Serikali yaja na mkakati wa kupima na kupata taarifa za madini nchi nzima

 

WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde

                                  Na Joyce Kasiki,Geita

WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde amesema ,Serikali imedhamiria kufanya utafiti na kupata taarifa za uwepo madini katika maeneo yote nchini ili kiwawezesha wachimbaji wa Madini kufanya kazi hiyo kwa uhakika.

Akizungumza kwenye maonesho ya sita  ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita 2023,Mavunde amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha utafiti huo unakamilika ifikapo 2030 kwa maana ya  ndani ya miaka Saba kutoka hivi sasa .

Amesema hatua hiyo itawezesha wachimbaji kupiga hatua kubwa kwani hawatafanya kazi kwa kubahatisha hivyo mitajo Yao itaendelea kustawi siku hadi siku tofauti na hivi sasa mitajo ya wengi hupotea kwani wanaochimba katika maeneo ambayo hawana uhakika kama madini yanapatikana.

“Nchi yetu ina kilomita za mraba ukizipeleka kwenye ekari ina ukubwa wa eneo ekari milioni 233,sisi tumefanya utafiti wa kina katika eneo la asilimia 16 tu ya eneo la ukubwa wa ekari milioni 233 ,na humo tutatoa maeneo ya makazi,tutatoa maeneo ya mbuga za wanayama na maeneo ambayo hivi sasa shughuli za madini haziruhusiwi kufanyika lakini bado tunabaki na eneo kubwa sana ,

“Sisi kama wizara na timu yangu tumekubaliana kwamba kama asilimia 16 tu ya eneo ambalo limefanyiwa utafiti ndipo eneo ambalo tunakimbizana wote na ndio  linachangia kuingiza fedha za kigeni kwa asilimia 56 ya mauzo yote ya bidhaa nje ya nchi,sekta ya madini inaongoza.”amesema Mavunde na kuongeza kuwa

“Mwaka uliopita tumeuza nje ya ncxhi bidhaa za madini zenye thamani ya dola bilioni 3.3 ,ukizipeleka kwenye madafu ni zaidi ya shilingi trilioni saba  hii ni kwenye pato la Taifa lakini kwenye  mapato ya kodi sekta ya madini inachangia asilimia 15 ya mapato ya kodi ya ndani,mwaka wa fedha uliopita tumechjangia shilingi trilioni 2,na fedha zilizozunguka kwenye masoko yote mwaka wa fedha uliopita ni sh trilioni 1.6 sasa tukajiuliza hivi tukiongeza eneo kubwa kufanya utafiti hii nchi itakuwa wapi .”

Aidha Mavunde amesema,utafiti huo utawezesha kuonesha maeneo yenye Maji,malighafi za utengenezaji wa mbolea na vitu vingine vingi ambavyo vyote kwa pamoja vileta ustawi nchini.

"Tukifanya utafiti tutakuwa nanuwezo wa kubaini miamba yenye Maji ambayo Serikali kupitia wizara ya maji itachimba visima na wananchi wengi watapata Maji na maisha ya watanzania yataboreka,

"Lakini pia kupitia Maji hayo tutaweza kuchimba mabwawa na wakulima watafanya kilimo Cha umwagiliaji na hivyo kulima mara mbili kwa mwaka na hivyo kuleta usalama wa chakula nchini “amesema

Vile vile Mavunde amesema utafiti huo itawesha kuonesha malighafi za kutengeneza mbolea bidhaa ambayo Serikali hitumiabfedha nyingi kiagiza tan 350,000 kwa mwaka ,kwa hiyo upatikanaji wa malighafi hiyo utashawishi wawekezaji wa Viwanda vikubwa vya mbolea nchini .

"Kwa hiyo hayo yote yatafanikiwa kwa upimaji ndiyoaana tunasema madini ni maisha yetu ,madini ni maisha na utajiri."amesema na kuongeza kuwa

"Nataka niwahahkikishie ,Serikali tumejipanga Ili wananchi mliopo kwenye tasnia ya uchimbaji muingie kwenye utajiri wenu."amesisitiza Mavunde

Share:

Mavunde aipongeza GF Trucks kurahisisha shughuli za uchimbaji

 




                                          Na Joyce Kasiki ,Geita

WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde ameishukuru Kampuni ya GF Trucks&Equipment inayojishughulisha na uuzaji wa magari,mashine na mitambo kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za uchimbaji Madini kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na sekta ya madini hasa wachimbaji katika kuwapatia vifaa katika mfumo ambao utawezesha wachimbaji wengi kumiliki vifaa vitakavyosaidia katika shughuli za uchimbaji.

