Wagombea kiri cha Rais na Makamu wa Rais SAU nao wachukua fomu INEC


Published from Blogger Prime Android App
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Jacobs Mwambejele akiwakabidhi mkoba wenye fomu za kuwania kiti cha urais wagombea kutoka chama cha sauti ya Umma ( SAU).Majalio Paul Kyara (mgombea kiti cha Rsis) na Mhe. Satia
Mussa Bebwa (kushoto) Kiti cha Makamu wa Rais

Published from Blogger Prime Android App

Wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mhe.
Majalio Paul Kyara na Mhe. Satia
Mussa Bebwa (kushoto) wakionesha mkoba wa fomu za uteuzi waliokabidhiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi leo Agosti 13, 2025
Share:

Chama cha DP wachukua fomu kuwani kiti cha Rais na Makamu wa Rais uchaguzi Mkuu ujao


Na Mwandishi Wetu,INEC

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP), Mhe. Abdul Juma Mluya. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Sadoun Abrahman Khatib (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 13, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. (Picha na INEC).

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Mhe. Abdul Juma Mluya. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Sadoun Abrahman Khatib (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 13, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima. 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhani Kailima, akimwelekeza Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Mhe. Abdul Juma Mluya
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Mhe. Abdul Juma Mluya akisaini kitabu.

Mgombea Mwenza, Mhe. Sadoun Abrahman Khatib akisaini kitabu huku akishuhudiwa na Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Mhe. Abdul Juma Mluya akisaini kitabu.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza, Kushoto aliyeketi ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk. 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza, Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk na kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima.
Share:

TAWA YASAINI MIKATABA YA UWEKEZAJI MAHIRI YENYE THAMANI YA TZS BILIONI 719


Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App




📍 Neema yaja kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya uwekezaji

Na Beatus Maganja, Dar es Salaam

Katika hatua ya kihistoria na kishindo kwa sekta ya utalii nchini, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), leo Agosti 12, 2025, imesaini mikataba minne ya uwekezaji wa utalii kupitia utaratibu wa Uwekezaji Mahiri (SWICA) na kampuni ya kitanzania ya Uhusiano International ICT Ltd.

Mikataba hiyo inatarajiwa kuingiza mapato ya Dola za Marekani milioni 281.5 (sawa na Shilingi Bilioni 719 za Kitanzania) kwa kipindi cha miaka 20 ikiwa ni wastani wa Shilingi Bilioni 36 kwa mwaka.

Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam na imehusu uwekezaji katika vitalu vinne vya Burko Open Area (Monduli – Arusha), Selous MHJ1, Selous MHJ2 na Selous ML1 (Liwale – Lindi), vyote vikiwa chini ya kampuni ya Uhusiano International ICT Ltd inayomilikiwa na Watanzania kwa asilimia 100.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana amesema uwekezaji huo utaimarisha sekta ya uwindaji wa kitalii na utalii wa picha, sambamba na kuleta ajira, kuboresha huduma za jamii na kuchochea maendeleo ya wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya uwekezaji. Miradi ya maendeleo itakayoibuliwa na wananchi wenyewe inakadiriwa kugharimu Dola milioni 1.8 (sawa na Shilingi Bilioni 4.6) kwa miaka 20.

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana pia alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake madhubuti katika kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia filamu za Amazing Tanzania na The Royal Tour, zilizochochea ongezeko la watalii na wawekezaji.

Aliahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kusisitiza umuhimu wa matumizi endelevu ya rasilimali kwa kuzingatia sheria, kanuni na misingi ya uhifadhi bora. Alitoa wito kwa wawekezaji zaidi kuja kuwekeza katika vivutio vya kipekee vya utalii vilivyopo nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA, Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis R. Semfuko, amesema TAWA imepiga hatua kubwa kwa kusaini mikataba minne mipya ya SWICA na kufikisha jumla ya mikataba 13 kati ya 14 iliyopangwa  sawa na asilimia 92.3 ya lengo, hatua iliyowezesha kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 27.4 kati ya Januari 2024 na Agosti 2025.

Aidha, Meja Jenerali Semfuko alibainisha kuwa TAWA ipo katika hatua za mwisho kusaini mkataba na kampuni ya GBP Trading Ltd (GTL) kwa ajili ya ujenzi wa kambi za kudumu za kitalii katika hifadhi za Kijereshi, Mpanga-Kipengere na Wami-Mbiki, hatua itakayoongeza vitanda 240 na kupunguza uhaba wa malazi kwa watalii.

