Mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji mapato ya maegesho ya magari kuleta tija katika ukusanyaji mapato


Mhasibu Kitengo cha Mapato wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Osward Mobily akiwa katika banda la TARURA jijini Dodoma akionyesha maeneo ambayo Ttarura iinayafanyia kazi.

Afisa Uhusiano wa TARURA Theresia Chimagu akimpa kipeperushi mteja aliyefika katika banda la TARURA jijini Dodoma.


JOYCE KASIKI,DODOMA

MFUMO wa malipo ya kielektroniki wa maegesho ya magari unatarajiwa  kufikia mikoa yote hapa nchini  ifikapo Juni 2022 ili mfumo huo uanze kutumika kote nchini kwa lengo la kuongeza tija katika ukusanyaji wa mapato ya maegesho ya magari.

Hayo yamesemwa jijini hapa na Mhasibu Kitengo cha Mapato kutoka Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Osward Mobily wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya Usalama na Afya Mahali pa kazi huku akisema kwa sasa mfumo huo umeshafika katika mikoa 10 hapa nchini.

Ameitaja mikoa ambayo mfumo huo tayari umeshaanza kufanya kazi kuwa ni pamoja na Iringa,Singida,Dodoma,Mwanza,Dar es Salaam,Pwani,Morogoro,Tanga,Kilimanjaro na Mbeya.

Mobily amesema ,TARURA wameanzisha mfumo huo ili kukoa mapato ambayo yamekuwa yakipotea kutokana na pesa zinazokusanywa kupita kwenye mikono mingi na kusababisha upotevu kabla ya kufika panakohusika.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea mafanikio katika mikoa ambayo imeshaanza  kuutumia mfumo huo huku akisema,mfumo umeonyesha mafanikio makubwa katika ukusanyaji wa mapato ya maegesho ya magari ikilinganishwa  na ushuru wa maegesho ulivyokuwa unakusanywa kupitia kwenye mikono ya watu.

“Ndio maana mfumo ulifanyiwa majaribio katika mikoa michache na kuanza kuongezwa mikoa mingine ambapo hadi sasa kuna mikoa kumi ambayo mfumo umewekwa na tayari kuna mikoa ambayo ipo kwenye mchakato wa kuongezwa kwenye matumizi ya mfumo huo ambapo itaongezwa mikoa mitano mitano kwa awamu mpaka kukamilika mikoa yote.”amesema Mobily

Kwa mujibu wa Mobily  mfumo wa awali uliokuwa unahusisha kupokea fedha taslim, kulikuwa kuna ucheleweshwaji na upotevu wa fedha kutokana na kupita katika mikono ya watu wengi ambapo ilikuwa inapunguza usalama wake tofauti na mfumo mpya wa kidigitali ambao muhusika akishalipa fedha ile inaenda moja kwa moja kwenye mfuko wa Serikali.

“Kwa hiyo fedha zinakuwa zinapatikana kwa wakati na zinaenda kufanya shughuli zilizokusudiwa ikiwemo uboreshaji wa barabaraza mijini na Vijijini .”amesisitiza Mobily

Akizungumzia changamoto za mfumo wa awali amesema,kulikuwa na wateja ambao wanaondoka bila kulipa ushuru licha ya kuandikiwa risiti lakini kwa mfumo huu imekuwa ni rahisi kwa sababu chombo kikifika tu kinachukuliwa taarifa na kutengenezewa  Ankara ya kudaiwa .

Vile vile amesema,kulikuwa na usumbufu kwa wanaokusanya ushuru dhidi ya wenye vyombo vya moto kutaka mazungumzo hali ambayo kwa sasa haipo kwani haihusishi na kuchukua fedha taslim,hivyo hakuna mazungumzo yoyote huku akisema hatua hiyo imerahisisha na imeongeza ufanisi ambao umepelekea makusanyo kuongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na makusanyo yaliyokuwa yanapatikana awali.

Hata hivyo Mobily amesema,bado kuna uhitaji wa elimu ya mfumo mpya kufika kwa watumiaji wa vyombo vya moto ili kuuelewa vizuri mfumo huo na kuondoa changamoto katika utekelezaji wake.

“Wananchi bado wanahitaji elimu kwani bado haijawafikia vya kutosha ,kwa hiyo kwa sehemu kubwa tunahitaji nguvu kubwa ya kuwekeza kwenye utoaji wa elimu na kuhakikisha mmiliki wa chombo cha moto anakuwa na uelewa dhidi ya mfumo huu lakini pia watu wetu wanaofanya ile kazi tuwaongezee uelewa zaidi ili wawe mabalozi wazuri wanapokutana na wateja kwani wao ndio wanakutana na wateja moja.”

Hata hivyo amesema , tayari wameshaanza kufanyia kazi changamoto zote zinazoukabili mfumo ili kuufanya kuwa na tija kwa wateja na Taifa kwa ujumla.

Mobily amesema TARURA pia imejikita zaidi katika utengenezaji,usanifu na maboresho ya miundombinu ya barabara za mijini na vijijini ili ziweze kupitika vizuri katika majira yote ya mwaka.

Maonyesho hayo yanafanyika Jijini Dodoma katika viwanja vya Jakaya Kikwete ambapo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi (TUCTA) na Wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi.

