Rais Dkt.Samia aamsha shangwe ya wanawake,azungumza nao kwa njia ya simu


         NA JOYCE KASIKI,DODOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamsha shangwe ya wanawake katika ukumbi wa jakaya Kiwete jijini Dodoma baada ya kuzungumza nao kwa njia ya simu huku akiwaahidi kutumia nafasi yake ya kinara wa Nishati safi ya kupikia Afrika kwamba  ameibeba agenda hiyo ili wananchi hususan wanawake waachane na matumizi ya kuni na mkaa.

Akizungumza na wanawake hao kupitia simu ya mkononi ya Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la wanawake la Nishati safi ya kupikia ,Rais Dkt.Samia amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia ni muhimu ili kuokoa vyanzo vya maji na kutunza mazingira.

"Tukiwa tumesherehekea siku yetu jana Mimi Kiongozi wenu nabeba agenda ya nishati safi ya kupikia barani Afrika na mimi ndio champion wake,na niseme tu nimefurahishwa na maandalizi ya Mkutano huu ambao walengwa wake ni wanawake." amesema Rais Dkt. Samia na kuongeza kuwa  

" Ahadi yangu kwa wizara ya Mazingira na wizara ya Nishati nitaibeba hiyo agenda nikisaidiwa na ninyi na kama mnavyojua mwezi wa tano tunakwenda kutafuta fedha za kukuza Nishati safi ya kupikia Afrika, sasa katika Afrika nitaibeba nchi yetu kadiri nitakavyoweza"alisisitiza Dkt. Samia

Ametumia nafasi hiyo kuwaasa wanawake waliohudhuria kongamano hilo kwenda kuwaelimisha wanawake wengine kwenye maeneo yao ili wanawake wengi sasa aanze kutumia Nishati safi ya kupikia. 

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango alisema kukuza Nishati safi ya kupikia ni moja ya agenda za kipaumbele za Taifa huku alisema serikali itaendelea kuongeza rasilimali kuhakikisha agenda hiyo inafanikiwa. 

Amesisitiza ushirikiano wa dhati kati ya Serikali, asasi za kiraia, sekta binafsi na Bunge ili Serikali ifanikiwe kupunguza na hatimaye kuondoa kabisa matumizi ya nishati chafu ya kupikia. 

Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko alisema kuwa sekta ya nishati nchini inachangia kwa kiasi kikubwa kwa maendeleo ya Uchumi wa Nchi na kwamba Nishati safi ya kupikia inachangia takribani asilimia 90 ya nishati yote inayotumika nchini. 

"Matumizi ya kuni ni asilimia 63.5,matumuzi ya mkaa ni asilimia 26.2 na matumizi ya gesi za mitungi ni asilimia 5.1 peke yake wakati matumizi ya umeme yakiwa chini sana kwa asilimia 3."amesema Dkt.Biteko

 Awali  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CCM Taifa(UWT) Mary Chatanda amesema kuwa hatua hiyo ya kuhakikisha wanawake wengi wanatumia Nishati safi ya kupikia pamoa na mambo mengine itasaidia wakina mama  kulinda afya zao kutokana na mgonjwa ya mapafu,kulinda mazingira kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na kuwapatia wanawake muda wa kutosha kufanya kazi za uchumi na kuweza kukua kwa uchumi wa familia.

Chatanda ametumia nafasi hiyo kuiomba Serikali kuona namna ya kupunguza gharama za nishati safi ya kupikia ili wananchi wengi hususan wanawake waweze kumudu gharama .

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.