Awali, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, Bw. Mlage Yusuph Kabange, alisema tangu kusainiwa kwa mikataba ya awali ya SWICA mwaka 2024, TAWA imeshuhudia ongezeko kubwa la mapato  kutoka Shilingi Bilioni 55 hadi Shilingi Bilioni 87.12 katika mwaka wa fedha 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 158.2.

Aliongeza kuwa TAWA inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa uwekezaji, ikiwemo ujenzi wa kilomita 453.2 za barabara kwa kiwango cha changarawe katika maeneo ya kimkakati  sawa na asilimia 40 ya lengo la kujenga kilomita 1,127 ifikapo mwaka 2026.

Kamishna Kabange alisisitiza kuwa TAWA ipo tayari kushirikiana na wawekezaji ili kuhakikisha utekelezaji bora wa mikataba hiyo kwa manufaa ya Taifa na wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Kampuni ya Uhusiano International ICT Ltd, Bw. Zahir Hassan Mulla, alitoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Maliasili na Utalii, pamoja na Bodi na Menejimenti ya TAWA kwa kuridhia pendekezo lao la uwekezaji. Alisema huu ni mwanzo mzuri kwa wawekezaji wa ndani kuonesha uwezo wao katika sekta ya utalii.
Share:

Dkt.Biteko:Watanzania tusikubali uchaguzi utugawe


Published from Blogger Prime Android App



📌 Asema Kuna Maisha baada ya Uchaguzi

📌 Amwakilisha Rais Samia,miaka 40 Kanisa Anglikana Dayosisi ya Kagera

📌 Rais Samia achangia Tsh. Milioni 50 Ujenzi wa Kanisa Dayosisi ya Kagera

📌 Anglikana Waishukuru Serikali, washirika wa maendeleo

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kuwapima wagombea wa nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu ujao na kuchagua kwa haki ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025 (mwaka huu) na katu wasikubali Uchaguzi uwagawe.

Dkt. Biteko amesema hayo Agosti 12, 2025 wakati akimwakilisha Mheshimiwa Rais katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa kwa Dayosisi ya Kagera iliyofanyika katika Viwanja vya Kanisa Kuu Yohana Mbatizaji – Murgwanza, Ngara.

Amesema kuwa watanzania wanayo haki ya kuwapima wagombea kwa matendo yao na hatimaye kutenda haki kwa kufanya uchaguzi wao kwa njia ya demokrasia huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia kampeni za kistaarabu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa maadili.

Akiwasilisha salamu za Mheshimiwa Rais, Dkt. Biteko amesema Dkt. Samia anatambua na kuheshimu mchango wa taasisi za dini na mchango wake katika maendeleo ya Taifa. “ Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni mdau wa kujenga na kila mnachokifanya kinalenga katika maendeleo ya watu hivyo anaunga mkono jitihada za maendeleo ya wananchi,” amesema Dkt. Biteko.

Katika kufanikisha azma yake, Rais Dkt. Samia amechangia shilingi milioni hamsini (50,000,000/=) katika harambee ya ujenzi wa Kanisa jipya la Anglikana Dayosisi ya Kagera.

Dkt. Biteko Amesisitiza umuhimu wa kila mtu kuwa kisababishi cha furaha kwa mwenzake ili kuwa na maisha ya ya furaha.

Awali, Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Kagera, Darlington Misango Bendankeha ameishukuru Serikali kwa ushirikiano mkubwa unaopatikana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Askofu Bendankeha amesisitiza kuwa Serikali katika ngazi zote inatoa ushirikiano na hivyo kufanikisha utekelezaji wa miradi ya Afya, Elimu kwa maendeleo ya jamii.

Ameiomba Serikali kufanikisha ujenzi wa Barabara inayounganisha taasisi mbalimbali za utoaji wa huduma yenye urefu wa mita 900, Gari la wagonjwa pamoja na mchango wa ujenzi Kanisa ambalo ujenzi wake unaendelea kwa gharama ya shilingi Bilioni 1.18

Kufuatia maombi hayo, Dkt. Biteko amemwelekeza Mkuu wa Mkoa, Mkuu Wilaya na Wakala wa Barabara mijini na vijijini (TARURA) kufanikisha ujenzi wa Kipande hicho huku akitoa ahadi ya gari la wagonjwa katika Hospitali ya Murgwanza baada ya kuwasiliana na Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama.

