Wazazi watakiwa kutowakatisha tamaa watoto wanaokosa alama za kuendelea na kidato cha tano
VETA inavyonufaisha vijana katika kujiajiri
AFISA Uhusiano wa VETA Dorah Tesha |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini (VETA) imewezesha kutoa mafunzo na vyeti kwa vijana zaidi ya 10,000 nchi nzima ambao walipata ujuzi nje ya mfumo rasmi wa kupitia vyuo vya VETA.
Afisa uhusiano wa VETA Dorah Tesha ameyasema hayo wakati akizungumza na waandihsi wa habari walipotembelea banda la VETA katika maonyesho ya Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi yaliyoratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) na kufanyika ka uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Dorah amesema,mafunzo hayo ambayo huratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na VETA ,yamesaidia kuboresha ujuzi wa vijana hao na hatimaye kuweza kujiajiri katika fani mbalimbali na hivyo kujipatia kipato.
Kuhusu maonyesho hayo Dora amesema,wameshiriki ili kuonyesha na kuwapa taarifa wananchi shughuli za VETA na namna inavyotoa mafunzo.
“Katika maonyesho haya ushiriki wetu umejikita katika kuonyesha mafunzo tunayotoa ambayo yamelenga kuwapa ujuzi watu wa rika mbalimbali .”amesema Dorah na kuongeza kuwa
“Pamoja na mambo mengine,atakayetembelea banda letu atapata kujua kuhusu masuala ya ubunifu unaofanywa na walimu na wafunzi katika vyuo vya VETA “
Afisa uhusiano huyo amesema ,mafunzo ya VETA yamejikita katika vitendo zaidi huku akiwakaribisha wananchi kutembelea banda lao ili kujionea uhalisia wa kupata stadi na ubunifu wa vitu ambavyo vinaweza kutatua changamoto kwenye jamii lakini fursa ya kujiajiri.
Aidha amesema, VETA imejikita katika kuandaa nguvukazi ya kuhudumia viwanda hapa nchini.
Mbunge Chikota ahoji mpango wa Serikali wa kuanza ujenzi mradi wa maji wa mto Ruvuma hadi Manispaa ya Mtwara
Mbunge wa Nanyamba Abdallah chikota |
JOYCE KASIKI,DODOMA
MBUNGE wa Nanyamba Abdallah Chikota (CCM) ameitaka Serikali kueleza ni lini itaanza ujenzi wa mradi wa mto Ruvuma kwa kuyatoa maji katika mto huo na kuyapeleka katika Manispaa ya Mtwara .
Akiuliza swali la nyongeza jana Bungeni jijini Dodoma,Chikota alisema kukamilika kwa mradi huo kutanufaisha Jimbo la Nanyamba na Manispaa ya Mtwara.
“Nataka kujua ,hivi sasa kuna mradi mkubwa wa kutoa maji mto Ruvuma kupeleka Manispaa ya Mtwara mradi ambao utanufaisha Jimbo la Nanyamba na Manispaa ya Mtwara ,je mradi huu lini utaanza kutekelezwa?”alihoji Chikota
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi alisema,mradi wa mto Ruvuma ni moja kati ya miradi ya mkakati wa wizara ya Maji iliyolenga kutatua changamoto ya maji kwa wananchi.
“Serikali inaenda kuhakikisha maji ya Mto Ruvuma yanakwenda kutatua matatizo ya maji katika maeneno yote ambayo mradi utapitia ,na mradi huu utaanza kutekelezwa tutakapopata fedha .alisema Mhandisi Mahundi
Awali katika swali la msingi Mbunge wa Viti Maalum Tunza Malapo (CHADEMA) alitaka kujua je, ni lini Mradi wa maji wa Ikozi uliopo Sumbawanga Vijijini utakamilika.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi alisema, Utekelezaji wa mradi utakamilika katika mwaka wa fedha 2022/2023
Aidha alisema,katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali imeendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Bwawa la Ikozi utakaohudumia viijiji vya Ikozi, Kazwila, Chituo na Tentula vya kata ya Ikozi Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.
Alisema,mradi huo unahusisha ujenzi wa bwawa, ulazaji wa bomba kuu umbali wa Kilometa 1.2, nyumba ya mtambo, ununuzi na ufungaji wa pampu za kusukuma maji na ujenzi wa mfumo wa kusafisha na kutibu maji.