Akizungumza katika uzinduzi wa Ofisi ya GF Truck mkoani Geita,Mavunde amewaomba waendelee kutanua wigo na kuwezesha wachambiji wengi zaidi kupata vifaa hivyo ambavyo vitaleta tija kubwa katika Taifa.

“Na sisi kama Wizara ,kwa kuwa tunao mkakati wa kuhakikisha kwamba tunaongeza shuguli za uzalishaji wa madini hapa nchini wa kuongeza wigo mpana zaidi wa madini ya aina mbalimbali kwa tafiti ambazo tutakwenda kuzifanya .”amesema Mavunde

Aidha ametumia nafasi  hiyo kutoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini nchini (STAMICO) kusimamia makubaliano waliyoingia baina yao na GF Truck ya kuwasaidia wachimbaji wadogo ili waweze kunufaika na mpango mzuri wa GF Trucks  wa kupata magari,mitambo na mashine kwa ajili ya shughuli zao za uchimbaji.

“Mpango mliokuja nao ni mzuri mkitekeleza katika maeneo machache mliyokuja nayo itasaidia kurahisisha shughuli za uchimbaji.”amesema Mavunde

Awali Mkurugenzi Biashara GF Trucks &equipment Salman Kalman amewakaribisha wadau mbalimbali wakiwemo wachimbaji wa madini kupata huduma katika Ofisi zilizopo mkoani Geita.

Ametumia nafsi hiyo kumpongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo yanakwenda kuleta tija kwa wachimbaji,wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Magari tuliyonayo ambayo baadhi tunawakabidhi wateja wetu ni  matunda mazuri ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hasaan kwa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji ambapo hivi sasa tunajivunia kuwa kiwanda chetu kilichopo Kibaha mkoa wa Pwani ambacho ni kiwanda pekee hapa nchini kuunganisha magari ,

“Na Mwaka huu kiwanda chao kitaunganisha magari zaidi ya 1500 mwaka huu tulianza kufanya upanuzi wa kiwanda chetu kwa lengo la kuanza kuunganisha magari madogo .”


Share:

Nguvu Moja Secury inavyojali afya za wafanyakazi wake

Meneja Nguvu Moja Security Caroine Mushi

 
Mmoja wa wafanyaazi wa Nguvu Moja Security Jacob Zacharia

                   Na Joyce Kasiki,Geita

KAMPUNI ya Uinzi ya  Nguvu Moja ( Nguvu Moja Security service)  imesema,moja ya jambo muhimu inaloiangalia kwa wafanyakazi ni pamoja na afya zao na Mazingira wanayoishi pamoja na magonjwa.

Hayo yamebainishwa  Meneja wa Kampuni hiyo Caroine Mushi ambapo amesema,kampuni imeuwa na desturi ya  kuwapima afya wafanyakazi wake kabla ya kuingia kazini, na Mwaka mmoja akiwa kazini na hata akimaliza mkataba wake.

" Tunapoajiri wafanyakazi wetu, kitu cha kwanza sisi hatutaki mfanyakazi anayeugua ugua kazini, kwahiyo tunampima kabla hajaingia kazini, pia tutampima afya yake baada ya Mwaka mmoja akiwa kazini, vile vile ikitokea mfanyakazi akasema hawezi kuendelea na kazi na Nguvu Moja Security services au mkataba umekwisha, au amesema ameenda kusoma, pia tutampima afya yake,

“Tunampima kwa sababu gani  tunataka tuhakikishe  mfanyakazi tulivyompokea ana afya bora, anaweza kufanya kazi, na anapotoka ndani ya security services kule anapoelekea anakua na afya yake ile ile kwasababu kumetokea magonjwa mbalimbali, kunatokea taadhari mbalimbali ambazo mtu hawezi kujua je hizi nimeipata nikiwa kazini au nilipata nikiwa napitapita katika miangaiko yangu ya kila siku" amesema Mushi

Amesema kitu kingine wanachoangalia kwa wafanyakazi wake ni Mazingira, Mazingira wanayofanyia kazi yawe safi, wanaoangalia uvaaji wake, chakula chake anachotumia kila siku hili tunazingatia sana.

Aidha amesema katika masuala ya kazi wamekua wakilinda sana  afya ya wafanyakazi wao, hivyo wamejikita zaidi katika kuwapatia vifaa Bora vya eneo lao la kazi na kuwapatia elimu sahihi ya jinsi ya kutumia vifaa hivyo ikiwa ni sambamba na kuhakikisha wanavilinda vifaa hivyo ili vibaki katika hali nzuri.

