RAIS SAMIA ATOA MAELEKEZO KWA JESHI LA POLISI


Published from Blogger Prime Android App


Na Joyce Kasiki,DODOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amelitaka  Jeshi la PolisiNchini kkuongeza nguvu katika kukomesha matukio ya watu kupotea nchini.

Rais Dkt.Samia ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma , Leo Juni 27,2025 wakati akihitimisha rasmi Bunge la 12 

Amesema kuwa pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano ya Bunge hilo, bado yapo mambo yanayohitaji kushughulikiwa kwa dharura, likiwemo suala la usalama wa raia, hasa katika matukio ya watu kutoweka bila maelezo.

"Jeshi la Polisi lina wajibu wa kuhakikisha usalama wa wananchi, na mojawapo ya vipaumbele vyake sasa ni kuhakikisha kuwa matukio ya watu kupotea yanakomeshwa kabisa,” alisisitiza Rais Dkt. Samia
Share:

RAIS DKT. SAMIA AZUNGUMZA WAKATI WA KULIFUNGA BUNGE LA 12: "WABUNGE MMETIMIZA WAJIBU WENU KWA WELEDI NA UZALENDO"


Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki,DODOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amelihutubia Bunge la Kumi na Mbili katika hafla ya kulifunga rasmi, huku akilipongeza Bunge hilo kwa kazi kubwa na nzuri ya kutunga sheria, kuisimamia serikali, na kuwakilisha wananchi kwa weledi na uzalendo mkubwa.

Akizungumza ndani ya Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, Rais Samia alimpongeza Mheshimiwa Spika Dkt. Tulia Ackson kwa kuliongoza Bunge kwa umahiri mkubwa, licha ya changamoto zinazotokana na tofauti za kisiasa na mitazamo ya wabunge mbalimbali.

"Mheshimiwa Spika, kuliongoza Bunge si kazi rahisi. Kwenye wengi kunamengi, lakini kwa umahiri wako na weledi, umeweza kuivusha mashua yetu salama hadi bandari, kama manahodha mahiri wa baharini,” alisema Rais Samia huku akishangiliwa na wabunge.

Rais Samia pia alitambua mafanikio ya kihistoria ya Spika Dkt. Tulia Ackson kwa kuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kushika nafasi ya Urais wa Mabunge ya Afrika (PAP), akisema mafanikio hayo yameongeza heshima ya Tanzania kimataifa.

Katika hotuba yake, Rais aliwapongeza wabunge wote kwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kushiriki kikamilifu katika kujadili sera na mipango ya maendeleo ya taifa. Alisema kuwa Bunge hilo limekuwa na mchango mkubwa katika kujenga ustawi wa wananchi na kuleta maendeleo ya kweli.

"Nitumie fursa hii kulitushukuru Bunge kwa tuzo mlionipatia. Ninathamini kwa dhati kutambua kwenu mchango wangu katika maendeleo na ustawi wa nchi yetu,” alisema Rais.

Share:

WANANCHI SHINYANGA WAOMBA KUONGEZEWA SIKU ZA MADAKTARI BINGWA WA SAMIA

 

Published from Blogger Prime Android App



Na WAF, Shinyanga 

Wananchi mkoani Shinyanga wameomba kama kuna uwezekano wa kuongezwa siku za Madaktari Bingwa na Bobezi wa Rais Samia ili changamoto za Afya zinazowakabili ziweze kutatuliwa.

Hali hiyo imejitokeza Juni 25, 2025 ikiwa ni siku tatu tu, tangu kuanza kwa kambi ya madaktari bingwa wa Rais Samia  mkoani hapo. 

"Hatujui kwa wingi wetu huu kama kweli hizi siku sita zilizopangwa kama zitatutosha kama unavyoweza kuona Umati huu wa watu waliokuja kupata huduma za kibingwa," amesema Mzee John Mandu mkazi wa Chamaguha mkoani Shinyanga.

Kwa uoande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Manispaa Dkt. Moshi Ryioba amesema kumekuwa na ongezeko la idadi ya watu ikilinganishwa na siku zingine ambazo hazikuwa na Madaktari Bingwa.

"Tumepokea wananchi waliokuja kwa siku moja 167, hii sio hali ya kawaida kwani idadi ya kawaida huwa ni watu kati ya 50 hadi 70  kwa siku za kawaida," amesema Dkt. Ryioba.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji Dkt. Boazi Mwasambili kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, amekiri kupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wenyeji wake na kufanikisha Operesheni mbili huku akijiandaa kufanya zingine nne (4). 

