ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025 (mwaka huu) na katu wasikubali Uchaguzi uwagawe.

Dkt. Biteko amesema hayo Agosti 12, 2025 wakati akimwakilisha Mheshimiwa Rais katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa kwa Dayosisi ya Kagera iliyofanyika katika Viwanja vya Kanisa Kuu Yohana Mbatizaji – Murgwanza, Ngara.

Amesema kuwa watanzania wanayo haki ya kuwapima wagombea kwa matendo yao na hatimaye kutenda haki kwa kufanya uchaguzi wao kwa njia ya demokrasia huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia kampeni za kistaarabu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa maadili.

Akiwasilisha salamu za Mheshimiwa Rais, Dkt. Biteko amesema Dkt. Samia anatambua na kuheshimu mchango wa taasisi za dini na mchango wake katika maendeleo ya Taifa. “ Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni mdau wa kujenga na kila mnachokifanya kinalenga katika maendeleo ya watu hivyo anaunga mkono jitihada za maendeleo ya wananchi,” amesema Dkt. Biteko.

Katika kufanikisha azma yake, Rais Dkt. Samia amechangia shilingi milioni hamsini (50,000,000/=) katika harambee ya ujenzi wa Kanisa jipya la Anglikana Dayosisi ya Kagera.

Dkt. Biteko Amesisitiza umuhimu wa kila mtu kuwa kisababishi cha furaha kwa mwenzake ili kuwa na maisha ya ya furaha.

Awali, Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Kagera, Darlington Misango Bendankeha ameishukuru Serikali kwa ushirikiano mkubwa unaopatikana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Askofu Bendankeha amesisitiza kuwa Serikali katika ngazi zote inatoa ushirikiano na hivyo kufanikisha utekelezaji wa miradi ya Afya, Elimu kwa maendeleo ya jamii.

Ameiomba Serikali kufanikisha ujenzi wa Barabara inayounganisha taasisi mbalimbali za utoaji wa huduma yenye urefu wa mita 900, Gari la wagonjwa pamoja na mchango wa ujenzi Kanisa ambalo ujenzi wake unaendelea kwa gharama ya shilingi Bilioni 1.18

Kufuatia maombi hayo, Dkt. Biteko amemwelekeza Mkuu wa Mkoa, Mkuu Wilaya na Wakala wa Barabara mijini na vijijini (TARURA) kufanikisha ujenzi wa Kipande hicho huku akitoa ahadi ya gari la wagonjwa katika Hospitali ya Murgwanza baada ya kuwasiliana na Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama.

Akizungumzia uchaguzi Mkuu ujao, Askofu Bendankeha amewahimiza wananchi kushiriki kikamilifu na kuwachagua viongozi wao katika uchaguzi Mkuu ujao ili kuchochea maendeleo “ Tujiandae kushiriki uchaguzi Mkuu ujao, kura yetu ndiyo nguvu ya mabadiliko.” Amesema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Fatuma Mwassa amelipongeza Kanisa la Anglikana Tanzania kwa huduma mbalimbali za maenseleo zinazotolewa kwa jamii.

Share:

Wanahabari wachukua fomu kuwania kiti cha Urais na Makamu wa Rais ,ni Mwalimu na Minja

Na Mwansiahi Wetu Dodoma 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) Mhe. Salum Mwalimu. Mgombea huyo alichukua fomu hizo leo Agosti 12, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. (Picha na INEC).

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Mhe. Salum Mwalimu. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Devotha Mathew Minja (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 12, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima.  (Picha na INEC).
Waandishi wa Habari, Salum Mwalimu aliyepata kufanya kazi katika kituo cha Televisheni cha Channel Ten na Devotha Minja aliyekuwa mwandishi wa ITV mkoa wa Morogoro leo wamechukua mkoba wa fomu za uteuzi wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais kupitia Chama cha CHAUMA. Wagombea hao pichani wakiwa na mkoba wao wa fomu za uteuzi.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza. 
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza. 

Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) Mhe. Salum Mwalimu akielekeza namna ya kujaza kitabu.
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) Mhe. Salum Mwalimu akisaini kitabu.
Mgombea Mwenza Mhe. Devotha Minja akisaini kitabu
Mgombea Mwenza Mhe. Devotha Minja akisaini kitabu
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhani Kilima akizungumza.


Baadhi ya wajumbe wa Tume wakiwa katika utoaji fomu.

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Chauma wakiwa katika utoaji fomu.

Mwenyekiti wa Chauma Mhe. Hashim Rungwe akiwa Benson Kigaila
Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.