AFISA Uhusiano wa VETA Dorah Tesha |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini (VETA) imewezesha kutoa mafunzo na vyeti kwa vijana zaidi ya 10,000 nchi nzima ambao walipata ujuzi nje ya mfumo rasmi wa kupitia vyuo vya VETA.
Afisa uhusiano wa VETA Dorah Tesha ameyasema hayo wakati akizungumza na waandihsi wa habari walipotembelea banda la VETA katika maonyesho ya Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi yaliyoratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) na kufanyika ka uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Dorah amesema,mafunzo hayo ambayo huratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na VETA ,yamesaidia kuboresha ujuzi wa vijana hao na hatimaye kuweza kujiajiri katika fani mbalimbali na hivyo kujipatia kipato.
Kuhusu maonyesho hayo Dora amesema,wameshiriki ili kuonyesha na kuwapa taarifa wananchi shughuli za VETA na namna inavyotoa mafunzo.
“Katika maonyesho haya ushiriki wetu umejikita katika kuonyesha mafunzo tunayotoa ambayo yamelenga kuwapa ujuzi watu wa rika mbalimbali .”amesema Dorah na kuongeza kuwa
“Pamoja na mambo mengine,atakayetembelea banda letu atapata kujua kuhusu masuala ya ubunifu unaofanywa na walimu na wafunzi katika vyuo vya VETA “
Afisa uhusiano huyo amesema ,mafunzo ya VETA yamejikita katika vitendo zaidi huku akiwakaribisha wananchi kutembelea banda lao ili kujionea uhalisia wa kupata stadi na ubunifu wa vitu ambavyo vinaweza kutatua changamoto kwenye jamii lakini fursa ya kujiajiri.
Aidha amesema, VETA imejikita katika kuandaa nguvukazi ya kuhudumia viwanda hapa nchini.
No comments:
Post a Comment