Matukio katika picha ni wageni mbaimbai waliofika katika banda la NIC katika maonesho ya Madini Mkoani Geita katika Hamashauri ya mji wa Geita |
Na Joyce Kasiki,Geita
WACHIMBAJI wa madini nchini wameaswa kukatia Bima mitambo wanayotumia katika shughuli zao za uchimbaji ili pale inapotokea imeharibika ili waweze kutengenezewa bila kuathiri shughuli zao za uchimbaji.
Akizungumza katika maonesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili halimashauri ya mji wa Geita,Meneja wa Shirika la Bima (NIC) kanda ya ziwa Stella Marwa amesema kuwa bado hakuna muamko kwa wachimbaji wa Madini kukata Bima.
“Kwa hiyo kutokana na muamko mdogo kwa wachimbaji kukata Bima,tumeona tushiriki maonesho haya ili tuweze kutoa elimu ya Bima kwa wachimbaji na wananchi wote ili waweze kukata bima kwa ajli ya kujihakikishia usalama wao.”amesema na kuongeza kuwa
“Kwa mfano kuna bima ya ajali ambayo humsaidia mchimbaji pale ambapo anaweza kupata madhara katika shughuli zake za uchimbaji hivyo NIC kupitia bima yake ya ajali kwa ajili ya wachimbaji itaweza kumrudisha katika hali yake ya kawaida na endapo itatokea bahati mbaya amefariki warithi wake wanaweza kufidiwa na kuendeleza shughuli zao zakiuchumi.”
Ameongeza
kuwa mbali kutoa bima elimu ya bima hizo pia wanatoa elimu ya bima ya maisha
ambayo ina uwekezaji ndani na ulinzi ndani ambayo inamhakikishia mchimbaji au
mtu mwingine yeyote kuwa ukipatwa na janga lolote lile familia ikiwemo watoto
wataendelea kusoma.
"Pia katika maonesho haya tumekuja kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto kama magari,pikipiki na bajaji tunatoa elimu hii ili hao wasafirishaji waweze kukata bima hizo na kuepusha ajali ambazo zinaweza kuwatokea ikapelekea hayo magari yao kutokutengenezeka kabisa sababu yakutokuwa na bima wakikata bima na NIC Insurrance tutawalipa ndani ya siku saba na taratibu zote tunafanya kulingana na miongozo na zakumkatia ndiyo maana tunalipa ndani ya siku saba"amesema Marwa.
Aidha ameongeza kuwa NIC wameweza kufanya mabadiliko makubwa kwa kipindi kifupi ambapo wanatembea kifua mbele kuwa wana uwezo wakulipa madai ndani ya siku saba.
Aidha ametoa wito kwa wakazi wa Geita katika kipindi hiki cha maonesho kutembelea banda hilo kupata elimu mbalimbali kuhusu bima.
No comments:
Post a Comment