Akizungumzia uchaguzi Mkuu ujao, Askofu Bendankeha amewahimiza wananchi kushiriki kikamilifu na kuwachagua viongozi wao katika uchaguzi Mkuu ujao ili kuchochea maendeleo “ Tujiandae kushiriki uchaguzi Mkuu ujao, kura yetu ndiyo nguvu ya mabadiliko.” Amesema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Fatuma Mwassa amelipongeza Kanisa la Anglikana Tanzania kwa huduma mbalimbali za maenseleo zinazotolewa kwa jamii.

Share:

Wanahabari wachukua fomu kuwania kiti cha Urais na Makamu wa Rais ,ni Mwalimu na Minja

Na Mwansiahi Wetu Dodoma 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) Mhe. Salum Mwalimu. Mgombea huyo alichukua fomu hizo leo Agosti 12, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. (Picha na INEC).

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Mhe. Salum Mwalimu. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Devotha Mathew Minja (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 12, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima.  (Picha na INEC).
Waandishi wa Habari, Salum Mwalimu aliyepata kufanya kazi katika kituo cha Televisheni cha Channel Ten na Devotha Minja aliyekuwa mwandishi wa ITV mkoa wa Morogoro leo wamechukua mkoba wa fomu za uteuzi wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais kupitia Chama cha CHAUMA. Wagombea hao pichani wakiwa na mkoba wao wa fomu za uteuzi.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza. 
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza. 

Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) Mhe. Salum Mwalimu akielekeza namna ya kujaza kitabu.
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) Mhe. Salum Mwalimu akisaini kitabu.
Mgombea Mwenza Mhe. Devotha Minja akisaini kitabu
Mgombea Mwenza Mhe. Devotha Minja akisaini kitabu
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhani Kilima akizungumza.


Baadhi ya wajumbe wa Tume wakiwa katika utoaji fomu.

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Chauma wakiwa katika utoaji fomu.

Mwenyekiti wa Chauma Mhe. Hashim Rungwe akiwa Benson Kigaila
Share:

TBN yatoa onyo kali kwa Manabii wa mtandaoni,yataka sheria ichukue mkondo wake




Published from Blogger Prime Android App

Na Mwandishi wetu

Mtandao wa Bloga Tanzania (TBN) umekemea vikali tabia inayoshamiri ya watu kujinadi kufanya utabiri kwa watu na taifa kupitia mitandao ya kijamii, ukisema vitendo hivyo vinakiuka Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Kauli hiyo imetolewa kama azimio katika kikao kazi cha mafunzo ya mabloga kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Mabloga hao wameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kushirikiana kuwasaka na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaohusika na vitendo hivyo.

Katika kikao hicho, mabloga walibainisha kuwa kumeibuka kundi la watu wanaodai kuwa ni manabii na kutoa kauli zinazokiuka sheria za nchi na kuleta taharuki kuelekea uchaguzi. Walisisitiza kuwa baada ya kuchambua Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (Personal Data Protection Act), walibaini kwamba 'utabiri' wa namna hiyo unavuruga haki ya msingi ya faragha ya wahusika.

Kwa mujibu wa Bw. Innocent Mungy, mtoa mada kutoka Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), sheria hiyo inakataza mtu kuzungumziwa kuhusu afya yake, mwenendo, au taarifa zake binafsi kutolewa bila ridhaa yake. Mungy alisisitiza kuwa sheria hii ina adhabu kali na lazima ifuatwe na kila mtu, si tu mabloga na waandishi wa habari.

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na TCRA, yalilenga kuwaandaa mabloga kuripoti habari za uchaguzi kwa weledi na uadilifu. 

Pamoja na mada ya ulinzi wa taarifa binafsi, mada nyingine muhimu zilizotolewa ni pamoja na Mwongozo wa Waandishi wa Habari katika Uchaguzi na Matumizi ya Akili Mnemba (AI) katika uandishi wa habari.

Lengo kuu la mafunzo haya ni kuongeza uwezo wa mabloga kuhakikisha wanafuata sheria na maadili ya uandishi, jambo linalotazamiwa kuchangia mazingira ya uchaguzi yenye amani na utulivu.

