WAZIRI wa Ulinzi Dkt.Stergomena Tax akizungumza kwenye Mkutano wa Tume ya Pamoja baina ya Tanzania na Msumbiji. |
NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax ameshiriki Mkutano wa Nne wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano katika msuala ya Ulinzi na Usalama (JPCDS) baina ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika katika Ukumbi wa Joachim Chisano, Maputo nchini Msumbiji.
Waziri Tax ni Mwenyekiti Mwenza wa
Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji Cristovao Chume.
Mkutano huo unafanyika kwa mara ya nne sasa ambapo Mkutano wa kwanza ulifanyika hapa nchini mkoani Dar es Salaam, Februari 04 - 06 Februari, 2011 ambapo Tume hiyo ilianzishwa rasmi.
Mkutano huo umefanyika kwa ngazi
tatu, ambapo ulianza kwa kutanguliwa na ngazi ya wataalamu , ukifuatiwa na
kikao ngazi ya Makatibu Wakuu na kuhitimishwa na Mkutano wa mawairi wenye
dhamana ya masuala ya ulinzi na Usalama wa mataifa haya mawili.
Pamoja na mambo mengine vikao vya ngazi zote vilijadili ushirikiano kuhusu masuala ya kiulinzi, na hatimaye kutoa fursa kwa Mawaziri hawa wawili, kusaini mikataba itakayowezesha kutekelezwa kwa Hati ya Makubaliano kuhusu ushirikiano kupitia sekta ya Ulinzi na usalama, uliosainiwa kwa pamoja 21 Septemba, 2022 na Mawaziri wa pande zote mbili.
Utiaji saini huo, ulishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na mwenzake Rais wa Msumbiji, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi, wakati wa ziara ya kikazi ya siku tatu, aliyoifanya Rais Samia nchini Msumbiji hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment