PICHANI ni Katibu Mkuu wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Fatma Rajab akizungumza na wanawake wachimbaji madini kwenye maonyesho ya madini mkoani Geita |
NA JOYCE KASIKI,GEITA
KATIBU Mkuu,Wizara ya
Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo wa Zanzibar Fatma Hamad Rajab
amewaasa Wanawake wachimbaji kusambaza elimu ya uchimbaji kwa vijana hususan wa
kike ili waweze kujitegemea na kumudu mahitaji katika familia.
Rajab ameyasema hayo alipotembeea
katika banda la Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake (TAWOMA) katika
maonesho ya Madini yanayoendeea katika viwanja vya Bombambii katika mji wa
Geita mkoani Geita.
“Changamoto mnazokutana
nazo katika shughuli zenu mnapaswa mzichukulie kama fursa ,lakini pia
muendelee kutoa taaluma hasa kwa vijana wa kike kwa sababu wao ndiyo
wahitaji zaidi ili mwisho wa siku waweze kupambana wenyewe kuhudumia
familia badala ya kuwategemea wanaume,
“Mjitahidi kuonyesha ujasiri,
kupambana na kuonyesha wanawake tunaweza bila kumtegemea mwanaume,tufuate mfano
mzuri wa Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye anaonyesha kwa vitendo
kwamba wanawake tunaweza ,na atakayebisha hilo huyo atakuwa ana chuki zake
binafsi.”amesisitiza Rajab
Awali Katibu wa TAWOMA Salma
Ernest ameelezea mafanikio ya chama hicho katia kipindi cha miaka miwili ya
Rais Samia huku akisema,chama kimeweza kufanya programu mbalimbali za
kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya Madini.
Amesema,chama hicho kina
wanachama mikoa 21 ya Tanzania na wanatarajia kuongeza mikoa mingine
lakini pia wapo katika wilaya 41 na wana matawi au programu ya vijana
ambao mpaka sasa wana vikundi 14 vya vijana ambao wamejiajiri kwa kutengeneza
vitu mbalimbali kwa kutumia madini yenye ubora wa chini ambayo hayana soko.
Aidha amesema,chama hicho
kinaendesha vikundi 34 vya kusaidia jamii ambapo 17 vipo
Tanga na 12 kutoka Morogoro vijijini ambavyo hukopeshana na hivyo kumudu
kusaidia familia .
Katika hatua nyingine amesema
chama hicho kinatimiza miaka 25 ya chama chao na wamekuja na programu iitwayo
Malkia wa Madini ambapo wameandaa programu migodini pamoja na afya ya mama na
mtotom,utunzaji umbuumbu ,eimu ya miopo,vifaa na tenoojia ambapo pia
wameungana na maundi maaum waemavu ambao wapo nao wenye programu hiyo.
Amesema,Sherehe hizo zitafanyika
Septemba 29 mwaka huu ambapo watakuwa na matembezi ya Hisani kutoka
ukumbi wa Halmashauri mpaka kwenye viwanja vya maonesho huku mgeni rasmi
akitarajiwa kuwa Waziri wa Maendeeo ya Jamii,Jinsia na Maundi Maalum
Dkt.Dorothy Gwajima huku uzinduzi wa proramu hiyo ukipangwa kutafanyia Otoba 30 mwa TAWOMA enezeni elimu ya uchimbaji kwa vijana wa kikeKatika sherehe hizo mgeni rasmi atazindua na kumvisha taji malkia wa Madini Tanzania 2023.
No comments:
Post a Comment