@@@@@@@@@@@@@
Share:

RAIS SAMIA AAHIDI KUENZI MCHANGO WA HAYATI JOB NDUGAI


Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App




Na Joyce Kasiki.Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaongiza viongozi mbalimbali wa Kitaifa kutoa salamu za rambirambi na kumkumbuka aliyekuwa Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, katika ibada ya kuuaga mwili wake jijini Dodoma.

Aidha ,viongozi hao wamemtaja Ndugai kama kiongozi mwenye maono, mbunifu na mpenda maridhiano.

Akizungumza katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, mara baada ya ibada maalumu ya kuuaga mwili wa marehemu, Rais Samia  
ameahidi kwamba  Serikali itaendelea kuenzi na kudumisha mchango mkubwa wa kimaendeleo uliotolewa na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Job Yustino Ndugai

Hayati Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi wachapakazi waliotoa mchango mkubwa katika kuimarisha elimu, hususan kwa vijana wa Jimbo la Kongwa ambako alilitumikia kwa kipindi kirefu kama Mbunge.

“Kupitia utumishi wake, tumeshuhudia jitihada kubwa katika kuhakikisha vijana wanapata elimu bora na fursa za maendeleo. Kifo chake ni pigo kubwa si tu kwa familia na wananchi wa Kongwa, bali kwa taifa zima. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuifariji familia yake na kuwaongoza katika kipindi hiki kigumu,” alisema Rais Samia.

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, alisema chombo hicho kinatoa shukrani kwa wote walioungana nacho katika kipindi hiki cha majonzi, kufuatia kuondokewa na kiongozi na ndugu waliyempenda.

“Kifo hiki kimeshtua wengi, hasa tukizingatia tupo katika mchakato wa uchaguzi, lakini Mungu ndiye mpangaji wa kila jambo, hivyo tunashukuru kwa yote,” alisema.

Dkt. Tulia alimwelezea marehemu Ndugai kama kiongozi aliyekuwa akitekeleza maneno yake kwa vitendo, bila kubagua chama, na aliyeleta mageuzi makubwa ndani ya Bunge.

Alitaja ubunifu wa kuendesha vikao kwa njia ya mtandao wakati wa janga la korona kama mfano wa fikra zake za kimapinduzi.

Aliongeza kuwa katika kipindi chake cha uongozi, Ndugai alisimamia utekelezaji wa sheria ya kuhamishia makao makuu ya Serikali Dodoma, akihakikisha Bunge linaendelea kulinda heshima yake.

“Alikuwa mpambanaji dhidi ya utovu wa nidhamu na mleta maridhiano, huku wabunge wapya wakimwona kama mwalimu kwa namna alivyowaongoza,” alisema.

Dkt. Tulia aliwaombea faraja familia ya marehemu, akisema maisha yake yatabaki kuwa dira na somo kwa wote.

Aidha, alionya kuhusu baadhi ya watu wachache wanaotoa kauli za kuumiza familia, akisisitiza kuwa wema alioutenda unazidi kwa wingi maneno machache ya kuumiza.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatoa pole kwa Bunge na Watanzania wote walioguswa na msiba huo, akisema kazi ya Mungu haina makosa. 

“Tunashukuru kwa ushirikiano tulioupata kutoka kwake katika kipindi cha uhai wake, na tunamuombea apumzike mahali pema peponi,” alisema.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, naye alieleza masikitiko makubwa kwa kuondokewa na kiongozi aliyeitumikia nchi kwa bidii na uadilifu. 

“Msiba huu umetokea ghafla na umetuumiza, lakini hakuna budi kuupokea,” alisema.

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, alisema Ndugai alikuwa rafiki na mshauri wa karibu, akimkumbuka tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.

“Msiba huu ni mkubwa na ni msiba wa kila mmoja wetu. Tumempoteza mtu wa thamani sana,” alisema.

Mwili wa marehemu Ndugai uliagwa leo kabla ya kusafirishwa kwenda wilayani Kongwa kwa maziko, huku mamia ya wananchi, wabunge na viongozi wa Serikali wakihudhuria shughuli hiyo ya kumuaga.






























Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule, alieleza kuwa Hayati Ndugai ameacha alama tatu muhimu katika mkoa wa Dodoma, ambazo ni: kuimarisha nidhamu na uwajibikaji katika vikao vya kimaendeleo, kufanya mapinduzi ya elimu hasa wilayani Kondoa, na kuhimiza kilimo cha zao la korosho katika wilaya za Kongwa na Mpwapwa.

