Nguvu Moja Security yajivunia mafanikio yake

 




              Na Joyce Kasiki,Geita

KAMPUNI ya Ulinzi ya Nguvu Moja security services limited inayojishughulisha na masuala ya ulinzi imeelezea mafanikio ya kampuni hiyo ikiwa ni pamoja kupata tuzo ya kampuni bora inayozingatia masuala ya afya na usalama mahala pa kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya  sita ya teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili  Mtu wa Utawala wa kampuni hiyo Kelvin Steven amesema,tuzo hizo wamepata kutoka Kwa  Wakala wa Afya na Usalama mahala pa Kazi (OSHA) 2022 na 2023.

Amesema kampuni yao inafanaya kazi zake kwa viwango vya Kimataifa kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wateja wake katika masuala ya ulinzi.

Kwa upande wake Meneja Mikataba wa Nguvu Moja  security services limited Jacob Zakaria  Amesema kampuni ina miaka 14 tangu kuanzishwa kwake na katika kipindi chote hicho hadi sasa imeendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake.

Kwa mujibu wa Jacob Amesema kuwa  watumishi katika kampuni hiyo  inayojumuisha wastaafu kutoka katika vikosi maalum hapa nchini pamoja na vijana kutoka Jeshi la Kujenga Taifa na watu wengine wakawaida ambao wanapewa mafunzo ya kitalaam lakini wengine wanakuwa wafanyakazi wakawaida .

Pia kampuni imekuwa ikitoa mafunzo kwa vijana kwa wiki tatu kwa ajili ya kuwajenga na kuwapa uelewa wa kazi ambayo wanakwenda kuifanya lakini pia kampuni imekuwa ikiendelea kuzingatia masuala mbalimbali ya viwango vya kiutendaji kazi katika sehemu za kazi .

Naye Meneja wa Usalama Mahala pa Kazi wa Nguvu Moja  security services limited Caroline Mushi Amesema wamekuwa wakifanya vipimo kwa wafanyakazi wao vya mara kwa mara kutokana na mazingira ya migodini kuwa na vihatarishi vingi kwa afya za binadamu.

“Askari anapoajiriwa lazima apimwe afya wakati anaanza kazi , lakini pia baada ya mwaka mmoja anapimwa tena afya yake pia anapoondoka labda anataka kwenda kusoma lazima apime afya yake na hii yote ni kutokana kwamba maeneo tunayofanya kazi hasa migoni ni eneo lenye vihatarishi vingi kwa hiyo ni lazima tujue afya ya askari wetu.”amesema Mushi

Caroline  amesema,kampuni hiyo inatoa mafunzo mbalimbali kwa askari wake ili kutambua vihatarishi mahala pa kazi ili aweze kukitoa ama kutoa taarifa ili kihatarishi hicho kitolewe kama hawezi,lakini pia tunatoa mafunzo ya zimamoto ili waweze kukabiliana na 

majanga ya moto pindi yanapotokea katika maeneo yao ya kazi lakini pia tunatoa mafunzo ya huduma ya kwanza kwa askari wetu ili waweze kusaidiana kazini kabla ya kufika hospitali .

Kwa upande wake Meneja wa Oparesheni wa Nguvu Moja Desdery Kelvin amesema,askari wao wamewagawa katika makundi matatu ambapo wapo askari wa eneo ,askari wanaokuwa katika chumba maalum cha kamera kwa ajili ya ulinzi wa eneo kubwa viwandani pamoja na askari wa matukio.

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.