.
Mbunge Sanga apaza sauti kero ya maji Makete
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
MBUNGE wa Makete Festo Sanga(CCM) ameitaka Serikali lini itakamilisha ujenzi wa mradi wa Matamba Kinyika ambao umefgharimu fedha nyingi lakini umeshindwa kutekelezeka kwa takribani miaka saba sasa.
Mbunge huyo ameoa kauli hiyo Bungeni jijini hapa wakati akiuliza swali la nyongeza ambapo alisema licha ya mradi huo kutokamilika kwa muda mrefu lakini tayari umeshaigharimu Serikali kiasi cha shilingi bilioni 2.8 kuujenga.
“Je ni lini serikali itakabidhi mradi huo kwa wananchi wa kijiji cha Nungu ,kijiji cha Ng’onde ,kijiji cha Mbela na kijiji cha Itani ili waweze kupata huduma ya maji Kwa sababu imebaki hatua ya usambazaji?”alihoji Mbunge huyo
Vile vile alitaka kujua ni lini Serikali itatoa kiasi cha shilingi bilioni 2.5 kati ya shilingi bilioni tatu ili kukamilisha mradai huo baada ya kutoa shilingi milioni 500 pekee yake mpaka hivi sasa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo kwa wananchi wa kata ya Iwawa .
Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi alisema,Serikali inaendelea kutoa pesa na kutekeleza miradi ya maji ili wananchi wapate maji safi na salama.
Kuhusu mradi ambao umeshatolewa shilingi milioni 500 na Serikali,Mhandisi Mahundi alisema,utekelezaji wake unaendelea vizuri .
“Huu ni ule mradi uliotumia fedha za mapambano dhidi ya uviko 19 na fedha iliyobaki tutaendelea kutoa kuanzia mwezi huu wa sita na tutaendelea kuongeza fedha ili kuukamisha.”
Kuhusu mradi wa Matamba Kinyika ,Mhandisi Mahundi alikiri kwamba ni kweli mradi huo umechukua muda mrefu huku akisema huo ni miongoni mwa ile miradi ambayo iikuwa ni chechefu.
Hata hivyo alisema Serikali inaendelea kuikwamua na mradi umeshafikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 katika utekelezaji wake na kwamba utamaliziwa muda siyo mrefu.
Awali katika swali la msingi Sanga alitaka kujua Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa mradi wa maji Kata ya Iwawa Makete Mjini.
Akijibu swali hilo Mhandisi Mahundi alisema,katika mwaka wa fedha 2021/22 Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji wa kuhudumia Kata ya Iwawa kwa kutumia chanzo cha mto Isapulano. “Mradi huu unahusisha ujenzi wa chanzo, ulazaji wa bomba kuu umbali wa Kilometa 12.5, ulazaji wa mabomba ya usambazaji umbali wa Kilometa 39.0 na ujenzi wa matanki matatu yenye ujazo wa lita 450,000. “alisema Mhandisi Mahundi
Aidha alisema,utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha 2022/2023.
wadau waombwa kuishiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Malezi ,Makuzi ya watoto
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Shabani Muhali akifunga mafunzo kwa wadau wa Malezi na Makuzi ya watoto jijini Dodoma. |
JOYCE KASIKI,DODOMA
WAKATI Serikali ikitekeleza Programu jumuishi ya Taifa ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) ya miaka mitano 2021/22-2025/26,wadau nao wameombwa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa programu hiyo kwa kuweka kwenye bajeti zao kwa lengo la kufikisha elimu hiyo katika jamii.
Asilimia 43 ya watoto nchini Tanzania wapo kwenye hatari ya kutofikia hatua timilifu za ukuaji na maendeleo kutokana na viashiria mbalimbali vya hatari vya maendeleo kama vile utapiamlo ,umasikini,kukosekana kwa uhakika wa chakula ,msongo wa kifamilia ,miundombinu duni na uhaba wa rasilimali pamoja na utekelezaji na unyanyasaji wa watoto.
Akifunga mafunzo kwa wadau yaliyoandaliwa na Mtandao wa Malezi na Makuzi ya Watoto (TECDEN) yaliyofanyika jijini Dodoma,Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Seriakli za Mitaa (TAMISEMI) Shabani Muhali alisema,hatua hiyo itasaidia elimu ya malezi na makuzi kufika kwa jamii na hivyo kufanikisha lengo la Programu ya MMMAM na hatimaye kujenga kizazi chenye tija kwa Taifa.
