NA JOYCE KASIKI,DODOMA
SERIKALI
imepiga marufuku vitabu 16 kutumika mashuleni kutokana na vitabu hivyo kukinzana
na mila , desturi na tamaduni za kitanzania .
Aidha imesema,kwa
shule ambayo itabainika kuendelea kutumia vitabu hivyo mara baada ya katazo la
Serikali itachukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na kisheria ikiwemo
kufutiwa usajili wake.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
kufutwa kwa vitabu hivyo Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf
Mkenda amesema, uwepo wake pia unahatarisha malezi bora ya watoto.
Amevitaja
vitabu vilivyopigwa marufuku kutumika mashuleni ni pamoja na Diary of Wimpy
Kid,Dairy of Wimpy Kid-Rodrick Rules,Diary of Wimpy Kid- The last Straw,Diary
ofi Wimpy Kid –The Ugly Truth na Diary of Wimpy Kid-Cabn Fever.
Vitabu
vingine vilivyopigwa marufuku hiyo ni Diary of Wimpy Kid –The Third Wheel,Diary
of Wimpy Kid –Hard Luck,Diary of Wimpy Kid-The long Haul,Diary of Wimpy Kid –Old
SchoolDiary of Wimpy Kid-Double Down na Diary of Wimpy Kid-The Gateway.
Kwa mujibu
wa Profesa Mkenda ,pia vitabu vya Diary of Wimpy Kid-Diper Overlode,Is for
TANSGENDER(you know best who you are),Is for LGBTQIA (find the word that make
you you na Sex Education a guid to life ,vyote vimepigwa marufuku.
“Hii ni
orodha ya kwanza ,baada ya ukaguzi na kuhakikiwa kwamba vitabu hivi vinakiuka
maudhui ya malezi mema ya mtanzania,ukaguzi unaendelea ,tunahimiza wazazi ,walimu
,wanafunzi na jamii kwa ujumla kwa ambaye atagundua kitabu kingine chochote
kinachokiuka maudhui apige simu kwenye namba 0262160270 au 0737962965.”amesema
Profesa Mkenda
Waziri huyo
ametumia nafsi hiyo kuwahimiza wazazi kukagua mabegi ya watoto mara kwa mara
ili kuhakikisha hawatumii vitabu hivyo.
No comments:
Post a Comment