Serikali yafungia shule ya chalinze modern islamic kuwa kituo cha mitihani

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknlojia

Serikali yafungia shule ya chalinze modern islamic kuwa kituo cha mitihani

                          

Na WyEST,Dar Es Salaam

 

Serikali imeifungia Shule ya Awali na Msingi Chalinze Morden Islamic kuwa kituo cha Mitihani kutokana na udanganyifu uliofanyika katika Mtihani wa darasa la Saba uliofanyika Oktoba 5 na 6, 2022.

 

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanyika uchunguzi kufuatia taarifa zilizotolewa na Mwanafunzi Iptisam Suleiman Slim wa kituo cha Mtihani wa shule ya Awali na Msingi Chalinze Morden Islamic akieleza kwamba alibadilishiwa namba yake ya mtihani  wakati akifanya mtihani wa somo la mwisho.

 

Akizungumza Jijini Dar es salaam Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema uchunguzi uliofanywa na Kamati ya mitihani ya Mkoa wa Pwani  na ule wa  wataalamu wa miandiko  " Forensic"  uliofanywa na Jeshi la polisi umebaini  ufanano wa miandiko kwa watahiniwa 7 wa shule hiyo .

 

Waziri Mkenda amesema kwa kuwa kulikuwa na uzembe uliofanyika pamoja na kuifungia shule hiyo watumishi wa Serikali ambao walikuwa wasimamizi wa kituo hicho watachukuliwa hatua za kinidhamu  huku akimuagiza Mmiliki wa shule ya Awali na Msingi ya Chalinze Morden Islamic kuwafukuza kazi walimu wote waliohusika katika udanganyifu huo. 

 

 “Kwa kuwa Shule hii ni ya binafsi tunaifungia kuwa kituo cha mitihani na haitaruhusiwa kufanyia tena mitihani, lakini pia mwenye shule hakikisha unawafukuza kazi mara moja waalimu waliohusika  na kama hilo halitafanyika  nakuagiza  Kamishna wa Elimu  futa usajili wa shule hiyo na kuifunga  mara moja,”amesema Waziri Mkenda

 

Aidha kufuatia changamoto hiyo Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limefanya marekebisho ya namba za Mtihani za watahiniwa husika ili kila mtahiniwa aweze kupata matokeo yake halali.

 

“Nakupongeza Mwanafunzi Iptisam wa kuwa na ujasiri wa kutoa taarifa, tayari NECTA imefanya marekebisho hata kwa wengine ambao wamefanyiwa udanganyifu kama huo. Natoa wito kwa wananchi na wanafunzi wote ukiona mtu anafanya mchezo kwenye mitihani toa taarifa na serikali itachukua hatua mara moja,”amesema Prof. Mkenda 

 

Kwa upande wake Mzazi wa Mwanafunzi Iptisam, Suleiman Said ameishukuru Serikali kwa kufanyia kazi changamoto hiyo  aliyoipata mtoto wake wakati wa kufanya mitihani yake ya kuhitimu darasa la Saba. Pia amevishukuru Vyombo vya Habari kwa kutoa taarifa hiyo na kuweza kuwafikia walengwa na kuifanyia kazi.


Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.