Awali, Katibu wa Bunge, Bw. Baraka Leonard, akisoma wasifu wa marehemu, alieleza kuwa Hayati Ndugai alifariki dunia mnamo tarehe 6 Agosti 2025, majira ya saa 9 alasiri jijini Dodoma, kutokana na shinikizo la damu kushuka kwa kiwango kikubwa (septic shock) kilichotokana na maambukizi makali ya mfumo wa hewa (severe pneumonia).

Katika maisha yake ya utumishi kwa umma, Ndugai alishikilia nyadhifa mbalimbali zenye mchango mkubwa kwa taifa, zikiwemo:

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Wildlife Protection Fund (2001–2004),

Mjumbe wa Bodi ya Hifadhi ya Ngorongoro (2007–2010),

Mjumbe wa Baraza la Seneti la Chuo Kikuu cha Dodoma (2007–2010),

Mjumbe wa Bodi ya Uwekezaji ya Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola – Kanda ya Afrika (2015–2022).


Mbali na nafasi za kitaasisi, Hayati Ndugai pia alikuwa muumini wa Kanisa la Anglikana Tanzania na alihudumu kama Mzee wa Kanisa, na hadi umauti unamkuta alikuwa Lay Canon wa Dayosisi ya Mpwapwa – nafasi ya heshima inayomhusisha na ushauri wa kiroho kwa Askofu.

Hayati Job Yustino Ndugai alizaliwa tarehe 21 Januari 1963 katika Kijiji cha Laikala, Kata ya Sagara, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 65, na ameacha mke, watoto na wajukuu.
Share:

TCRA yatoa Ratiba ya mafunzo kwa TBN kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025




Published from Blogger Prime Android App





Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeandaa mafunzo maalumu kwa Mtandao wa Mabloga  (TBN) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Mafunzo haya yatafanyika Jumatatu, Agosti 11, 2025, katika Makao Makuu ya TCRA.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka TCRA mafunzo hayo yana lengo la kuwaandaa mabloga na wanahabari kwa ujumla ili waweze kuripoti habari za uchaguzi kwa weledi na uadilifu. 

Mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wataalamu kutoka taasisi tofauti. Baadhi ya mada zitakazojadiliwa ni pamoja na Mwongozo wa Waandishi wa Habari katika Uandishi wa Habari za Uchaguzi, Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa za Mwaka 2020, na uhusiano kati ya Waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi katika kulinda usalama.

Mada nyingi zitatoka Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, itakayozungumzia maadili na sheria kwa waandishi wa habari, mada kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii na Akili Bandia (AI) kuelekea uchaguzi na mada kutoka Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) itakayozungumzia Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuelekea uchaguzi.

Mafunzo haya yana faida kubwa kwa mabloga na jamii kwa ujumla kwani yatawawezesha wanahabari kutoa taarifa sahihi na zenye uwajibikaji, jambo ambalo ni muhimu katika kujenga mazingira ya uchaguzi yenye amani na utulivu.

Pia, yanatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na Akili Bandia ili kuepuka taarifa za uongo.

mwisho

















TCRA yatoa Ratiba ya mafunzo kwa TBN kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeandaa mafunzo maalumu kwa Mtandao wa Mabloga  (TBN) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Mafunzo haya yatafanyika Jumatatu, Agosti 11, 2025, katika Makao Makuu ya TCRA.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka TCRA mafunzo hayo yana lengo la kuwaandaa mabloga na wanahabari kwa ujumla ili waweze kuripoti habari za uchaguzi kwa weledi na uadilifu. 

Mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wataalamu kutoka taasisi tofauti. Baadhi ya mada zitakazojadiliwa ni pamoja na Mwongozo wa Waandishi wa Habari katika Uandishi wa Habari za Uchaguzi, Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa za Mwaka 2020, na uhusiano kati ya Waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi katika kulinda usalama.

Mada nyingi zitatoka Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, itakayozungumzia maadili na sheria kwa waandishi wa habari, mada kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii na Akili Bandia (AI) kuelekea uchaguzi na mada kutoka Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) itakayozungumzia Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuelekea uchaguzi.