"Kama unavyoweza kuona hapa nipo na wataalam wawili, ambao tumekuwa nao bega kwa bega tangu siku ya kwanza kuna siku tulitoka hapa karibu saa mbili za usiku lakini hawajaacha kunipatia ushirikiano wakutosha," amesema Dkt. Mwasambili. 

Madaktari Bingwa walioweka kambi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ni pamoja na Daktari bingwa Watoto, Wanawake, Upasuaji, Pua, Koo na Sikio, Magonjwa ya ndani, Meno pamoja na Wauguzi Mabingwa.
Share:

Waziri Jenista Mhagama: Mkataba wa Huduma Bora kwa Wateja kuchochea huduma bora




Published from Blogger Prime Android App




Joyce Kasiki,DODOMA

Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, amezindua rasmi Mkataba wa Huduma Bora kwa Wateja, hatua inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya na kuongeza uwajibikaji miongoni mwa watoa huduma katika vituo vyote vya afya nchini.

Akizungumza leo, Juni 25, 2025 jijini Dodoma katika hafla fupi ya uzinduzi wa mkataba huo, Waziri Mhagama ameagiza utekelezaji wake ufanyike kwa haraka na kwa ufanisi katika ngazi zote — kuanzia zahanati hadi hospitali za rufaa, taasisi na vituo vya afya binafsi.

"Ndani ya muda mfupi sana, nataka kuona kila kituo cha afya nchini kikiwa kimekamilisha mkataba huu. Hii ni pamoja na Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya, Rufaa za Mikoa na Kanda, pamoja na Taasisi zote za afya,” amesema Waziri Mhagama.

Aidha, amesisitiza kuwa mkataba huo si tu utakaoainisha haki na wajibu wa watoa huduma na wagonjwa, bali pia utatoa mwongozo wa gharama na viwango vinavyopaswa kuzingatiwa ili kuhakikisha huduma bora, za haki, na zenye uwiano sawa.

Waziri Mhagama amesema mkataba huo pia utawezesha utoaji wa taarifa muhimu kwa wagonjwa kabla ya matibabu, jambo linalojenga imani na kuondoa sintofahamu.

"Ni matarajio yangu kuwa kupitia mkataba huu, kila mmoja atatimiza wajibu wake. Hii itasaidia kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima na kuifikisha sekta ya afya pale ambapo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka ifike,” ameongeza.

Katika hotuba yake, Waziri huyo pia amepongeza juhudi za Rais Samia katika kuimarisha sekta ya afya kwa kuwekeza katika mafunzo ya wataalamu wa afya, ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa kama MRI, PET-Scan na mashine za X-Ray — vifaa ambavyo amesema ni adimu hata kwa baadhi ya mataifa mengine.

Aidha, amesema mkataba huo unaendana na dira ya Wizara ya Afya ya kujenga jamii yenye ustawi bora inayochangia kikamilifu maendeleo ya taifa, sambamba na dhima ya utoaji wa huduma bora za afya kwa wote.

"Kazi kubwa tuliyobakiwa nayo sasa ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora bila kikwazo cha fedha. Tumeshatekeleza bima ya afya kwa wote, sasa tunalenga kuhakikisha fedha za kuendeleza huduma zinapatikana ili tuendelee kuwekeza zaidi,” amesema.

Pamoja na hayo, mkataba huo umeainisha huduma zitakazotolewa ikiwa ni pamoja na ushauri wa kitaalamu wa masuala ya afya, huduma za chanjo, utoaji wa vyeti vya usajili wa kitaaluma, leseni na vibali, pamoja na taarifa mbalimbali za sekta ya afya.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Seif Shekalage, amesema mkataba huo utaimarisha zaidi utendaji kazi na kuongeza uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa sekta hiyo.


Share:

Waziri Mkuu Majaliwa azindua Mfumo wa kubadilisha taarifa

Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), akizindua rasmi Mfumo wa Kubadilishana Taarifa Serikalini (Government Enterprise Service Bus - GovESB) kwa kutumia kishkwambi, katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2025, katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.


Mfumo wa GovESB umesanifiwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao(e-GA) ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Tanzania Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan na Sheria ya Serikali Mtandao Namba 10, ya mwaka 2019, ya kuhakikisha mifumo yote ya taasisi za umma inasoma na kubadilishana taarifa, ili kuboresha huduma kwa wananchi.



Published from Blogger Prime Android App
Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.