 

 

 

Share:

TPDC yaeleza ilivyojipanga kufikisha huduma ya gas asilia kwa wananchi

 

Afisa Usalama Mahala pa Kazi Deusdedit Kiheka akiwa katika banda la Shirika la Petroli nchini jijini Dodoma akionyesha namna ya kuvaa mtungi wa oksijeni mtu anapokuwa  kwenye moshi au mahali ambapo hakuna hewa ya oksijeni ya kutosha (SCBA).

 

JOYCE KASIKI,DODOMA

SHIRIKA  la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) limesema,linaendelea kufanya taratibu za kuwaunganisha wananchi na gas asilia inayosafirihswa kwa bomba la mafuta lilijengwa kutoka Dar es Salaam hadi Mtwara kwa ajili ya matumizi ya majumbani ambapo kwa mkoa wa Lindi pekee tayari wateja wapatao 200 wameshaunganishwa .

Akizungumza jijini hapa kwenye maonyesho ya Usalama na afya mahala pa kazi yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA) na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Afisa Maendeleo ya Jamii,Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano  wa TPDC Jackob Haule amesema  kazi hiyo inafanywa na TPDC kwa kushirikiana na kampuni yake Tanzu ya Gasco .

Amesema,mradi huo wa kusambaza gas asilia kwa ajili ya matumizi ya majumbani umeanza katika mikoa  Dar es Salaam ,Lindi na Pwani .

Aidha Haule amewatia moyo wananchi ambao  bado hawajafikiwa na huduma hiyo huku akisema serikakli yao ya awamu ya sita kwa ujumla wake inaendelea kujipanga kuhakikisha wananchi wengi wanafikiwa na gas asilia ukiwemo mkoa wa Dodoma.

Amesema,katika mko huo tayari wameshaanza kufanya stadi ili kufahamu hasa  mahitaji ya huduma itakayohitajika ambapo baada ya stadi kukamilika ndipo shirika litafahamu uhitaji na kuona namna ya kufikisha huduma mkoani humo.

 “Gas asilia inatakiwa ufahamu mahitaji ya eneo husika ndipo upeleke ,hii hatupeleki kama maji au umeme wa kawaida,kwa ujumla stadi inaendelea na pale itakapokamilika tutafahamu kwamba tunahitaji gas kiasi gani ili iweze kuwafikia wakazi wa Dodoma.”amesema Haule na kuongeza kuwa

“Kwa Dodoma bado hatujafika kwa sababu hakuna miundombinu ya gas ambayo imefika Dodoma ,hata hivyo  tayari kuna stadi maalum imefanyika ambayo baada ya kukamilika kwake wakazi wa Dodoma watapata gas asilia ambayo iatakuwa ikisafirishwa kwa njia ya magari  na kutakuwa na kituo ambacho wahitaji wa gas asilia watakuwa wanapata ambayo itasambazwa kutoka kwenye hicho kituo hadi kwa watumiaji kwa huduma mbalimbali.”

Vile vile amesema,hapa nchini kuna ugunduzi wa gas asilia na tayari kuna baadhi ya maeneo wameshaanza kuitumia huku akisema kuwa  serikali bado ipo kwenye mkakati wa kuhakikisha kwamba na wao wanaanza kutumia gas asilia ambayo itasaidia kuweka mazingira katika hali ya usalama zaidi kwani wananchi wengi watatumia nishati hiyo na kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni ambayo yamekuwa yakisababisha uharibifu mkubwa wa mazingira nchini,

Katika hatua nyingine Haule amesema,pia upo  mradi wa kusambaza  miundommbinu ya kutumia gas asilia kwenye magari na pia kuna baadhi ya viwanda ambavyo tayari vinatumia gas asilia .

Amesema,mpaka sasa tayari kuna jumla  viwanda 52 ambavyo vinatumia gas asilia katika mikoa ya Dar,Pwani na Mtwara .

Kwa mujibu wa Haule TPDC kwa kushirikiana na Gasco ambayo inashughulika na miundombinu ya  gas wameingia mkataba na wananchi wa maeneo ambayo limepita bomba la gas(MKUZA) kwa ajili ya kuhakisha ulinzi wa bomba hilo ambalo limejengwa kutoa Dar es Salaam hadi Mtwara .

Pia amesema, TPDC kwa kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu katika kulinda na kunufaika na uwepo wa gas kwenye maeneo yao ambapo TPDC kwa kutumia Sera yao ya kurudisha kwa jamii wamekuwa wakisaidia wananchi katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika michezo ,masuala ya utawala bora elimu na afya kwa kuweka miundombinu mbalimbali katika maeneo hayo.

“Katika Afya tumekuwa tukishirikiana na wananchi pamoja na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuhakikisha kwamba tunawezesha ujenzi wa zahanati pamoja na kununua vifaa tiba kwenye hizo zahanati..,ambapo kwenye elimu tumekuwa tukishirikiana na halmashauri na wananchi kwa maana ya kata ,vijiji na viongozi wengine kuhakikisha kwamba kwenye sekta ya elimu tunawezesha kujenga madarasa pamoja na kuwapatia madawati na vifaa vingine katika sekta ya elimu.”

Katika masuala ya utawala Bora wamekuwa wakisaidia ujenzi wa ofisi za Serikali za Mitaa kwa maana ya kata na vijiji,kujenga na kuweka samani za ofisi lakini pia wamekuwa wakiandaa mabonza mbalimbali ambayo yanakuwa na dhima tofauti ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kulinda miundombinu,kulinda afya zao lengo kuu ni kujenga ushirikiano na mahusiano mazuri hasa katika kulinda rasiliamli za shirika hilo ipasavyo .



 



Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.