PICHA zote zinaonyesha miti ya aina mbaimbai iwiemo ya matunda inayouzwa na Ruthberta |
Na Joyce Kasiki, Geita
MKURUGENZI wa Kampuni ya Ruthberta Supply inayojishughulisha na uzalishaji na uuzaji wa miche ya aina mbalimbali ikiwemo ya matunda Ruthberth Myonga amewaasa watanzania kila mmoja kwa nafasi yake kushiriki kikamilifu katika upandaji miti Ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Hayo yamesemwa leo Septemba 22 Mwaka huu Mkoani Geita na
Mkurugenzi wa Ruthberth ,Ruthberth Myonga kwenye Maonyesho ya 6 ya
Teknolojia Madini yanayofanyika katika Viwanja vya Bombambili .ambapo pia
amewahamasisha wanawake kote nchini kupanda miti mbalimbali ya matunda na
kivuli Kwa lengo la kudhibiti mabadiliko ya tabia ya nchi.
"Kupanda miti kuna umuhimu kumbwa sana ingawa siyo Kila mtu ni wa kupanda,hii inawezesha kusaidia Kuzuia majanga mbalimbali ,Kuna aina ya miti kama miharadani kama unataka kupanda miti hii usichukie popo angalia una faida gani kwa miaka 200 ijayo."amesema Myonga
Amesema kwa kutumia maonyesho hayo amekuja na miti ya matunda katika mkoa wa Geita kutokana na mkoa huo kukata mingi kwa ajili ya shughuli za uchimbaji huku akisema miti hiyo itasaidia katika kuboresha Afya zao lakini pia kurudisha uoto wa asili.
Ametumia nafasi hiyo kuwaasa watanzania kufuatilia vyombo vya habari Ili waweze kujifunza vitu mbalimbali katika maonyesho hayo ikiwemo shughuli za utunzaji mazingira.
Aidha amesema mbali na kupanda miti ya matunda pia amewaasa wajikite katika kupanda miti ya maua ambayo pia ni fursa katika kujikwamua kiuchumi.
" Ruthberta Kampuni tupo katika Maonyesho haya lengo kubwa nikuja kuwahamasisha Watanzania juu ya umuhimu wa kupanda miti na kutunza na ikimbukwe kuwa hivi Sasa Kuna changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabia ya nchi hivyo ni muhimu Kwa kila Mtanzania kupanda na kutunza Mazingira kwenye maeneo yanayowazunguka"amesema na kuongeza kuwa
"Hivi sasa katika mikoa ya Kanda ya ziwa ikiwemo Mkoa huu wa Geita kumekuwa na mwamko mkubwa wa watu kupanda miti ya matunda na hata hapa mmeona watu mbalimbali wanakuja kuuliza na kununua miti kwani wamejua umuhimu wa kupanda miti ."
Myonga ametumia nafasi hiyo kuishukuru serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mazingira kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau ikiwa pamoja na kutoa matamko mbalimbali yanayohamasisha upandaji wa miti .
"Kupitia Kampuni ya Ruthberta tutahakikisha tunaongeza kasi ya kuelimisha Watanzania pamoja na kuzalisha miti Kwa wingi ili kila Mwananchi apande miti Ili kufikia malengo yaliyowekwa hasa katika suala Zima la utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ."amesema Myonga
Ameihakikishia Serikali na wananchi kwanunumla kuwa Kampuni hiyo kwa
kushirikiana na Serikali na wadau wengine wa mazingira ,itafuatilia ili kupata
taarifa mbalimbali zinazohusu utunzaji wa mazingira kwa lengo la
kupungaza kasi ya ukataji miti kitendo ambacho ni chanzo cha uharibifu wa
mazingira.
Aidha amewahimiza wananchi kufika katika maonyesho hayo na kutembelea katika Banda lake Ili wajionee na kununua miti ya matunda ambayo ni muda mfupi sana ukiwemo mti wa ukwaju wenye ladha kama ya tende lakini pia ni mtidawa unaosaidia katika uboreshaji Afya za wananchi.
Wakati huohuo Mkurugenzi huyo ametoa rai kwa wadau mbalimbali ambao
wanaomba fedha Kwa ajili ya Mazingira kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwenye
eneo lililokusudiwa na si kufanya ujanjaujanja kwani kufanya hivyo nikurudisha
nyuma harakati za Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
ambayo inahamasisha uutuzaji wa Mazingira,kupanda miti katika maeneo mbalimbali
nchini.
Mur |
No comments:
Post a Comment