Meneja Nguvu Moja Security Caroine Mushi |
Mmoja wa wafanyaazi wa Nguvu Moja Security Jacob Zacharia |
Na Joyce Kasiki,Geita
KAMPUNI ya Uinzi ya Nguvu Moja ( Nguvu Moja Security service) imesema,moja ya jambo muhimu inaloiangalia kwa wafanyakazi ni pamoja na afya zao na Mazingira wanayoishi pamoja na magonjwa.
Hayo yamebainishwa Meneja wa Kampuni hiyo Caroine Mushi ambapo amesema,kampuni imeuwa na desturi ya kuwapima afya wafanyakazi wake kabla ya kuingia kazini, na Mwaka mmoja akiwa kazini na hata akimaliza mkataba wake.
" Tunapoajiri wafanyakazi wetu, kitu cha kwanza sisi hatutaki mfanyakazi anayeugua ugua kazini, kwahiyo tunampima kabla hajaingia kazini, pia tutampima afya yake baada ya Mwaka mmoja akiwa kazini, vile vile ikitokea mfanyakazi akasema hawezi kuendelea na kazi na Nguvu Moja Security services au mkataba umekwisha, au amesema ameenda kusoma, pia tutampima afya yake,
“Tunampima kwa sababu gani tunataka tuhakikishe mfanyakazi tulivyompokea ana afya bora, anaweza kufanya kazi, na anapotoka ndani ya security services kule anapoelekea anakua na afya yake ile ile kwasababu kumetokea magonjwa mbalimbali, kunatokea taadhari mbalimbali ambazo mtu hawezi kujua je hizi nimeipata nikiwa kazini au nilipata nikiwa napitapita katika miangaiko yangu ya kila siku" amesema Mushi
Amesema kitu kingine wanachoangalia kwa wafanyakazi wake ni Mazingira, Mazingira wanayofanyia kazi yawe safi, wanaoangalia uvaaji wake, chakula chake anachotumia kila siku hili tunazingatia sana.
Aidha amesema katika masuala ya kazi wamekua wakilinda sana afya ya wafanyakazi wao, hivyo wamejikita zaidi katika kuwapatia vifaa Bora vya eneo lao la kazi na kuwapatia elimu sahihi ya jinsi ya kutumia vifaa hivyo ikiwa ni sambamba na kuhakikisha wanavilinda vifaa hivyo ili vibaki katika hali nzuri.
Naye mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Nguvu Moja Security services Jacob Zacharia, ( Contract Meneja ) amesema cha kwanza wanahakikisha wanawapata Vijana ambao ni waadirifu, mazuri na waaminifu kutoka huko wanakotokea katika makazi ya kawaida.
" Kabla ya kuwaajiri wanahakikisha wanawafanyia vipimo vya uhakika baada ya kujilidhisha kwa wale waliotuma maombi baada ya kujilidhisha nao wanakwenda katika hatua ya pili ni kuwaajiri Vijana wenye sifa waliopitia JKT na waliopitia mgambo" amesema Zacharia.
" Lakini pia kwakua hii ni kampumi ya kizalendo ya kitanzania haibagui watu wote, tunaajiri hata watu ambao ni raia wa kawaida ni wale ambao wanaatuma ya kutosha, waaminifu ambao pia wanaweza kunisaidia Kampuni hii kuweza kusonga mbele.
Aidha amefafanua kuwa Kampuni hiyo inaanza kuajiri kuanzia daasa la sana, kidato cha nne, kidato cha sita, diploma digrii na kuendelea kulingana na uhitaji na utaalam unaotakiwa.
Amesema Kampuni ya Nguvu Moja Security services haina ubaguzi kwenye kuajiri, kila mwenye sifa na kila ambaye anastahili basi atapata ajira katika Kampuni hii ya Nguvu Moja.
Hata hivyo Operation Meneja Desideri Stevin amesema Kampuni hiyo imejikita kwenye maeneo la migodi ambayo wanatoa aina tofauti tofauti za huduma za kiaskari ambayo wanatoa.
No comments:
Post a Comment