Maonyesho ya Madini na Uwekezaji yafungua fursa

 

MENEJA wa Kampuni ya Uchimbaji Madini Elianje Genesis 

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Elianje Genesis wakiwa kazini



Na Joyce Kasiki,Ruangwa

Meneja wa Kampuni ya Elianje Genesis Philbert  Massawe ameipongeza Serikali kupitia.mkoa wa Lindi kwa kuandaa maonyesho ya madini na Uwekezaji ambayo yamefungua fursa ya wachimbaji kujulikana hasa kwa wawekezaji wazawa lakini pia na kwa wawekezaji  wageni

 Massawe  ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari waliotembelea mgodini hapo kuona namna mgodi huo unavyoendesha shughuli zake za uzalishaji.madini hasa ya dhahabu.

Pia ametaja madini mengine yanayozalishwa katika Kampuni ya Elianje kuwa ni pamoja na  Graphite, Nikei, Chuma, Green Garnet, Dhahabu, na Copper

Amesema,mara baada ya maonyesho hayo yaliyofanyika hivi karibuni mkoani humo kumalizika ,wadau wameanza kuweka oda za kuzalishiwa madini

"Napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuandaa maonyesho ya Madini na Uwekezaji,kwetu Elianje imekuwa ni fursa kubwa,maana mara TU baada ya maonyesho kumalizika,tumeanza kupokea oda za wadau tofauti na ilivyokuwa mwanzo,hii inaonyesha.mooa wa Lindi sasa umefahamika kwamba nao una madini."amesema Massawe

Hata hivyo,mbali na kuipongeza Serikali Massawe amezungumzia changamoto zinazoikabili Kampuni hiyo ni ya nishati ya umeme huku akiomba Serikali iliabgalie suala Hilo na kulifanyia kazi.

Amesema,changamoto hiyo i.ekuwa ikisababosha uzalishaji kuwa chini huku akisema upatikanaji wa umeme wa uhakika utaongeza tija hasa katika kipindi hiki ambacho wadau wanajitoleza kununua madini katika mkoa wa Lindi.

"Ukosefu ama upatikanaji wa umeme usio wa uhakika itazoroyesha na kurudisha nyima ufanisi katika uzalishajiadini na kushindwa kufikia mahitaji ya wateja wetu ambao tunaamini wataendelea kuongezeka,

"Sasa kama wataongezeka na tukashindwa kuzalisha tutakuwa hatujayatendea haki maonyesho ya madini na Uwekezaji ambayo lengo lake lilikuwa ni kuutambulisha mkoa wa Lindi kwamba nao una madini ya kutosha na hivyo kualika wadau kuja kununua madini."amesema Massaw

Akizungumza kuhusu malengo ya Kampuni hiyo Massawe amesema ni kutoka kwenye uchimbaji mdogo Hadi kwenye uchimbaji mkubwa kwa maslahi yao binafsi na maslahi.mapana ya Jamii na Taifa kwa ujumla.

 "Kampuni yetu kwa.sasa Ina leseni ya uchimbaji mdogo,lakini lengo letu ni kutoka hapa tulipo na kupata leseni kubwa ya uchimbaji  , hivyo tuko kwenye mchakato huo ambao lazima tutaongeza ukubwa wa leseni ambayo itatuwezesha  kukuza kile ambacho tunakipata, lakini pia oda tulipopokea tutaenda kuongeza Maendeleo ambayo tulikua nayo, Ina maana tutatoka kwenye hatua Moja ya uzalishaji na kwenda kwenye hatua nyingine.

Akiongelua katika suala la kukabiliana na ajira,, Massawe amesema Kampuni ya Elianje Genesis Kampani Limited imefanikiwa kuajiri zaidi ya wafanyakazi wapatao 200 wengi wao wakiwa ni Vijana kutoka Mtwara na Lindi.

Kuhusu suala la ajira  kwa Vijana hasa katika maeneo yanayozunguka Mgodi huo ,Massawe amesema  Kampuni imefanikiwa kijaiti wafanyakazi wapatao 200 Hadi sasa kutoka wafanyakazi 10 waliokiwa wameajiriwa 2016 wakati mgodi unaanza.

" Kupitia jitihada zetu, tumeajiri zaidi ya wafanyakazi wapatao 200 ambao wanapata huduma zote za msingi Kwa maana ya Bima ya afya kutoka NHIF na pia wanachangia mfuko wa hifadhi za jamii ( NSSF) hii ni Kwa waliokidhi vigezo, hawa  wote wamechangia Kwa kiasi kikubwa katika kuleta Maendeleo kwa eneo hili na hatimaye kuinua uchumi wa watu katika kata wanazotokea" amesema Meneja Massawe

" Tunaelewa umuhimu wa kuwekeza katika jamii yaani rasilimali watu,nanndio maana tumewajengea uwezo wafanyakazi wetu ili waweze kufanya kwa ufanisi na katika Mazingira ya usalama mkubwa" ameongeza Massawe

Kuhusu huduma za kijamii amesema, kampumi ya Elianje Genesis imeweza kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuunganisha miundombinu nya barabarani za Vijiji na Vijiji, kujenga madarasa katika shule zinazozunguka Mgodi pamoja na  kuchimba kisima cha maji kwa jamii.


Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.