Na Joyce Kasiki,Dodoma
NAIBU Waziri wa Fedha,Hamad Hassan Chande amewataka wafanyakazi wa Ofisi za Taifa za Takwimu Bara na Zanzibar kufanya kazi kwa weledi,bidii na maarifa.
Aidha amewataka vijana na watumishi wote wa ofisi hizo mbili kutoridhika na elimu waliyonayo bali wajiendeleze kimasomo kwa lengo la kuongeza ufanisi na tija.
Akifungua Mkutano wa wafanyakazi wa Ofisi za Takwimu za Taifa Tanzania Bara na Zanzibar ,Chande amesema kujienseleza kimasomo ni muhimu kwani kunaongeza ujuzi ambao unakuwa na tija kwa vijana na Taifa kwa ujumla.
"Sasa vijana hawa wanatakiwa wapewe hiyo fursa ya kwenda kujiendeleza kimasomo ,hii itawaongezea ufanisi na tija,lakini pia wanaofanya vizuri wapewe motisha."amesema Chande
Chande ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa Taasisi nyingine zilizopo katika Wizara ya Fedha kuwa na vikao vinavyojumuisha wafanyakazi kutoka Zanzibar na Bara kwa ajili ya kuendelea kujenga umoja na upendo miongoni mwao lakini pia kudunisha Muungano.
pitisha vikao kama hivyo ambavyo vinahusisha Tanzania Bara na Visiwani.
Awali Mtakwimu Mkuu wa Serikali,Dkt. Albina Chuwa amesema lengo la kikao hicho kujadili mafanikio na changamoto katika Ofisi za takwimu Tanzania Bara na Zanzibar.
Anasema kikao hicho kimelenga kuwaunganisha pamoja wafanyakazi wa pande hizo mbili ili kuondoa tofauti miongoni mwao.
Naye,Mwenyekiti wa Tughe Tawi la Takwimu Shagilu Shagilu amewataka wafanyakazi kutunza utu na uadilifu.
Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Salum Kassim Ally amesema mkutano huo ni adimu huku akiwasihi wafanyakazi kushiriki mkutano huo kikamilifu.
"Takwimu ni tasnia mtambuka ila bado tuna nafasi ya kuzalisha takwimu zenye kiwango cha Kitaifa na kimataifa."amesema
Kamisaa wa Sensa Tanzania Bara, Anne Makinda amesema lazima wafanyakazi wa takwimu wajitahidi kusoma ili wawe na ubora zaidi huku akiwataka kuwa na maadili na uaminifu.
Xxxxxxx
No comments:
Post a Comment