TAFORI yafanya Tafiti 5 kuongeza tija katika viwanda vya mazao ya misitu Nchini


Published from Blogger Prime Android App
Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki



Na Joyce Kasiki,Dodoma

SERIKALI imesema,Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)   imefanya jumla ya tafiti 17 zikiwemo tafiti tano za kimkakati ambapo Tafiti  zilizofanyika ni pamoja na tathmini ya rasilimali za misitu kwa ajili ya kuongeza tija katika viwanda vya mazao ya misitu Nchini.

 Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma leo 31 mwaka huu wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2024/26.

Amesema tathmini hiyo imefanyika katika Mikoa ya Kanda za Magharibi, Kati, Nyanda za Juu Kusini na Ziwa ambapo imebainika kuwepo kwa viwanda takriban 940 vya msingi (viwanda vinavyopokea malighafi moja kwa moja kutoka msituni) vyenye mahitaji ya malighafi za mita za ujazo 7,473,826. 

"Tathmini imebaini kuwa malighafi zinazopatikana kwa sasa ni mita za ujazo 3,772,239 sawa na asilimia 50 ya mahitaji huku akisema pia tathimini hiyo  imebaini uwepo wa takriban hekta 266,457.98 zilizopandwa miti kwa ajili ya kutoa malighafi kwenye viwanda vya misitu vilivyopo Nchini. "Amesema Kairuki

Amesema,upungufu wa malighafi uliopo unaonesha kuwa uwekezaji kwenye viwanda vya misitu ni mkubwa kuliko kasi ya upandaji miti. 

Ametumia nafasi hiyo kutoa  rai kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo iliyopo kwa kuanzisha mashamba ya miti katika maeneo yao.

Kwa mujibu wa Kairuki,TAFORI pia imefanya tathmini ya idadi ya miti, hali ya masoko na mchango 
wa miti jamii ya Mkurungu ,Msandali (Osyris lanceolate), na Msekeseke ambayo ina mahitaji makubwa sokoni.

 Amesema tathmini hiyo imefanyika katika Mikoa ya Tabora, Katavi, Kigoma, Songwe, Lindi, Ruvuma, 
Dodoma, Manyara, Arusha, Tanga na Iringa ambapo matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa miti hii inapatikanakatika maeneo husika na hupatikana kwa viwango tofauti kati ya jamii moja na nyingine katika misitu iliyohifadhiwa.

Kairuki amesema mahitaji ya miti jamii ya Mkurungu 
kwenye soko la kimataifa kwa Mwaka ni takriban mita za ujazo 188,440 ambapo Tanzania inachangia asilimia 7.4 sawa na mita za ujazo 13,883. 

"Kwa kutambua umuhimu wa aina hii ya miti, Wizara imeweka mkakati wa kuhakikisha kuwa inaendelea 
kuhifadhiwa na kuimarisha upatikanaji wake kwa 
miaka mingi ijayo,

"Miongoni mwa mikakati iliyopo ni pamoja na kukusanya mbegu za miti hiyo na kuanzisha vitalu vya miche kimkakati kwa jamii hiyo ya miti na miti mingine ya asili katika vituo vya Morogoro, Babati, Mlele na Rondo."amesema Kairuki
 
Amesema,katika kuhakikisha kuwa changamoto zilizopo kwenye sekta ya ufugaji nyuki hasa zile zinazohusu uzalishaji wa asali zinapata 
ufumbuzi, TAFORI inaendelea na utafiti wa Miaka mitatu utakaokamilika Mwaka 2025 unaohusu maeneo yanayofaa kwa ufugaji nyuki katika kanda mbalimbali za kilimo-ikolojia; aina ya mizinga inayofaa kwenye kila kanda ya kilimo-ikolojia; na uwezo wa Nchi wa kuzalisha asali pamoja na sifa za asali zinazozalishwa. 

Vilevile amesema , utafiti unaangalia athari za spishi za mimea vamizi kwenye ufugaji wa nyuki; pamoja na kuandaa kalenda ya ufugaji nyuki kwa kila kanda ya kilimoikolojia.

 "Utafiti huu umeanza kufanyika katika wilaya za Kongwa, Chamwino, Manyoni, Sikonge, Kasulu, Mlele, Bukombe, Butiama, Itilima, Morogoro, Kibiti, Handeni, Pangani, Mtama, Tunduru, Mufindi, Njombe, Chunya, Siha, Same na Simanjiro,

 "Matokeo ya awali yanaonesha kuwa maeneo yanayofaa kwa ufugaji nyuki yametawaliwa na uoto wa Miombo, Migunga,Afromontane (uoto wa mlimani), Mikoko pamoja na uoto wa vichaka vya Itigi,na utafiti huu umesaidia kubaini maeneo yenye uwezo wa kutoa asali yenye sifa za kipekee."amesisitiza

Katika hatua nyingine Kairuki amesema,katika   kuhakikisha kuwa takwimu za misitu na ufugaji nyuki zinahifadhiwa na kupatikana kwa wakati, TAFORI imeboresha mfumo wa kieletroniki wa kuhifadhi na kutoa taarifa za misitu na nyuki kwa kuanzisha moduli inayotoa nafasi kwa wadau kuwasilisha taarifa za tafiti na miradi wanayotekeleza inayohusu Sekta za Misitu na Nyuki 
ambapo kwa sasa wadau wameanza kuitikia wito wa kuwasilisha takwimu. 

Aidha amesema , Taasisi ya TAFORI 
inaendelea na zoezi la kuhamasisha wadau kujiunga kwenye mfumo huu. Kwa upande mwingine, TAFORI imekamilisha ukusanyaji wa taarifa za mazao na 
huduma mbalimbali za misitu na nyuki kwa ajili ya kufanya tathmini ya mchango wa sekta ya misitu 
kwenye Pato la Taifa (GDP) kwa kutumia “Green Accounting’’.
Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.