Mafunzo haya yana faida kubwa kwa mabloga na jamii kwa ujumla kwani yatawawezesha wanahabari kutoa taarifa sahihi na zenye uwajibikaji, jambo ambalo ni muhimu katika kujenga mazingira ya uchaguzi yenye amani na utulivu.

Pia, yanatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na Akili Bandia ili kuepuka taarifa za uongo.

mwisho
Share:

Tanzania  yang'ara maonyesho ya 97 ya kilimo na Biashara Zambia


Published from Blogger Prime Android App


 

Na Abdallah Nassoro- MOI

TAMZANIA  imeibuka mshindi wa pili katika maonesho ya kimataifa ya 97 ya kilimo na biashara yaliyofanyika Lusaka, Zambia kuanzia tarehe 29 Julai hadi 4 Agosti 2025.

Tanzania imetangazwa kuwa mshindi wa pili kati ya nchi 25 zilizoshiriki maonesho hayo ikitanguliwa na Zimbabwe iliyoshika nafasi ya kwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 8, 2025 katika ukumbi wa MOI, Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema ushindi wa Tanzania umetokana na maelezo ya kina na elimu iliyotolewa na wataalam kuhusu huduma za afya za kibingwa na  kibobezi  zinazopatikana Tanzania, pamoja na sekta ya usafirishaji.

“Taasisi tano zilishiriki katika maonesho hayo zikiwemo MOI, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya (MZRH), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la ndege la ATCL, kwa ujumla wetu tumefanya vizuri na kushika nafasi ya pili” amesema Dkt. Mpoki

Amesema ushiriki wa Taasisi za afya kutoka Tanzania kwenye maonesho hayo umelenga kuhamasisha utalii tiba ili wagonjwa kutoka Zambia waje Tanzania kupata huduma badala ya kusafiri nje ya bara la Afrika kufuata huduma hizo kwa gharama kubwa. 

“MOI na JKCI tunatoa matibabu ya zaidi ya asilimia 96 ya magonjwa yote ya moyo, mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu, hivyo ni kimbilio sahihi kwa bara la Afrika katika kupata matibabu bora na kwa gharama nafuu … tukiwa Zambia taasisi hizi tatu za afya tumeweza kuona watu 911 kati ya hao 105 wameahidi kuja Tanzania kwa matibabu zaidi” amesema Dkt. Mpoki
 
Ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo uliratibiwa na kusimamiwa na ubalozi wa Tanzania nchini Zambia chini ya Mhe. Balozi Lt. Gen  Mathew Edward Mkingule ambapo pia banda hilo lilitembelewa na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichelema Agosti, 2, 2025.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Utalii Tiba Tanzania Dkt. Peter Kisenge ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisis ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) amesema kamati hiyo imewekeza nguvu kubwa katika kujitangaza ili badala ya kupeleka wangojwa nje ya bara la Afrika kwa kufuata huduma bora na teknolojia ya hali ya juu, sasa wanapaswa kuwaleta wagonjwa wao Tanzania ambako huduma ni bora sawa na sehemu nyingine duniani.

“Awali tulienda visiwa vya Comoro na kutoa huduma kwa watu 2,292 na hadi leo tumepokea wagonjwa zaidi ya 150 katika hospitali zetu za MOI, MNH, JKCI na Ocean road, haya yote ni matunda ya ushiriki wetu kwenye maonesho kama haya” amesema Dkt. Kisenge na kuongeza kuwa 

“Watu wanapoleta wagonjwa Tanzania wanasaidia kukuza uchumi wetu kwasababu watalala katika hoteli zetu, watanunua chakula na huduma zingine muhimu, hayo yote yatachagiza ukuaji wa uchumi na ndio maana tunaita tiba utalii kwa maana anatembea nchi yetu kwa ajili ya kupata matibabu”

Share:

Rais Dkt.Samia kuchukua fomu kesho kuwania urais




Published from Blogger Prime Android App


Na Mwandishi wetu Dodoma 

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM, tarehe 9 Agosti 2025, katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Zoezi hilo linaashiria kuanza rasmi kwa mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba mwaka huu, kwa vyama vyote vya siasa nchini.

Akizungumza leo, Agosti 8, jijini Dodoma, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla, amethibitisha kuwa chama hicho kipo tayari kikamilifu kwa hatua hiyo muhimu ya kidemokrasia. Aidha, alieleza kuwa baada ya kuchukua fomu hiyo, Dkt. Samia atapokelewa katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM, Dodoma, ambako atapata nafasi ya kusalimiana na wananchi.

