NAIBU WAZIRI WA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA OMARY KIPANGA AKIZUNGUMZA WAKATI WA MAADHIMISH0 YA KIMATAIFA YA WASICHANA NA WANAWAKE |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
NAIBU waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia
amewataka wazazi na jamii kwa ujumla kuweka jitihada za kuwahamsisha wasichana
na wanawake kuingia katika masomo ya Sayansi ili wapende kusoma masomo ya
sayansi ambayo yatawafanya kuwa wabunifu na hatimaye kuwa wenye tija kwa jamii
na Taifa kwa ujumla.
Ameyasema hayo Februari 11,2023 katika maadhimisho
ya siku ya Kimataifa ya Wasichana na wanawake ambayo yamelenga kuleta chachu
kwa makundi hayo ili nchi iweze kuwa na wanasayansi,wahandisi na wabunifu
katika nyanja mbalimbali.
“Suala la wanawake na wasichana ni mtambuka na
hivyoyanahitaji ushiriki na mchango wa wadau wote bila kujali kama wapo katika
sekta binafsi au sekta ya umma.”amesema Kipanga na kuongeza kuwa
“Sote tunatambua kuwa ujuzi uliojengwa katika
misingi ya sayansi ,teknolojia ,uhandisi na Hisabati unachagiza ubunifu na ni
muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa mipango mbalimbali kwa Taifa.”
Kwa mujibu wa Kipanga maadhimisho hayo yana umuhimu
wa kipekee kuhamasisha wanawake na wasichana kuunga mkono juhudi za serikali
kuendeleza ubunifu wa kisayansi ambao ni nyenzo ya msingi katika kuleta
maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa nchini.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni ‘Buni
,onesha ,inua ,boresha na endeleza,ambayo inalenga kuhamsisha ushiriki wa
wanawake na wasichana katika Sayansi,teknolojia na ubunifu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya
Elimu,Teknolojia na Ubunifu Profesa Maulilio Kipanyula amesema,siku hiyo
ilianza kuadhimishwa na Umoja wa Mataifa 2015 huku kwa hapa nchini ilianza
kuadhimishwa mnamo 2021.
Kwa mujibu wa takwimu za UNESCO,ni asilimia 24 tu
ya wasichana wote wanaoenda vyuo vikuu ndiyo wanaosoma masomo ya
sayansi,teknlojia,uhandishi na hisabati .
Naye Rais wa Taasisi ya Wahandisi wanawake Mhandisi
Ester Christopher amesema,katika chama cha wahandisi kina wanachama wapatao
4000 lakini wanawake ni 300 tu na kwamba kwenye Bodi ya Wahandisi ,wahandisi
waliosajiliwa ni kama 30000 hivi lakini wahandisi wanawake ni 4000 tu sawa na
asilimia kama 12 tu.
“Kwa hiyo tunatakiwa kuweka jitihada za ziada ili kuweza kuhakikisha kwamba hilo ‘gap’tunaliziba kwa kuwahamasisha wasichana kupenda masomo ya sayansi ambayo yatawapeleka kwenye masuala ya Sayansi,Uhandisi,teknlojia na hisabati na kuleta tija kwa Taifa hapo baadaye.” Amesema Mhandisi huyo
No comments:
Post a Comment