MSEMAJI MKUU WA SERIKALI GERSON MSIGWA |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
MSEMAJI Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa maezindua
Taasisi ya wanahabari wanaoandika habari za mtandaoni (TOMA) huku akilitaka
kundi hilo kuandika kwa kuzingatia weledi na maadili yote ya taaluma hiyo
lakini pia lijiendeleze kielimu.
Akizunguumza katika uzinduzi wa Taasisi hiyo,Msigwa
amesema,wanahabari wa mtandaoni lazima wajitofautishe na watu wengine
wanaotumia mitandao ambao hawana taaluma ya habari.
“Lazima tujitofautishe na watu wengine na tuonyeshe
taaluma yetu ,nafasi tunayo,pia tujiendeleze kitaaluma ili tutengeneze maudhui
bora katika vyombo vya habari vya mtandaoni.”amesema Msigwa
Amesema kwa upande wa Idara ya habari Melezo ipo
tayari kushirikiana na TOMA katika kuhakikisha mazingira ya habari mtandaoni
yanaboreka.
Ametumia nafasi hiyo kuwataka waandishi wa habari
za mtandaoni wajiunge na TOMA ,lakini pia waandike habari zao kwa kuheshimu
mipka ,sheria,kanuni na taratibu za nchi zilizopo kwa lengo la kutozua taharuki
katika jamii .
“Sisi wenyewe ndiyo tunaotakiwa tulinde heshima
yetu ili watu watuamini na wanedlee kutufuatilia kwenye mitandao kusoma taarifa
tunaoweka huko.”amesisitiza Msigwa
Aidha amewaasa wanachama wote wa TOMA kutotumika vibaya na watu wasiolitakia
mema Taifa la Tanzania.
No comments:
Post a Comment