Muhali ambaye aliiwakilisha TAMISEMI katika mafunzo hayo amesema,Serikali imeamua kuja na programu ya kuwaleta wadau pamoja katika kushughulikia masuala ya mtoto tangu akiwa tumboni ili kuhakikisha jamii inalea watoto kwa kuzingatia mambo yote muhimu yakiwemo Afya bora,lishe ya kutosha,malezi yenye mwitikio,ujifunzaji wa awali pamoja na ulizni na usalama wa mtoto huku akisema malezi hayo humfanya mtoto kukua katika utimilifu wake.
Aidha kiongozi huyo ametumia nafasi hiyo kuwaongoza wadau hao kula
kiapo cha kwenda kuifanya kazi ya kuelimisha jamii kuhusu Programu ya MMMAM ili
kufika kwa jamii na siyo kubaki kwenye makabati.
Mkurugenzi wa TECDEN Mwajuma Rwebangira amesema inawategemea wadau
hao kwamba wanakwenda kufanya kazi ya kuhakikisha PJT-MMMAM inakwenda kufanikiwa katika utekelezaji wake.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la Malezi na Makuzi ya Mtoto (CiC) Craig Ferla alisema,wadau ni moja ya watu wanaotegemewa katika mafanikio ya utekelezaji wa Programu hiyo.
Aidha amesema Programu ya MMMAM ni fursa ya kipekee kwa Taifa ambayo inahitaji ushirikiano wa wadau kwa lengo la kuhakikisha mtoto anakuwa katika utimifu wake.
Mkuregenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (cic) Creig Ferla akizungumza na wadau wa malezi na Makuzi ya watoto jijini Dodoma
“Mwaka huu tuna zoezi la Sensa ya Watu na Makazi,Sintashangaa kuona theluthi moja ya watanzania kuwa ni watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 0-8,kwa mantiki hiyo kama Taifa tukiweza kuwekeza kwa watoto hao ,tutakuwa na Taifa bora la kesho.”alisema Craig na kuongeza kuwa
“Katika maendeleo ya mtoto kila afua ina nafasi yake hivyo inahitaji ushirikiano wa wadau ili tupige hatua kufikia njozi za Taifa.,”
Kwa upande wadau nao waliahidi kufanya kazi ya kufikisha elimu kwa jamii kama walivyopata mafunzo huku kila mkoa ukiweka mpango kazi wake huku kwa upande wa Maafisa Ustawi na Maafisa Maendeleo ya Jamii wakiahidi ushirikiano kwa waandishi wa habari katika utekelezaji wa prograu hiyo .
Wadau wa masuala ya Malezi na Makuzi wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dodoma
Felista John Mwakilishi wa Taasisi za Kimataifa aliahidi kutoa ushirikiano katika jambo hilo kwa kadri itakavyohitaika.
Akizungumza na mtandao huu,Rehema Francis Mkazi wa Majengo jijini Dodoma amishukuru Serikali kuanzisha programu hiyo huku akiiomba Serikali na wadau wafanye kila linalowezekana kuhakikisha elimu ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali inafika kwa jamii na kuiishi.
“Elimu hii ikifika kwa jamii ipasavyo itasaidia sana kuwalea watoto kwa kuzingatia maeneo muhimu ya ukuaji wao,nasema hivi kwa sababu wapo wakina mama ambao huwapiga sana watoto wao wadogo wasiokuwa hata na uwezo wa kusema ,lakini unakuta mama huyu anafanya hivyo bila kujua madhara anayomsababishia mtoto huyo.”amesema Rehema
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto ateta na wadau kuhusu utekelezaji wa Programu ya Malezi na Makuzi ya Watoto
JOYCE KASIKI,DODOMA
MKURUGENZI wa Idara ya Maendele ya Watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku amesema,Programu Jumuishi ya Kitaifa ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) haikuja kama mbadala wa programu nyingine za masuala ya watoto zilizotangulia.
Akifungua warsha ya wadau wanaojishughulisha na malezi na makuzi ya watoto iliyofanyika mkoani Dodoma,Kitiku amesema ,wakati wadau wakitekeleza programu hiyo katika kelimisha jamii,lazima wazingatie na programu zilizopo.
