Mashirika ya Ndege ya Kimataifa kutangaza vivutio vya utalii


Published from Blogger Prime Android App
Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki akisoma makadirio ya mapato na matumizi Bungeni jijini Dodoma



Na Joyce Kasiki,Dodoma


WAZIRI wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki amesema,mashirika ya ndege ya Kimataifa ya Qatar Airways, Emirates na Turkish Airlines yanaenda  kutangaza vivutio vya utalii vivanvyopatikana nchini Tanzania.

Aidha amesema, Wizara itaendelea kutangaza utalii ndani na nje ya Nchi kupitia matangazo katika Ligi na Mashindano ya Michezo yenye wafuatiliaji wengi zaidi Duniani kwa lengo la kuongeza watalii nchini hadi kufikia watalii milioni tano.

Akizungumza leo Mei 31 mwaka huu Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2024/25 ambapo ametaja vipaumbele vya Wizara hiyo kuwa ni pamoja na Wizara kutumia  watu mashuhuri na wenye ushawishi, Mabalozi wa hiari wa utalii, vyombo vya habari vya Kimataifa vyenye ushawishi pamoja na mitandao ya kimataifa ya utalii kama vile TripAdvisor na Expedia Group, vyombo vya habari kama CNN.

Pia ametaja vipaumbele vingine kuwa ni Wizara kuweka mifumo maalum ya mawasiliano katika misitu ya hifadhi ya asili na mashamba ya miti ili kubaini matukio ya moto; na kutoa elimu ya uhifadhi pamoja na kupambana na kuzuia matukio ya moto. 

Akizungumza kuhusu mkutanonwa wadau wa nyuki Waziri huyo amesema,katika kuelekea mkutano wa wadau wa nyuki wa  Kimataifa  2027,  Wizara itaanza utekelezaji wa  Programu ya Nyuki kwa Vijana na Wanawake ili kuandaa wataalamu na wajasilisamali wa mazao yatokanayo na asali na mazao mengine ya nyuki” Alisema Mhe. Kairuki.

Aidha, Wizara itaandaa Miongozo na Taratibu za kutwaa na kuhamisha umiliki wa rasilimali za malikale kutoka kwa wamiliki kwenda kwa Wadau kwa ajili ya kuendeleza shughuli za uhifadhi na kuandaa Mkakati wa utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Kale ya Mwaka 2008.

Kairuki amesema kuwa wizara itahuisha h muda wa kulipa Ada ya Leseni ya Biashara za utalii na kuwa katika kipindi cha miezi 12 kuanzia siku ya mwisho ambayo wakala wa biashara za utalii amelipia leseni yake badala ya utaratibu wa sasa.

"Wizara kwa mwaka ujao wa fedha itapunguza Ada ya  Leseni ya Biashara za utalii  kwa wakala wa kupandisha watalii mlimani (mountain climbing), kufuta tozo kwa waongoza watalii wenye leseni hai kila wanapoingia hifadhini."amesema Kairuki na kuongeza kuwa

"Wadau watalipa  Ada ya  Leseni ya Biashara za utalii kwa kutumia shilingi ya Tanzania badala ya Dola za Marekani pamoja na kuongeza muda wa Leseni ya Biashara za utalii kwa Waongoza watalii ambapo kwa sasa  itadumu kwa kipindi cha miaka mitatu badala ya mwaka mmoja wa sasa."
Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.