Naye mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Nguvu Moja Security services Jacob  Zacharia, ( Contract Meneja ) amesema cha kwanza wanahakikisha wanawapata Vijana ambao ni waadirifu, mazuri na waaminifu kutoka huko wanakotokea katika makazi ya kawaida.

" Kabla ya kuwaajiri wanahakikisha wanawafanyia vipimo vya uhakika baada ya kujilidhisha  kwa wale waliotuma maombi  baada ya kujilidhisha nao wanakwenda katika hatua ya pili ni kuwaajiri  Vijana wenye sifa waliopitia JKT na waliopitia mgambo" amesema Zacharia.

" Lakini pia kwakua hii ni kampumi ya kizalendo ya kitanzania haibagui watu wote, tunaajiri hata watu ambao ni  raia wa kawaida ni wale ambao wanaatuma ya kutosha, waaminifu ambao pia wanaweza kunisaidia Kampuni hii kuweza kusonga mbele.

Aidha amefafanua kuwa Kampuni hiyo inaanza kuajiri kuanzia daasa la sana, kidato cha nne, kidato cha sita, diploma digrii na kuendelea kulingana na uhitaji na utaalam unaotakiwa.

Amesema Kampuni ya Nguvu Moja Security services haina ubaguzi kwenye kuajiri, kila mwenye sifa na kila ambaye anastahili basi atapata ajira katika Kampuni hii ya Nguvu Moja.

Hata hivyo Operation  Meneja Desideri Stevin  amesema Kampuni hiyo imejikita kwenye maeneo la migodi ambayo wanatoa aina tofauti tofauti za huduma za kiaskari ambayo wanatoa.

Share:

Wachimbaji wazawa wamshukuru Rais Samia


 

 


 

 


            Na Joyce Kasiki,Geita                                                              

KAMPUNI ya FEMA Mining and Drilling  LTD inayojihusisha na  uchimbaji,uchongaji na ulipuaji wa madini nchini iliyopo Munekeze-Katoro Mkoani Geita wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Hassan Suluhu kwa kuwapa fursa kampuni za kizawa kufanya kazi katika migodi iliyopo nchini.

Hayo yamesemwa na Mratibu mradi kutoka Kampuni hiyo Mhandisi Jacquline Mtei waati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya sita ya kimataifa ya Teknolojia ya Madini  yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita.

Amesema, kwa sasa milango ya kufanya kazi wazawa na kupewa kazi mbalimbali hasa kwenye sekta ya madini ni dhahiri kuwa sekta hiyo inazidi kukua siku hadi siku.

 " Napenda kumshukuru Rais  Dkt Samia Hassan Suluhu kwa kuweza kutengeneza Mazingira ya uwezekano wa wazawa 'makampuni mama' kuweza kufanya kazi katika migodi yetu hii ya kati pamoja na Migodi  mikubwa,Kupitia kampuni  yetu ya FEMA sisi ni kampuni zawa kampuni ya kitanzania  kwa hiyo tumeona mama alivyotengeneza mazingira ambayo imetuwezesha kapata zabuni katika migodi ya kati na mikubwa" Amesema Jacquline

Amesema Sekta ya madini inaoongoza kwakuchangia uchumi wa nchi hivyo inapotokea milango inapofunguliwa kwa wazawa kufanya kazi katika migodi hii pia itasaidia kukua zaidi kwani watatanguliza uzalendo katika nchi yao.

Aidha amewaaalika wanawake kusoma masomo ya sayansi hasa kuhusu miamba na madini kuwa wasiogope kazi zipo pia waondoe dhana potofu kuwa kazi zinazohusu madini ni wanaume pekee.

"Fursa za  ajira kwa  wanawake katika sekta ya madini zipo sisi  kampuni yetu imeweza kutusaidia sisi wanawake kupata  ajira zaidi ya wanawake kumi na tano wamepata ajira nikiwemo mimi kwa hiyo wanawake wenzangu msiogope tuje huku"amewahasisha Jacquline

Kwa upande wake Afisa manunuzi na usambazaji kutoka FEMA Mining and  Drilling  LTD Frank Joseph amesema hao kama FEMA wameweza kushirikiana na makampuni tano tofauti  katika kuwapa  zabuni katika kampuni yao kama vile usambazaji wa vipuri,mafuta na virainisha kwa ajili ya mashine zao  pia pamoja na  huduma zingine ikiwemo  usafi,chakula na huduma nyingine za kijamii.

