MURUGNZI Muu wa REA Hassan Saidy aizungumza na waandishi wa habari moani Geita wenye maonesho ya Sita ya imataifa. |
Na Joyce Kasiki,Geita
SERIKALI
kupitia Wakala wa Nishati vijijini (REA) umefanikiwa kufikisha nishati
ya umeme vijijini katika vijiji 10,987 ambayo karibu asilimia 89 ya
vijiji vyote 12318 vilivyopo hapa nchini vimeshafikiwa na umeme.tu
ambavyo baadhi yake wakandarasi wapo saiti wanaendelea na kazi.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya Sita ya Kimaitfa ya Madini mkoani Geita,Mkurugenzi Mkuu wa REA Mhandisi Hassan Saidy amesema
matarajio mpaka mwakani vijiji vyote vitakuwa vimeshafikiwa na umeme
lakini vijiji vingi vitapata umeme kabla ya desemba mwaka huu na
vingine mwakani.
“Kwa hiyo tukimaliza zoezi la
kupeleka umeme vijijini tunahamia kwenye vitongoji ingawa mradi ya
kupeleka umeme kwenye vitongoji tulikuwa tumeshauanza .”amesema
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi huyo ,Tanzania Bara ina vitongoji 64,760 ambapo
karibu vitongoji 28586 vimeshafikiwa na umeme kwa hiyo utakuja kuona
kuna vitoingoji 36,000 ndio bado havijafikiwa na umeme.
“Kama
mnavyofahamu Tanzania tumebarikiwa nchi yetu ni kubwa ,Tanzania peke
yake ukijumlisha Kenya, Uganda , Ruanda na Burundi yaani Afrika
Mashariki ya mwanzo,bado Tanzania ni kubwa lakini serikali imeweza
kufikisha umeme kwenye eneo lote la nchi.”amesema na kuongeza kuwa
“Kwa
hiyo suala la umeme kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa na sasa hivi kama
unavyoona pamoja na kushughulika na umeme tunaingia kwenye nishati safi
ya kupikia .”
Mwishoni mwa mwaka juzi Rais
alizindua kongamano la Nishati ya kupikia ambapo katika kikao hicho
aliagiza kuanzishwa kwa dira ya Taifa na Mfuko wa Taifa wa Nishati ya
kupikia lengo lilikuwa ni kwa ajili ya kuhama kutoka kwenye njia na
nishati ya asili ya kupikia kuja kwenye nishati safi na bora ya kupikia.
Kufuatia
uzinduzi huo REA tumekuwa tukielimisha wananchi nchi nzima kuachana na
matumizi ya kuni na mkaa ambavyo vimekuwa ni chanzo cha ukataji miti
hovyo na hivyo kufanya uharibifu wa mazingira.
Amesema,wamekuwa
wakielimisha wananchi kuhusu athari na faida za matumizi ya nishati
safi ya kupikia huku akisema madhara ni kusababisha uharibifu wa
mazingira na kuleta mabadiliko ya Tabianchi .
Vile vle amesema zipo athari za kiafya ikiwa ni pamoja na macho kuwa mekundu,athari kwa akina mama wajawazito lakini pia vifo .
“Kwa
hiyo maeneo mengi hapa nchini tunaweza kuhama kwenye matumizi ya kuni
na mkaa na kuingia kwenye nishati safi ya kupikia ambayo pia inasadia
kuokoa misitu yetu ambayo wataalam wanatuambia tunapoteza misitu ya heka
laki nne kwa mwaka lakini pia kuna vifo vinavyoadiriwa kufikia wastani
wa 33,000 kwa mwaka kutokana na matumizi ya nishati ya kuni,
“Lakini
pia bado kuna madhara mengine ya kiafya,mtu anaweza asife lakini kuna
kuathirika macho,akina mama wajawazito wanaathirika lakini tuseme ni
jambo ambalo lina athari kubwa sana .”amesisitiza
Amesema
wakati umefika sasa kwa wananchi kuachana kupikia kuni na mkaa na
kuhamia kwenye nishati safi ya kupikia kama vile gesi,umeme kwani
serikali imeshaweka miundombinu hiyo.
No comments:
Post a Comment