CPA Makalla amesisitiza kuwa kwa kuwa mgombea Urais anatokana na Chama Cha Mapinduzi, hatua hiyo ni sehemu ya mchakato wa utekelezaji wa maamuzi ya vikao vya juu vya chama kuhusu kuwania nafasi ya Urais kwa kipindi kijacho.

Ikumbukwe kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anachukua fomu hiyo kuwania nafasi ya Urais kwa muhula wa pili wa miaka mitano, ikiwa ni sehemu ya kukamilisha safari ya uongozi wake aliyoianza mwaka 2021.
Share:

MANAIBU MAKATIBU WAKUU OR-TAMISEMI WATEMBELEA BANDA LA TARURA*




Published from Blogger Prime Android App



#Waipongeza kwa kuwafungulia barabara wakulima

Dodoma

Manaibu Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI wakiongozwa na Mhandisi Rogatus Mativila  Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) Sospeter Mtwale - Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI) na Prof. Tumaini Nagu - Naibu Katibu Mkuu (Afya) wametembea Banda la Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika kilele cha Maonesho ya Sikukuu  ya Wakulima Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma.

Makatibu Wakuu hao wamepatiwa maelezo mbalimbali kutoka kwa Wataalamu wa Wakala huo wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Bi. Catherine Sungura kuhusu majukumu, utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na mipango ya TARURA inayohusu uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini. 

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Naibu Katibu Mkuu Sospeter Mtwale amewapongeza TARURA kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kufungua barabara hususan maeneo ya wakulima,wavuvi na wafugaji na hivyo kuwarahisishia kusafirisha mazao yao.

Pia amesema barabara hizo zimesaidia waendesha bodaboda na waendesha vyombo vya moto vingine na hivyo kupata ajira hivyo kuwataka kuendelea kuboresha barabara za vijijini ili ziweze kupitika wakati wote.
Share:

INEC yawasihi Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kusambaza taarifa sahihi kuhusu uchaguzi Mkuu ujao

Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App


Na Joyce Kasiki, Dar Es Dalaam 


 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), Jaji Mstaafu Jacobs Mwambegele, amewasihi wazalishaji wa maudhui mtandaoni kutumia majukwaa yao kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kampeni na upigaji kura kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Akifungua Mkutano wa siku moja wa Kitaifa kati ya INEC na wazalishaji wa maudhui mtandaoni uliofanyika leo Agosti 3,2025  jijini Dar es Salaam, Jaji Mstaafu Mwambegele amesema lengo la mkutano huo ni kuwajengea uwezo wauelewa wa kutosha wazalishaji hao ili waweze kusambaza taarifa sahihi kuhusu masuala ya uchaguzi.

"Wazalishaji wa maudhui mtandaoni ni wadau muhimu,taarifa wanazochapisha huenea kwa kasi na kuwafikia wananchi wengi. Ni muhimu wakahakikisha habari wanazotoa zinajikita katika ukweli, zinahamasisha amani na zinawaelimisha Watanzania kuhusu haki na wajibu wao katika uchaguzi,” amesema Mwambegele.

Ameongeza kuwa mitandao ya kijamii imekuwa chanzo kikuu cha habari kwa jamii ya sasa, hivyo ni muhimu wazalishaji wa maudhui kutumia fursa hiyo kwa ufanisi, bila kupotosha umma au kusababisha taharuki.

"Mitandao ya kijamii ina nguvu kubwa ya kuathiri maamuzi ya watu,tunawasihi muwe sehemu ya kuhimiza amani, mshikamano na ushiriki wa wananchi kwa njia ya kuwapa taarifa sahihi na zenye maadili,” amesisitiza.

INEC imeahidi kuendelea kushirikiana na wazalishaji wa maudhui na vyombo vingine vya habari ili kuhakikisha taarifa zote zinazohusiana na uchaguzi zinatolewa kwa uwazi, uaminifu na kwa kuzingatia misingi ya sheria na maadili ya uandishi.

Mkutano huo umeandaliwa na INEC kama sehemu ya mkakati wa kuhakikisha mchakato wa uchaguzi mkuu unakuwa shirikishi, wa haki na wa amani, kwa kuwajumuisha wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, wanaharakati wa kidijitali, na wanahabari wa mitandao ya kijamii.



Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.