Mbunge wa Nanyamba Abdallah chikota |
JOYCE KASIKI,DODOMA
MBUNGE wa Nanyamba Abdallah Chikota (CCM) ameitaka Serikali kueleza ni lini itaanza ujenzi wa mradi wa mto Ruvuma kwa kuyatoa maji katika mto huo na kuyapeleka katika Manispaa ya Mtwara .
Akiuliza swali la nyongeza jana Bungeni jijini Dodoma,Chikota alisema kukamilika kwa mradi huo kutanufaisha Jimbo la Nanyamba na Manispaa ya Mtwara.
“Nataka kujua ,hivi sasa kuna mradi mkubwa wa kutoa maji mto Ruvuma kupeleka Manispaa ya Mtwara mradi ambao utanufaisha Jimbo la Nanyamba na Manispaa ya Mtwara ,je mradi huu lini utaanza kutekelezwa?”alihoji Chikota
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi alisema,mradi wa mto Ruvuma ni moja kati ya miradi ya mkakati wa wizara ya Maji iliyolenga kutatua changamoto ya maji kwa wananchi.
“Serikali inaenda kuhakikisha maji ya Mto Ruvuma yanakwenda kutatua matatizo ya maji katika maeneno yote ambayo mradi utapitia ,na mradi huu utaanza kutekelezwa tutakapopata fedha .alisema Mhandisi Mahundi
Awali katika swali la msingi Mbunge wa Viti Maalum Tunza Malapo (CHADEMA) alitaka kujua je, ni lini Mradi wa maji wa Ikozi uliopo Sumbawanga Vijijini utakamilika.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi alisema, Utekelezaji wa mradi utakamilika katika mwaka wa fedha 2022/2023
Aidha alisema,katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali imeendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Bwawa la Ikozi utakaohudumia viijiji vya Ikozi, Kazwila, Chituo na Tentula vya kata ya Ikozi Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.
Alisema,mradi huo unahusisha ujenzi wa bwawa, ulazaji wa bomba kuu umbali wa Kilometa 1.2, nyumba ya mtambo, ununuzi na ufungaji wa pampu za kusukuma maji na ujenzi wa mfumo wa kusafisha na kutibu maji.
.
No comments:
Post a Comment