Halmashauri ya Hanang ,SUMAJKT watiliana saini ujenzi wa nyumba za waathirika wa maporomoko ya udongo




      Na Mwandishi wetu ,Manyara

 

HALMASHAURI ya Hanang’ imetiliana saini na Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 108 za waathirika wa maporomoko ya udongo yaliyotokea hivi karibuni Katesh katika wilaya ya Hanang mkoani Manyara.

 

Mkuu wa  mkoa Manyara Queen Sendiga ameshuhudia utiaji saini huo ambapo amesema kutokana na kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na SUMAJKT ana mategemeo makubwa kuwa watejenga  nyumba  zilizo bora na kukamilika kwa wakati.

 

“Tunategemea na kwa uzoefu wao SUMAJKT ambao wao wenyewe wamekiri kwamba nyumba hizi zitajengwa katika mtindo wa oparesheni hivyo zitajengwa kwa muda mfupi ,na hata mimi nakiri kwamba zitamalizika katika muda mfupi na kwa ubora unaotakiwa na watakaopata nyumba hizo wajue kweli wamepata nyumba.”amesema

 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata,  ameeleza kuwa SUMAJKT ipo tayari kutekeleza jukumu ililopewa na serikali na katika muda waliopangiwa kutekeleza na kwamba watakamilisha jukumu hilo wa wakati.

 

Mshauri wa ujenzi huo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Joseph Msangi, amesema kuwa maandalizi ya ujenzi wa nyumba hizo tayari yamekamilika.

 

Amesema SUMAJKT limekuwa likipatiwa miradi ya kimkakati na serikali kutokana na utendaji wa kazi kwa ufanisi, ubora na kumaliza kazi kwa wakati.

 


Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.