Aidha ameongeza pia katika katika kurudisha shukrani kwa jamiii kwa kile wanachokipata pia wameweza kusaidia kununua madawa katika zahati zinazo zunguka mgodi sanjari na kujenga shule na kukarabati vyumba vya madarasa ikiwemo kuzalisha ajira kwa vijana zaidi ya miamoja wanaozunguka mgodi.

Share:

NIC yawaasa Wachimbaji wa Madini kukata Bima

 



Matukio katika picha ni wageni mbaimbai waliofika katika banda la NIC katika maonesho ya Madini Mkoani Geita katika Hamashauri ya mji wa Geita


                  Na Joyce Kasiki,Geita 

WACHIMBAJI  wa madini nchini wameaswa  kukatia Bima mitambo wanayotumia katika shughuli zao za uchimbaji ili pale inapotokea imeharibika ili waweze kutengenezewa bila kuathiri shughuli zao za uchimbaji.

Akizungumza katika maonesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili halimashauri ya mji  wa Geita,Meneja wa Shirika la Bima  (NIC) kanda ya ziwa Stella Marwa amesema kuwa bado hakuna muamko kwa wachimbaji wa Madini kukata Bima.

“Kwa hiyo kutokana na muamko  mdogo kwa wachimbaji kukata Bima,tumeona tushiriki maonesho haya ili tuweze kutoa elimu ya Bima kwa wachimbaji na wananchi wote ili waweze kukata bima kwa ajli ya kujihakikishia usalama wao.”amesema na kuongeza kuwa

“Kwa mfano kuna  bima ya ajali ambayo humsaidia mchimbaji pale ambapo anaweza kupata madhara katika shughuli zake za uchimbaji hivyo  NIC kupitia bima yake ya ajali kwa ajili ya wachimbaji itaweza kumrudisha katika hali yake ya kawaida na endapo itatokea bahati mbaya amefariki warithi wake wanaweza kufidiwa na kuendeleza shughuli zao zakiuchumi.”

Ameongeza kuwa mbali kutoa bima elimu ya bima hizo pia wanatoa elimu ya bima ya maisha ambayo ina uwekezaji ndani na ulinzi ndani ambayo inamhakikishia mchimbaji au mtu mwingine yeyote kuwa ukipatwa na janga lolote lile familia ikiwemo watoto wataendelea kusoma.

"Pia katika maonesho haya tumekuja kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto kama magari,pikipiki na bajaji  tunatoa elimu hii ili hao wasafirishaji waweze kukata bima hizo na kuepusha ajali ambazo zinaweza kuwatokea ikapelekea hayo magari yao kutokutengenezeka kabisa sababu yakutokuwa na bima wakikata bima na NIC Insurrance tutawalipa ndani ya siku saba na taratibu zote tunafanya kulingana na miongozo na zakumkatia ndiyo maana tunalipa ndani ya siku saba"amesema Marwa.

 Aidha ameongeza kuwa NIC wameweza kufanya mabadiliko makubwa  kwa  kipindi kifupi ambapo wanatembea kifua mbele kuwa wana uwezo wakulipa madai ndani ya siku saba.

 Aidha ametoa wito kwa wakazi wa Geita katika kipindi hiki cha maonesho kutembelea banda hilo kupata elimu mbalimbali kuhusu bima.

Share:

NSSF yajivunia kuongeza thamani ya Mfuko

 

MKURUGENZI Mkuu wa NSSF (aliyeshia kipaza sauti) akizungumza mbele ya Naibu Waziri Mkuu Dkt.Dotto Biteko alipofika wenye banda la Mfuko huo katika maonesho ya Madini Halmashauri ya mji wa Geita mkoani Geita