“Programu hii ,haikuja ku’replace’programu zilizopo ,imekuja kuangalia mahali ambapo hapajaweka nguvu au paliposahaulika ili kuhakikisha mtoto anakua kwa utimilifu wake.”
Kwa mujibu wa Muongozo wa Programu ya Taifa ya MMMAM, Programu hii inatambua programu zilizopo za kitaifa ambazo ambazo utekelezaji wake unajumuisha wadau wa sekta mbalimbali katika kutoa huduma zinazolenga vipengele vyote vya ukuaji na maendeleo ya mtoto.
Pamoja na programu nyingine,pia Programu hii inalenga kutumia uzoefu wa programu zilizopo ikiwemo Programu Jumuishi ya Taifa ya Lishe II ya mwaka 2021/22-2025/26 na mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA wa 2017/18-2021/22).
Amesema ,programu hiyo imewaleta wadau wengi pamoja ili kumlea mtoto katika maeneo muhimu matano badala ya kila mdau kufanya taratibu zake katika malezi ya mtoto.
“Programu hii imewaleta wadau pamoja ili kumlea mtoto bila kumkata vipande vipande..,mfano hapo awali kabla ya programu hii kuwepo,watu wa afya walimlea mtoto kivyao ,lakini tukasema, tulete programu hii ambayo itamlea mtoto kwa pamoja ili kuleta tija katika malezi na makuzi ya mtoto.”amesema Kitiku na kuongeza kuwa
“Moja ya sababu ya kuwekeza kwa mtoto ni kuhakikisha anapata mahitaji yote muhimu katika umri wa miaka 0 hadi minane ili kuwa na Taifa la kizazi chenye tija.”
Amesema sayansi inaeleza wazi kuwa asilimia 80 ya ubongo wa mtoto unakua katika kipindi cha umri wa miaka 0-8 ,huku akisema bila kumlea vyema mtoto inavyotakiwa katika umri huo ,kutakuwa na taifa lenye watu ambao hawana uwezo mkubwa katika kufikiri na kutafakari mambo na hivyo kushindwa kuchangia katika uchumi wa nchi.
“Kuna watu wazima sasa hivi wanaweza kungea jambo mpaka ukajiuliza maswali kutokana na alichozungumza na umri wake,hii ni kutokana na uwekezaji uliofanyika akiwa na umri wa miaka 0-8.”amesema Kitiku
Mkurugenzi wa TECDEN akizungumza katika warsha kwa wadau kuhusu utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa (PJT-MMMAM)
Awali Mkurugenzi wa Mtandao wa Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (TECDEN) Mwajuma Rwebangira alisema lengo la kikao hicho ni kuwapitisha wadau wa Mradi wa Mtoto Kwanza ambayo inalenga katika utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT- MMMAM) ili waweze kwenda kutoa elimu kwa jamii kuhusu Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto na hatimaye kufanikiwa kwa kwa Programu hiyo ya Taifa .
"Sisi wadau wa mradi wa Mtoto Kwanza katika kutekeleza mradi huu tuhakikishe tunatumia Programu hii ili kuhakikisha tunajikita katika kutoa elimu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto katika maeneo tunayotoka" amesema Mwajuma
Mkurugenzi wa Shirika la Bright Jamii Initiative Irene Fugara ni miongoni mwa wadau walioshiriki katika warsha hiyo ambapo amesema,Shirika la Bright Jamii limejikita kuhakikisha linatoa elimu ya Malezi kwa Mtoto ili kupambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya Watoto ili iweze kusaidia kuondoka na tatizo hilo.
"Lazima tuijengee jamii uwezo wa kuwa na uelewa kwenye masuala ya Malezi ili iwasaidie katika kuhakikisha watoto wanalelewa kwenye mazingira mazuri na yatakayowawezesha kuwa wazalendo, jasiri na wenye kujiamini " amesema
Naye Meneja Programu kutoka Shirika la KIHUMBE Jeremia Henry amesema Shirika hilo linashirikiana na Serikali na wadau wa maendeleo hasa upande wa miradi ya watoto na vijana katika masuala ya Afya, Malezi, Makuzi, pamoja na Lishe ndani ya jamii.
"Kupitia Programu hii Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto tumepata uelekeo utakaotusaidia kuona ni namna gani tutatoa elimu ya Malezi kwa jamii ili tuwe na jamii yenye watu wenye Malezi bora" amesema Jeremia