Banda la Mfuko wa Higfadhi ya Jamii NSSF ambao ni moja kati ya wadhanmini wa Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Madini |
Moja ya Banda la wadau wa madini ambao wameshiriki katika maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Madini katika viwanja vya EPZA kata ya Bombabili Halmashauri ya Mji wa Geita. |
NA JOYCE
KASIKI,GEITA
NAIBU Waziri
Mkuu ambaye pi ni Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika ufunguzi wa maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Madini mkoani Geita yatakayofunguliwa rasmi Septemba
23 mwaka huu katika Halmashauri ya Mji wa Geita huku Rais Dkt.Samia Suluhu
Hassan akitarajiwa kufunga maonyesho hayo.
Akizungumza leo
Septemba 21,2023 na waandishi wa habari katika viwanja vya EPZA vilivyopo katika
Kata ya Bombambili Halmashauri ya Mji wa Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin
Shigela amesema,maonyesho hayo ambayo tayari yameshanza jana ,mwaka huu
yamekuwa na mwitikio mkubwa kutoka na washiriki wengi Zaidi kujitokeza
kuonyesha shughuli wanazozifanya.
“ Maonyesho haya
yalianza 2018 na mwaka huu ni maonyesho ya sita ya madini ambapo dhamira ni
kuhakikisha kwamba wananchi wanapata maarifa mapya watakayoyatumia katika
shughuli za utafiti,kuongeza thamani na shughuli za uchenjuaji,
“Mwaka jana tulikuwa
na washiriki 250 ,lakini mwaka huu
washiriki walioingia mpaka sasa ni zaidi ya 400 maana yake mwitikio ni mkubwa
na wananchi hasa wachimbaji wameelewa maana ya uchimbaji hususan makampuni
yanayojihusisha na uchimbaji,uchenjuaji ,uongezaji thamani kwa maana kwamba wameona
umuhimu wa kushiriki katika maonyesho haya.”amesema Shigela
Aidha
amesema,Mkoa umeweka mazingira mazuri ili kuwawezesha wadau wa sekta ya madini
kuja na teknlojia mpya na rahisi zitakazowawezesha wachimbaji wadogo kufaidika
na teknolojia hizo kwa kuwa na gharama ndogo za uchjimbaji ,uchenjuaji na
uongezaji thamani wa madini ili nchi ifikie hatua ya kuhifadhi dhahabu ambayo
imeongezwa thamani kwa zaidi ya asilimia 100.
Mkuu wa Mkoa
ametuamia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi hasa wanaojishughulisha na uchimbaji,uongezaji
thamani na uchenjuaji wa madini kufika katika viwanja hivyo kujifunza na
kujionesha mitambo na mshine kwa ajili ya shughuli za uchimbaji.
No comments:
Post a Comment