                 Na Joyce Kasiki,Geita

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)  Masha Mshomba amesema ,katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  wameweza kuongeza thamani ya Mfuko huo kutoka Trilioni 4.8 Hadi kufikia shilingi Trilioni 7.6 kwa hesabu zinazoendelea kukaguliwa Hadi hivi sasa.
Mkurugenzi huyo ameyasema hayo mbele ya  Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Biteko  alipotembelea Banda hilo ambapo aliipongeza NSSF kwa hatua hiyo.
Masha amesema kuongeza thamani ya Mfuko Hadi kufikia kiasi Cha shilingi Trilioni 7.6 ni hatua kubwa .
"Thamani ya Mfuko imeendelea kukua  kwa kasi tukizungumzia mahesabu yaliyokaguliwa  hadi mwaka jana Juni,tulikuwa na mahesabu ya shilingi trilioni 6.08,lakini kwa mwaka  huu mpaka kufikia mwezi Juni mwaka huu hesabu ambazo bado zinaendeea kukaguliwa thamani ya Mfuko ni shiingi triioni  7.6"amesema na kuongeza kuwa
“Ni ukuaji mkubwa sana hasa ukizingatia kwamba kabla Rais Samia hajaingia madarakani thamani ya mfuko ilikuwa ni shiingi triioni 4.8 tu."
Akizungumza kuhusu uwepo wao katika maonesho ya Madini amesema wapo kwa sababu ya kuelimisha wadau na wananchi kwa ujumla ilinwaweze kujiunga na Mfuko huo Ili kuendelea kuongeza wananchi na thamani ya Mfuko.
"Katika maonesho hayo tumekuwa na mafanikio makubwa ,tumeongeza wachangiaji wa NSSF ambapo kwa mkoa wa Geita tunakusanya michango ya shilingi bilioni  96 ,lakini wakati   Rais Samia anaingia madarakani kwa mkoa huu tulikuwa tunapokea michango ya shilingi  bilioni  26 tu,tunaamini tutaendelea kufanya vizuri zaidi katika miaka ijayo."amesema na kuongeza kuwa
Aidha amesema .Mfuko kwa ujumla tumeuwa pia na 'perfomance' nzuri sana ambapo mwaka  unaoishia Juni  2023  thamani ya  michango ilikuwa shilingi Trilioni  1.66 na shilingi Trilioni 1.48  kwa mwaka ulioishia Juni 2022

Share:

Dkt.Biteko aipongeza BoT kutunza akiba ya fedha za kigeni






                 Na Joyce Kasiki,Geita

NAIBU Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania BoT  kwa kununua dhahabu kwa ajili ya kutunza akiba za nchi badala ya kutunza kama fedha huku akisema ni  ndoto ambayo Serikali ilikuwa inaitamani   kwa muda mrefu.

Aidha ametoa wito kwa BOT kushirikiana kwa karibu na Wizara ya madini pamoja na taasisi zake ili waweze kumfikia kila mchimbaji kwa sababu   kuna watu ambao hao wanaleta  pesa wanakusanyiwa wanapelekewa dhahabu  .

Akizungumza mkoani Geita katika maonesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini Mkoani Geita alipotembelea katika Banda hilo  amesema kuwa kwa sasa nchi inahitaji  fedha za kigeni kwa ajili ya manunuzi  ambapo kwa upande wa dolla imekuwa changamoto kwa kila nchi duniani hivyo lazima zitumike rasimali za nchi katika kupata dolla na hawawezi kuipata bila kutumia dhahabu.

"Nia yetu ni kuona kwamba eneo linalotupatia  fedha za kigeni kwa wingi bado itabaki  kuwa sekta ya madini   na sekta ya madini ikileta dolla kwa wingi hizo stress nyingine mnazoziona kama mafuta madawa na bidhaa zote tunazo ziagiza kutoka nje  kwakutumia dolla tutaweza kuzipata ili tuhudumie watanzania kwa hiyo hongereni sana kwa hatua hiyo"amesema Biteko ma kuongeza kuwa

"Ni imani yangu   baada ya miaka kadhaa na sisi  kama nchi tuseme tuna akiba ya dhahabu tani kadhaaa kama ilivyo nchi nyingine kubwa na kuwapongeza wafanyazi wa BOT kwa hatua waliochukua ya ununuzi wa dhahabu."

Kwa upande wake Meneja Msaidizi Kurugenzi ya Masoko ya Fedha BOT,Dkt Anna Lyimo amesema kuwa mbali kununua dhahabu bado wanaangalia namna ya kuwasaidia wachimbaji wadogo na wa kati kutokana na changamoto zinazowakabili .

Ametaja baadhi ya changamoto hizo ni  mitaji ,elimu na teknolojia huku akisema wameamua  kushirikiana na   STAMICO  ambao  itasimamia wachimbaji hao kuungana kupitia vikundi ambapo BOT itawezesha kupata mikopo na kuondokana uchimbaji mdogo na kuinuka zaidi katika uchumi wao binafsi  na hivyo kuchangia katika uchumi wa Nchi.

Aidha amesema katika maonesho hayo ya madini BoT wanatoa  elimu kuhusu sheria ya fedha za kigeni ya mwaka 2022 ambapo inataka matumizi na  mapato yote yanayopatikana katika mauzo ya nje ya nchi basi yaweze kurudishwa nchini ndani ya siku tisini huku akisema mapato hayo  na hivyo  kuongeza akiba za fedha za kigeni.

Ametumia nafasi hiyo kuishukuru serikali ya awamu ya sita chini yanuongozi thabiti wa Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kushirikiana bega kwa bega na BoT na hivyo kutekeleza majukumu yake

Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.